Maandiko Matakatifu
3 Nefi 13


Mlango wa 13

Yesu anawafundisha Wanefi Sala ya Bwana—Wanahitaji kuweka hazina zao mbinguni—Wale wanafunzi kumi na wawili katika huduma yao wanaamriwa kutofikiria vitu vya kidunia—Linganisha Mathayo 6. Karibia mwaka 34 B.K.

1 Amin, amin, nawaambia kwamba toeni asadaka zenu kwa masikini; lakini chungeni kwamba msitoe sadaka zenu mbele ya watu kwa kuonekana nao; la sivyo hamna thawabu ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni.

2 Kwa hivyo, wakati mtakapotoa sadaka zenu msivumishe tarumbeta mbele yenu, vile wanafiki hufanya kwenye masinagogi na katika barabara, ili wapate akutukuzwa na watu. Amin nawaambia, wana thawabu yao.

3 Lakini unapotoa sadaka acha mkono wako wa kushoto usijue vile mkono wa kulia unafanya;

4 Ili sadaka zenu ziwe katika siri; na Baba yenu ambaye huona kwa siri, mwenyewe atawalipa wazi.

5 Na wakati amnaomba hamtafanya kama wanafiki wanavyofanya, kwani wanapenda kuomba, wakisimama ndani ya masinagogi na kwenye pembe za barabara, ili waonekane na watu. Amin ninawaambia, wanayo thawabu yao.

6 Lakini wewe, unaposali, ingia kwenye chumba chako kidogo, na wakati umefunga mlango wako, sali kwa Baba yako ambaye yuko mafichoni; na Baba yako, ambaye huona kisiri, atakulipa wazi.

7 Lakini wakati unasali, usitumie marudio ya bure, kama walimwengu, kwani wanadhani kwamba watasikika kwa kutumia maneno mengi.

8 Kwa hivyo usiwe kama hao, kwani Baba yako aanajua ni vitu gani unavyohitaji kabla ya wewe kumwuliza.

9 Kwa hivyo amsali kwa bnjia hii: cBaba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.

10 Mapenzi yako yatimizwe duniani vile yalivyo mbinguni.

11 Na utusamehe deni zetu, kama tunavyowasamehe wadeni wetu.

12 Na ausituongoze kwenye majaribu, lakini utuokoe kutoka kwa maovu.

13 Kwani ufalme ni wako, na uwezo, na utukufu, milele. Amina.

14 Kwani, ikiwa amtasamehe watu makosa yao Baba yenu wa mbinguni atawasamehe pia.

15 Lakini kama hamtawasamehe watu makosa yao Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.

16 Tena amnapofunga msiwe kama wanafiki, wenye nyuso za kuhuzunika, kwani hukunja nyuso zao ili waonekane wanafunga. Amin ninawaambia, wanayo thawabu yao.

17 Lakini wewe, unapofunga, paka mafuta kwa kichwa chako, na unawe uso wako;

18 Ili usionekane na watu kama unafunga, lakini kwa Baba yako, aliye sirini; na Baba yako, ambaye huona asirini, atakupatia zawadi wazi.

19 Msijiwekee hazina duniani, ambapo nondo na kutu huozesha, na wezi wanavunja na kuiba;

20 Lakini mjiwekee ahazina zenu mbinguni, ambapo nondo wala kutu haziozeshi, na ambapo wezi hawawezi kuvunja na kuingia wala kuiba.

21 Kwani mahali ambapo hazina yako ipo, pale pia moyo wako utakuwa.

22 aNuru ya mwili ni jicho; kwa hivyo, ikiwa jicho lako liko moja, mwili wako wote utajaa nuru.

23 Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote utajaa giza. Kwa hivyo, ikiwa nuru iliyopo ndani yako itakuwa giza, sio hio ni giza kuu!

24 Hakuna mtu ambaye anaweza akutumikia mabwana wawili; kwani labda atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au kama sivyo atampenda mmoja na kumdhulumu mwingine. Huwezi kumtumikia Mungu na Mali.

25 Na sasa ikawa kwamba wakati Yesu alipokuwa amezungumza maneno haya alielekeza macho juu ya wale kumi na wawili ambao alikuwa amewachagua, na akawaambia: Kumbukeni maneno ambayo nimezungumza. Kwani tazama, ni ninyi ambao nimechagua akuwahudumia hawa watu. Kwa hivyo ninawaambia, bmsisumbukie maisha yenu, ni nini mtakula, au ni nini mtakunywa; wala mtavaa nini, kwenye miili yenu. Je, si maisha yako zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

26 Tazama ndege wa angani, kwani hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi kwenye maghala; lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, si ninyi ni bora kuliko wao?

27 Ni nani kati yenu kwa kufikiria anaweza kuongeza mkono mmoja kwa urefu wake?

28 Na kwa nini msumbuke kwa mavazi? Fikirieni maua ya mwituni vile yanakua; hayafanya kazi, wala hayasokoti;

29 Na bado ninawaambia, kwamba hata Sulemani, kwa enzi yake yote, hakupambwa kama moja ya hawa.

30 Kwa hivyo, ikiwa Mungu anavika nyasi ya shambani, ambayo ipo leo, na kesho itatupwa kwenye jiko, hata hivyo atakuvisha, ikiwa huna imani ndogo.

31 Kwa hivyo msisumbuke, mkisema, Tutakula nini? au, Tutakunywa nini? au, Tutavaa nini?

32 Kwani Baba yenu wa mbinguni anajua kwamba mna mahitaji ya hivi vitu vyote.

33 Lakini tafuteni kwanza aufalme wa Mungu na haki yake, na hivi vitu vyote vitaongezwa kwenu.

34 Kwa hivyo msisumbuke kwa kesho, kwani kesho itajishugulisha na vitu vyake yenyewe. Kila siku ina maovu yake ya kutoshana nayo.