Mosia 16
iliyopita inayofuata

Mlango wa 16

Mungu hukomboa wanadamu kutoka hali yao ya kuanguka—Wale ambao wana tamaa za kimwili wanaishi kama kwamba hakuna ukombozi—Kristo husababisha kutimizwa ufufuo kwa maisha ya milele au laana ya milele. Karibia mwaka 148 K.K.

1 Na sasa, ikawa kwamba baada ya Abinadi kuzungumza maneno haya alinyosha mkono wake na kusema: Wakati utakuja ambapo wote wataona awokovu wa Bwana; wakati kila taifa, kabila, lugha, na watu wataona ana kwa ana na bkutubu kwa Mungu kwamba hukumu zake ni za haki.

2 Na kisha waovu awatatupwa nje, na watakuwa na sababu ya kupiga makelele, na bkulia, na kuomboleza, na kusaga meno yao; na haya ni kwa sababu hawakutii sauti ya Bwana; kwa hivyo Bwana hatawakomboi.

3 Kwani wana atamaa na uibilisi, na bibilisi ana uwezo juu yao; ndiyo, hata yule nyoka wa kale caliyewadanganya wazazi wetu wa kwanza, ambayo ilikuwa ni sababu ya dkuanguka kwao; ambayo ni sababu ya wanadamu wote kuwa na tamaa, tamaa za kimwili, uibilisi, ekujua uovu na wema, na kujitolea kwa ibilisi.

4 Hivyo wanadamu wote awalipotea; na tazama, wangekuwa wamepotea daima kama sio kwamba Mungu aliwakomboa watu wake kutoka hali yao ya upotevu.

5 Lakini kumbuka kwamba yule anayeendelea na kufuata hali yake ya atamaa, na kuendelea katika njia za dhambi na kumuasi Mungu, hubaki katika hali yake ya kuanguka na ibilisi ana uwezo wote juu yake. Kwa hivyo kwake yeye ni kama bukombozi haukufanywa, akiwa adui kwa Mungu; na pia ibilisi ni adui wa Mungu.

6 Na sasa kama Kristo hangekuja ulimwenguni, akizungumza kuhusu vitu vitakavyokuja akama tayari vimeshakuja, hakungekuwa na ukombozi.

7 Na kama Kristo hangefufuka kutoka kwa wafu, au kuvunja kamba za kifo kwamba kaburi lisiwe na ushindi, na kwamba kifo kisiwe na auchungu, hakungekuwa na ufufuo.

8 Lakini kuna aufufuo, kwa hivyo kaburi halina ushindi, na uchungu wa bkifo umemezwa katika Kristo.

9 Yeye ni anuru na uzima wa ulimwengu; ndiyo, nuru isiyo na mwisho, ambayo haiwezi kuwekwa giza; ndiyo, na pia uzima usio na mwisho, kwamba hakutakuwa tena na kifo.

10 Hata huu mwili wenye kufa utajivika akutokufa, na hii iharibikayo itavaa isiyoharibika, na italetwa bkusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu, ckuhukumiwa na yeye kulingana na matendo yao kama ni mema au kama ni maovu—

11 Kama ni wema, watafufuliwa katika maisha na furaha aisiyo na mwisho; na kama ni waovu, watafufuliwa katika laana ya bmilele, na kuwekwa kwa ibilisi, ambaye amewatawala, ambayo ni laana—

12 Kwa vile walienda kulingana na nia zao za tamaa na tamaa za kimwili; wakiwa wamekosa kumlingana Bwana waliponyoshewa mikono ya rehema; kwani walinyoshewa mikono ya arehema, na hawakukubali; wao wakiwa wameonywa kuhusu uovu wao lakini hawakuuacha; na waliamriwa watubu lakini hawakutubu.

13 Na sasa, haiwapasi ninyi kutetemeka na kutubu dhambi zenu, na kukumbuka kwamba ni kwa na katika Kristo pekee mnakoweza kuokolewa?

14 Kwa hivyo, kama mnafundisha asheria ya Musa, fundisheni pia kwamba ni kivuli cha vile vitu vitakavyokuja—

15 Wafundishe kwamba ukombozi huja kwa Kristo aliye Bwana, ambaye ni aBaba kamili hasa wa Milele. Amina.