Maandiko
3 Nefi 14


Mlango wa 14

Yesu anaamuru: Msihukumu; ombeni Mungu; jihadhari na manabii wa uwongo—Anaahidi wokovu kwa wale wanaotenda nia ya Baba—Linganisha Mathayo 7. Karibia mwaka 34 B.K.

1 Na sasa ikawa kwamba wakati Yesu alipokuwa amezungumza maneno haya aligeuka tena akaelekea umati, na kufungua kinywa chake kwao, na kusema: Kweli, kweli, ninawaambia, aMsihukumu, kwamba msije mkahukumiwa.

2 aKwani kwa hukumu mnayo hukumia, mtahukumiwa nayo; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa tena.

3 Na mbona wakitazama kibanzi ambacho kiko ndani ya jicho la ndugu yako, lakini hufikirii kiboriti ambacho kiko kwenye jicho lako?

4 Au utasemaje kwa ndugu yako: Acha nitoe kibanzi ndani ya jicho lako—na tazama, kiboriti kiko ndani ya jicho lako?

5 Wewe mnafiki, kwanza ondoa akiboriti kutoka kwenye jicho lako; na ndipo utaona vema kukitoa kibanzi kutoka ndani ya jicho la ndugu yako.

6 Msitoe kile kilicho akitakatifu kwa mbwa, wala msitupe lulu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, na kugeuka tena na kuwararua.

7 aOmbeni, na mtapewa; tafuteni na mtapata, bisheni, na mtafunguliwa.

8 Kwani kila mmoja ambaye huuliza, hupata; na yule anayetafuta, huvumbua; na yule ambaye hubisha, hufunguliwa.

9 Au kuna mtu gani kwenu, ambaye, ikiwa mwana wake anamwomba mkate, atampatia jiwe?

10 Au kama anamwomba samaki, atampatia nyoka?

11 Ikiwa ninyi, mkiwa waovu, mnajua kuwapatia watoto wenu zawadi nzuri, je, ni vipi Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale ambao humwomba?

12 Kwa hivyo, vitu vyote ambavyo mngetaka kwamba watu wawafanyie, awafanyie pia wengine, kwani hii ni sheria na manabii.

13 Ingieni kwa kupitia amlango mwembamba; kwani mlango ni wazi, na bpana ndiyo njia iongozayo kwenye uharibifu, na waiendayo ni wengi;

14 Kwa sababu amlango umesonga, na njia ni bnyembamba, iendayo uzimani, nao waipatao ni cwachache.

15 Jihadharini na amanabii wa uwongo, ambao huwajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali.

16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je, watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

17 Hata hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; lakini mti mwovu huzaa matunda mabaya.

18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya wala mti mbaya kuzaa matunda mema.

19 Kila mti ambao ahauzai matunda mazuri hukatwa, na kutupwa motoni.

20 Kwa hivyo, kwa amatunda yao mtawajua.

21 Sio kila anayesema kwangu, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; lakini yule anayefanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi awatasema kwangu siku ile: Bwana, Bwana, si tulifanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako si tumetoa pepo wachafu, na katika jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Na ndipo nitawaambia dhahiri: aSikuwajua ninyi kamwe; bondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

24 Kwa hivyo, yeyote asikiaye maneno haya yangu na kuyafanya, nitamfananisha na mtu mwenye hekima, ambaye alijenga nyumba yake juu ya amwamba

25 Na amvua ilinyesha, na mafuriko yakaja, na pepo zikavuma, na zikapiga ile nyumba; na bhaikuanguka, kwani iliwekwa kwenye mwamba.

26 Na yeyote asikiaye maneno haya yangu na hayafanyi atalinganishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya amchanga

27 Na mvua ilinyesha, na mafuriko yakaja, na pepo zikavuma, na zikaipiga ile nyumba; na ilianguka, na mwanguko wake ulikuwa mkubwa.