2018
Furaha: Ni Zaidi ya Hali
April 2018


Furaha: Ni Zaidi ya Hali

Picha
happy breakfast plate

Tunafundishwa kwamba kuwa na furaha ni lengo la kuwepo kwetu (ona 2 Nefi 2:25). Hivyo kwa nini furaha wakati mwingine huonekana ngumu kupata? Pengine ni kwa sababu hatuelewi furaha hasa ni kitu gani … na kitu gani siyo furaha

Furaha Ni Nini?

Katika kiwango rahisi, furaha ni kimo cha hali yako ya kiakili katika hatua kubwa kuliko ile ya usawa wako wa mhemko wa kawaida.1 Kwa maneno mengine, inamaanisha kujisikia vizuri.

Kuna njia nyingi za kuchochea mhemko wa juu—kufanya utani na rafiki, kucheza mchezo wa kufurahisha, au hata kula kipande cha keki ya siagi—lakini kamwe haiwezi kudumu kwa muda mrefu. Mara nyingi tunaishia kuruka kutoka chanzo kimoja cha furaha kwenda kingine katika jaribio la kupata tena mhemko wa juu. Lakini si kuna furaha inayodumu?

Ndiyo—lakini ni vigumu kutambua kuliko unavyofikiria, ndiyo sababu mara nyingi tunakosa alama. Ulimwengu hutuambia kwamba maisha mazuri lazima yajazwe na matukio, kwamba maisha yako yanapaswa kuwa na msisimko usio na kikomo kuteremka kwa urahisi, barabara iliyojaa raha. Lakini ukweli ni kwamba, huitaji msisimko wa kudumu ili uishi “kwa furaha” (2 Nefi 5:27). Furaha ya kudumu—ile tunayoweza kuita furaha ya kweli —ni hisia tulivu zaidi, imara ya hali njema kuliko hisia ya kawaida ya wingi wa raha. Burudani na raha hufifia, lakini furaha ya kweli siyo hali inayopita—inadumu kwa muda mrefu zaidi. Kama kupata furaha ni kuinua hisia zako juu ya usawa, kupata furaha ya kweli ni kama kuinua usawa wenyewe.2

Unaweza kudhani kwamba furaha imara huhitaji mafanikio imara na uhuru kutokana na maumivu na majaribu. Lakini tafiti zinaonyesha kwamba hali nzuri sio kigezo cha furaha, na hali mbaya haziwezi kuiua. Badala yake, kati ya hali zote zinazoathiri furaha yako, chaguzi zako zina baadhi ya nguvu kubwa3 Mzee Ulisses Soares wa Urais wa Sabini alifundisha, “Furaha hutathiminiwa na mazoea, tabia, na mpangilio wa mawazo ambayo tunaweza kuyashughulikia moja kwa moja kwa matendo ya makusudi.” Furaha ni zaidi ya hali nzuri au maisha ya kutojali—ni njia ya kufikiria na kuishi ambayo tunaweza kuitawala. Viwango vya hali kwa ujumla hakika huathiriwa na vinasaba na makuzi yetu, lakini chaguzi zetu binafsi huchukua jukumu muhimu. Kwa ufupi, “furaha ni uchaguzi ambao yeyote anaweza kuufanya.”4

Je, Ninawezaje Kuwa na Furaha?

Hivyo ni kwa jinsi gani hasa “tunachagua” kuwa na furaha? Je, ni kiungo gani cha siri kwa ajili ya keki ya siagi yetu ya furaha? Kama Mzee Soares alivyoelezea, furaha ya kweli huhitaji “juhudi za-muda mrefu kwa ajili ya kitu muhimu zaidi katika maisha.” Vivyo hivyo, Viktor Frankl, mtu maarufu aliyenusurika maangamizi makuu na mtaalamu wa tiba ya magonjwa ya akili, alishauri kwamba furaha ni “matokeo ya kujitoa kwa mtu binafsi katika sababu iliyo kuu kuliko yeye mwenyewe.”5

Na nini kinaweza kuwa sababu kuu kuliko ile ambayo Mungu ameiweka kwa ajili yetu? Katika utafutaji wetu wa furaha, hatuhitaji kuangalia mbali zaidi kuliko mpango wa Baba wa mbinguni. Hata hivyo, unaitwa “mpango wa furaha” kwa sababu fulani! (Alma 42:8, 16.). Andiko baada ya andiko hushuhudia kwamba kufuata mpango wa Mungu kunaleta furaha (ona 2 Nefi 2:13; Helamani 13:38). Japokuwa kuishi kwa haki hakutatuokoa kutoka kila maumivu ya moyo, kutatuweka katika nafasi ambapo tunaweza kupata uzoefu zaidi wa furaha katika maisha haya, na kutuongoza kwenye kuinuliwa kwetu na shangwe ya milele katika ulimwengu ujao.

Kama vile imani, furaha inaweza kudhoofishwa au kuimarishwa, kutegemeana na matendo yako. Kama ukitumia muda wako kutafuta vicheko na viburudisho vya muda mfupi, furaha yako ita “chukuliwa na kila upepo” (Waefeso 4:14). Lakini kama utajitahidi kuishi kwa haki, utatengeneza hali imara ya amani na afya ambayo inaweza kuepuka dhoruba yoyote. Na unapoipa kipaumbele imani kuliko burudani, unaweza kugundua shangwe halisi—aina inayoweza kupatikana tu kwa “anayetubu na kutafuta furaha kwa unyenyekevu” (Alma 27:18).

Muhtasari

  1. Ona Carolyn Gregoire, “Huu Ni Ushahidi wa Kisayansi Kwamba Furaha ni Uchaguzi,” HuffPost, Dec. 13, 2013, huffingtonpost.com/2013/12/09/scientific-proof-that-you_n_4384433.html.

  2. Ona Alex Lickerman, “Jinsi ya Kuseti Upya Pointi Yako ya Furaha,” Saikolojia Leo, Apr. 21, 2013, psychologytoday.com/blog/happiness-in-world/201304/how-reset-your-happiness-set-point.

  3. Ona Michael Mendelsohn, “Saikolojia Chanya: Sayansi ya Furaha,” ABC News, Jan. 11, 2008, abcnews.go.com/Health/story?id=4115033&page=1.

  4. Carolyn Gregoire, “Huu Ni Ushahidi wa Kisayansi Kwamba Furaha ni Uchaguzi.”

  5. Viktor E. Frankl, Utafutaji wa Mwanadamu juu ya Maana (1984), 17.