Maandiko Matakatifu
3 Nefi 24


Mlango wa 24

Mjumbe wa Bwana atatayarisha njia kwa Ujio wa Pili—Kristo ataketi kwenye hukumu—Israeli inaamrishwa kulipa zaka na matoleo—Kitabu cha ukumbusho kinahifadhiwa—Linganisha Malaki 3. Karibia mwaka 34 B.K.

1 Na ikawa kwamba aliwaamuru kwamba waandike maneno ambayo Baba alimkabidhi Malaki, ambayo angewaambia. Na ikawa kwamba baada ya kuandikwa, aliyaeleza. Na haya ndiyo maneno aliyowaambia akisema: Baba alimwambia Malaki hivi—Tazama, nitamtuma amjumbe wangu, na atatayarisha njia kabla yangu, na Bwana mnayemgojea atakuja kwa ghafla kwenye hekalu lake, hata yule mjumbe wa agano ambaye mnafurahia ndani; tazama atakuja, asema Bwana wa Majeshi.

2 Lakini ni nani aatakayestahili siku ya kuja kwake, na ni nani atakayesimama atakapotokea? Kwani yeye yuko kama moto busafishao fedha, na kama sabuni ya dobi.

3 Na ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, na atawatakasa awana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha, ili dhabihu kwa Bwana liwe btoleo kwa haki.

4 Ndipo dhabihu ya Yuda na Yerusalemu zitapendeza mbele ya Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani.

5 Na nitawakaribia kwa hukumu; na nitakuwa shahidi mwepesi dhidi ya wachawi, na dhidi ya wazinzi, na dhidi ya waapao uwongo, na dhidi ya wale wamwoneao mwenye kuajiriwa kwa ajili ya mshahara wake, mjane na ayatima, na wale wanaompoteza mgeni, na hawaniogopi, asema Bwana wa Majeshi.

6 Kwa kuwa mimi ni Bwana, sibadiliki; kwa hivyo enyi wana wa Yakobo hamwangamizwi.

7 Hata kutoka siku za babu zenu, ammegeuka upande kutoka kwa maagizo yangu, na hamjayashika. bNirudieni na nitarudi kwenu, asema Bwana wa Majeshi. Lakini ninyi mwasema: Tutarudi kwa namna gani?

8 Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini mmeniibia. Lakini mnasema: Tumekuibia kwa namna gani? Katika azaka na bmadhabihu.

9 Mmelaaniwa na laana, kwani mmeniibia, hata hili taifa lote.

10 Leteni azaka kamili ghalani, ili kuweko chakula katika nyumba yangu; na mnijaribu sasa hivi, asema Bwana wa Majeshi, kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagia bbaraka, kwamba kusiwe na nafasi ya kutosha ya kuipokea.

11 Na nitamkemea mlaji kwa ajili yenu, na hataharibu matunda ya ardhi yenu; wala mizabibu wenu hautapukutisha matunda yake katika ardhi kabla ya wakati wake huko shambani, asema Bwana wa Majeshi.

12 Na mataifa yote yatawaita wenye heri, kwani mtakuwa nchi ya kupendeza, asema Bwana wa Majeshi.

13 Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema Bwana. Lakini mnasema: Tumesema nini dhidi yako?

14 Mmesema ni bure kumtumikia Mungu, na tumepata faida gani kwa kuzishika ibada zake, na kwamba tumetembea kwa huzuni mbele ya Bwana wa Majeshi.

15 Na sasa tunawaita wenye kiburi ndiyo walio heri; ndiyo, wale wanaotenda maovu na kunufaika; ndiyo, wanaomjaribu Mungu ndiyo wanaookolewa.

16 Ndipo wale wanaomcha Bwana, awalisemezana wao kwa wao, na Bwana akasikiliza na kusikia; na bkitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele yake kwa wao wanaomcha Bwana, na kulitafakari jina lake.

17 Na watakuwa wangu, asema Bwana wa Majeshi, katika siku ile anitakapofanya vito vyangu; na nitawaachilia vile mtu huachilia mwana wake amtumikiaye.

18 Ndipo mtakaporudi, na akupambanua miongoni mwa wenye haki na waovu, na miongoni mwa yule amtumikiaye Mungu na yule asiyemtumikia.