Maandiko Matakatifu
Etheri 12


Mlango wa 12

Nabii Etheri anawasihi watu waamini katika Mungu—Moroni anasimulia maajabu na miujiza inayofanywa kwa imani—Imani ilimwezesha kaka wa Yaredi kumwona Kristo—Bwana huwapa watu udhaifu ili wawe wanyenyekevu—Kaka wa Yaredi aliusogeza mlima Zerini kwa imani—Imani, tumaini, na hisani ni muhimu kwa wokovu—Moroni alimwona Yesu uso kwa uso.

1 Na ikawa kwamba siku za Etheri zilikuwa katika siku za utawala wa Koriantumuri; na aKoriantumuri alikuwa mfalme wa nchi yote.

2 Na aEtheri alikuwa nabii wa Bwana; kwa hivyo Etheri alijitokeza katika siku za Koriantumuri, na akaanza kutabiri kwa watu, kwani hangeweza bkuzuiliwa kwa sababu ya Roho wa Bwana ambayo ilikuwa ndani yake.

3 Kwani aalihubiri kutoka asubuhi, hata mpaka kwenda chini kwa jua, akihimiza watu kuamini katika Mungu kwenye toba wasije bwakaharibiwa, na akiwaambia kwamba kwa cimani vitu vyote hutimizwa—

4 Kwa hivyo, yeyote aaminiye katika Mungu angeweza kwa hakika akutumaini ulimwengu bora, ndiyo, hata mahali katika mkono wa kulia wa Mungu, tumaini ambalo huja kutokana na imani, hutengeneza bnanga kwa roho za watu, ambayo ingewafanya kuwa imara na thabiti, wakizidi sana kutenda ckazi njema, wakiongozwa dkumtukuza Mungu.

5 Na ikawa kwamba Etheri alitabiri vitu vikubwa vya ajabu kwa watu, ambavyo hawakuamini, kwa sababu hawakuviona.

6 Na sasa, mimi, Moroni, nitazungumza machache kuhusu vitu hivi; ninataka kuonyesha ulimwengu kwamba aimani ni vitu ambavyo bvinatumainiwa na chavionekani; kwa hivyo, msishindane kwa sababu hamwoni, kwani hamtapata ushahidi wowote mpaka baada ya dmajaribu ya imani yenu.

7 Kwani ilikuwa kwa imani kwamba Kristo alijionyesha kwa babu zetu, baada ya kuamka kutoka kwa wafu; na hakujionyesha kwao mpaka walipokuwa na imani ndani yake; kwa hivyo, lazima iwe kwamba wengine walikuwa na imani ndani yake, kwani hakujionyesha kwa ulimwengu.

8 Lakini kwa sababu ya imani ya watu amejionyesha kwa watu wa ulimwengu, na kulitukuza jina la Baba, na alitayarisha njia ambayo kwake wengine wangeshiriki kwa mwito wa zawadi ya mbinguni, kwamba wangetumainia vitu hivyo ambavyo hawajaviona.

9 Kwa hivyo, mnaweza kuwa pia na tumaini, na muwe washiriki wa zawadi, ikiwa mtakuwa tu na imani.

10 Tazama ilikuwa kwa imani kwamba wale wa kale awaliitwa kwa mpango mtakatifu wa Mungu.

11 Kwa hivyo, kwa imani, sheria ya Musa ilitolewa. Lakini katika kipawa cha Mwana wake Mungu ametayarisha njia abora zaidi; na ni kwa imani kwamba imetimizwa.

12 Kwani kama hakuna aimani miongoni mwa watoto wa watu, Mungu hawezi kufanya bmiujiza miongoni mwao; kwa hivyo, hakujionyesha mpaka baada ya imani yao.

13 Tazama, ilikuwa imani ya Alma na Amuleki ambayo ilisababisha agereza kuanguka chini.

14 Tazama, ilikuwa imani ya Nefi na Lehi ambayo ilileta amabadiliko juu ya Walamani, kwamba walibatizwa kwa moto na kwa bRoho Mtakatifu.

15 Tazama, ilikuwa imani ya aAmoni na ndugu zake ambayo bilileta muujiza mkuu miongoni mwa Walamani.

16 Ndiyo, na hata wote waliofanya amiujiza waliifanya kwa sababu ya bimani, hata wale walioishi kabla ya Kristo na pia wale waliokuwako baadaye.

17 Na ilikuwa kwa imani kwamba wale wanafunzi watatu walipata ahadi kwamba ahawangeona kifo; na hawakupokea ahadi hiyo mpaka baada ya wao kuwa na imani.

18 Na wala kwa muda wowote hakujawa na yeyote ambaye amefanya miujiza mpaka awe na imani; kwa hivyo waliamini kwanza katika Mwana wa Mungu.

19 Na kulikuwa na wengi ambao imani yao ilikuwa na nguvu sana, hata akabla ya Kristo kuja, ambao hawangeweza kuwekwa nyuma ya bpazia, lakini kwa ukweli waliona kwa macho yao vitu ambavyo walikuwa wameona kwa jicho la imani, na walifurahi.

20 Na tazama, tumeona katika maandishi haya kwamba mmoja wa hao alikuwa kaka wa Yaredi; kwani imani yake ilikuwa kubwa sana katika Mungu, kwamba Mungu alipoweka akidole chake mbele hakuweza kukificha kutoka kwa uwezo wa kuona wa kaka wa Yaredi, kwa sababu ya neno lake ambalo alikuwa amemzungumzia, neno ambalo alikuwa amepokea kwa imani.

21 Na baada ya kaka wa Yaredi kuona kidole cha Bwana, kwa sababu ya aahadi ambayo kaka wa Yaredi alikuwa amepata kwa imani, Bwana hangeweza kumzuia kuona chochote; kwa hivyo alimwonyesha vitu vyote, kwani hangeweza tena kuwekwa nje ya bpazia.

22 Na ni kwa imani kwamba babu zangu wamepata aahadi kwamba vitu hivi vitakuja kwa ndugu zao kupitia kwa Wayunani; kwa hivyo Bwana ameniamuru, ndiyo, hata Yesu Kristo.

23 Na nikasema kwake: Bwana, Wayunani watachekelea vitu hivi, kwa sababu ya aunyonge wetu katika maandishi; kwani Bwana umetufanya bwakubwa katika neno kwa imani, lakini hujatufanya wakubwa kwenye maandishi; kwani umefanya watu hawa wote kwamba wanaweza kusema sana, kwa sababu ya Roho Mtakatifu ambaye umewapatia.

24 Na umetufanya kwamba tuweze kuandika tu machache, kwa sababu ya mikono yetu kutokuwa miepesi. Tazama, hujatufanya mabingwa kwa auandishi kama kaka wa Yaredi, kwani ulimfanya ili vitu ambavyo aliandika viwe vikubwa hata vile wewe ulivyo, kwa kushinda mtu kuvisoma.

25 Umefanya pia maneno yetu yawe yenye nguvu na makubwa, hata kwamba hatuwezi kuyaandika; kwa hivyo, tunapoandika tunaona udhaifu wetu, na kuanguka kwa sababu ya upangaji wa maneno yetu; na ninaogopa Wayunani wasije awakacheka maneno yetu.

26 Na nilipokuwa nimesema hivi, Bwana alinizungumzia, akisema: Wajinga ahucheka, lakini wataomboleza; na neema yangu unatosha kwa walio wanyenyekevu, kwamba hawatafaidika na udhaifu wenu;

27 Na ikiwa watu watakuja kwangu nitawaonyesha audhaifu wao. bNinawapatia watu udhaifu ili katika udhaifu wao wawe wanyenyekevu; na cneema yangu inatosha watu wote ambao dhujinyenyekeza mbele yangu; kwani wakijinyenyekeza mbele yangu, na kuwa na imani ndani yangu, ndipo nitafanya vitu edhaifu kuwa vya nguvu kwao.

28 Tazama, nitawaonyesha Wayunani udhaifu wao, na nitawaonyesha kwamba aimani, tumaini na hisani huwaleta kwangu—chimbuko la haki yote.

29 Na mimi, Moroni, baada ya kusikia maneno haya, nilifarijika, na kusema: Ee Bwana, haki yako itafanyika, kwani najua kwamba unafanya miujiza kwa watoto wa watu kufuatana na imani yao;

30 Kwani kaka wa Yaredi alisema kwa mlima Zerini, aNenda—na ulisonga. Na ikiwa hangekuwa na imani haungesonga; kwa hivyo unafanya miujiza baada ya watu kuwa na imani.

31 Kwa njia hii ulijionyesha kwa wanafunzi wako; kwani baada ya wao kuwa na aimani, na kuzungumza katika jina lako, ulijidhihirisha kwao kwa uwezo mkuu.

32 Na ninakumbuka kwamba umesema kwamba umetayarisha anyumba kwa watu, ndiyo, hata miongoni mwa nyumba za Baba yako, ambamo kwake binadamu angekuwa na btumaini kamili; kwa hivyo lazima binadamu atumaini, au hatapokea urithi mahali ambapo umetayarisha.

33 Na tena, ninakumbuka kwamba umesema kwamba aunawapenda watu wote duniani, hata kwenye kuweka maisha yako chini kwa ajili ya walimwengu, ili ungeyachukua tena kutayarisha mahali kwa watoto wa watu.

34 Na sasa najua kwamba huu aupendo ambao umekuwa nao kwa watoto wa watu ni hisani; kwa hivyo, isipokuwa watu wawe na hisani hawawezi kurithi pale mahali ambapo umetayarisha nyumbani kwa Baba yako.

35 Kwa hivyo, ninajua kwa kitu hiki ambacho umesema, kwamba ikiwa Wayunani hawana hisani, kwa sababu ya unyonge wetu, kwamba utawahukumu, na kuchukua kutoka kwao atalanta zao, ndiyo, hata ile ambayo wamepokea, na uwapatie wale ambao watakuwa na nyingi zaidi.

36 Na ikawa kwamba niliomba kwa Bwana kwamba awape aneema Wayunani, ili wapate kuwa na hisani.

37 Na ikawa kwamba Bwana akasema nami: Kama hawana hisani haikuhusu wewe, umekuwa mwaminifu; kwa hivyo, nguo zako zitafanywa asafi. Na kwa sababu umeuona budhaifu wako utafanywa kuwa mwenye nguvu, hata kwa kukaa mahali ambapo nimepatayarisha katika nyumba ya Baba yangu.

38 Na sasa mimi, Moroni, ninaaga kwa Wayunani, ndiyo, na pia kwa ndugu zangu ambao ninawapenda, mpaka tutakapokutana mbele ya akiti cha hukumu cha Kristo, ambapo watu wote watajua kwamba bmavazi yangu hayajawekwa mawaa na damu yenu.

39 Na ndipo mtakapojua kwamba animemwona Yesu, na kwamba amenizungumzia buso kwa uso, na kwamba aliniambia katika unyenyekevu ulio wazi, hata vile mtu humwambia mwenzake kwa lugha yangu, kuhusu vitu hivi;

40 Na ni vichache tu ambavyo nimeandika, kwa sababu ya udhaifu wangu kwa kuandika.

41 Na sasa, nimekupendekeza akumtafuta huyu Yesu ambaye manabii na mitume wameandika kumhusu, kwamba neema ya Mungu Baba, na pia Bwana Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu, ambaye banashuhudia kwao, iwe na kuishi ndani yenu milele. Amina.