Maandiko Matakatifu
Alma 26


Mlango wa 26

Amoni anashangilia katika Bwana—Waaminifu hupewa nguvu na Bwana na kupewa ufahamu—Kwa imani binadamu wangewaleta watu wengi kutubu—Mungu ana uwezo wote na anafahamu vitu vyote. Karibia mwaka 90–77 K.K.

1 Na sasa, haya ndiyo maneno ya Amoni kwa ndugu zake, ambayo yanasema hivi: Ndugu zangu na jamaa zangu, tazama nawambia ninyi, ni sababu kiasi gani tunayo ya kutufanya tufurahi; kwani tungejuaje wakati atulipoanza safari yetu kutoka Zarahemla kwamba Mungu angetubariki sisi hivi kwa wingi?

2 Na sasa, nauliza, ni baraka gani kubwa ambayo ametupatia sisi? Mnaweza kunena?

3 Tazama, ninajibu kwa niaba yenu; kwani ndugu zetu, Walamani, walikuwa gizani, ndiyo, hata kwenye shimo la giza kubwa sana, lakini tazama, ni awangapi miongoni mwao wameletwa kuona mwangaza wa ajabu wa Mungu! Na hii ndiyo baraka ambayo tumeteremshiwa, kwamba tumetengenezwa kuwa bvyombo mikononi mwa Mungu kuimarisha kazi hii kubwa.

4 Tazama, amaelfu miongoni mwao wanafurahi, na kuletwa kwenye zizi la Mungu.

5 Tazama, ashamba lilikuwa bivu, na heri ninyi, kwani mlisukuma bpepeto, na mkavuna kwa nguvu, ndiyo, siku yote nzima mlifanya kazi; na tazama idadi ya cmiganda yenu! Na itakusanywa kwenye maghala, ili isiharibiwe.

6 Ndiyo, haitaangushwa na dhoruba ya mvua siku ya mwisho; ndiyo, wala haitatawanyishwa na vimbunga; lakini adhoruba itakapokuja itakusanywa pamoja, kwamba dhoruba isiweze kuipenya; ndiyo, wala haitasukumwa na upepo mkali popote adui atakapotaka kuipeleka.

7 Lakini tazama, wamo mikononi mwa Bwana wa amavuno, na ni wake; na batawainua katika siku ya mwisho.

8 Libarikiwe jina la Mungu wetu; acheni atuimbe kwa sifa yake, ndiyo, wacha btulishukuru jina lake takatifu, kwani yeye hufanya kazi ya haki milele.

9 Kwani kama hatungekuja kutoka kwa nchi ya Zarahemla, hawa ndugu zetu wapendwa, ambao wametupenda sana, wangekuwa bado wanasumbuliwa na achuki juu yetu, ndiyo, na wangekuwa pia wageni kwa Mungu.

10 Na ikawa kwamba baada ya Amoni kusema maneno haya, ndugu yake Haruni alimkemea, akisema: Amoni, ninaogopa kwamba shangwe yako imekusababisha kuelekea kujisifu.

11 Lakini Amoni alimwambia: Mimi asijisifu kwa nguvu yangu, wala kwa hekima yangu; lakini tazama, bshangwe yangu ni tele, ndiyo, moyo wangu umejawa na shangwe, na nitafurahi ndani ya Mungu wangu.

12 Ndiyo, najua kwamba mimi si kitu; kulingana na nguvu zangu mimi ni mlegevu; kwa hivyo sitaweza akujivuna mwenyewe, lakini nitajivuna katika Mungu wangu, kwani kwa bnguvu zake naweza kufanya vitu vyote; ndiyo, tazama, miujiza mingi mikuu tumetenda kwenye nchi hii, ambayo kwayo tutasifu jina lake milele.

13 Tazama, ni maelfu mangapi ya ndugu zetu ambao amewaachilia kutoka kwa uchungu wa ajehanamu; na wamefanywa bkuimba upendo ukomboao, na haya kwa sababu ya uwezo wa neno lake, ambao uko ndani yetu, kwa hivyo, si tuna sababu kuu ya kufurahi?

14 Ndiyo, tuna sababu ya kumsifu milele, kwani yeye ni Mungu Aliye Juu Sana, na amewafungua ndugu zetu kutoka kwenye aminyororo ya jehanamu.

15 Ndiyo, walizungukwa na giza lisilo na mwisho na uharibifu; lakini tazama, amewaleta kwenye amwangaza usio na mwisho, ndiyo, kwenye wokovu usio na mwisho; na wamezungukwa na ukarimu usiolinganishwa wa mapenzi yake; ndiyo, na tumekuwa vyombo mikononi mwake vya kufanya kazi hii kuu na ya kushangaza.

16 Kwa hivyo, wacha atusifu, ndiyo, btutamsifu Bwana; ndiyo, tutafurahi, kwani shangwe yetu imejaa; ndiyo, tutamsifu Mungu wetu milele. Tazama, ni nani anayeweza kufurahia sana kwa Bwana? Ndiyo, ni nani anaweza kuongea sana juu ya uwezo wake mkuu, na churuma yake, na uvumilivu wake kwa watoto wa watu? Tazama nasema kwenu, siwezi kusema sehemu ndogo ya yale ambayo ninahisi.

17 Ni nani ambaye angefikiria kwamba Mungu wetu angekuwa na huruma nyingi hivyo ili kutuokoa kutoka kwenye hali yetu chafu, ya kutisha, na yenye dhambi?

18 Tazama, tulienda mbele, kwa hasira na vitisho vingi akuangamiza kanisa lake.

19 Ee basi, kwa nini hakutuweka sisi kwenye maangamizo ya kutisha, ndiyo, kwa nini hakuachilia panga lake la haki kutuangukia, na kutulaani sisi kwa kutukatisha tamaa milele?

20 Ee, nafsi yangu, kama ilivyo, iko karibu kukimbia kutoka kwa wazo hilo. Tazama, hakutumia haki yake kwetu, lakini kwa hekima yake kuu ametuleta sisi nje ya ashimo lile lisilo na mwisho la kifo na taabu, hata kwenye wokovu wa nafsi zetu.

21 Na sasa tazama, ndugu zangu, ni mtu gani wa akawaida ambaye anajua vitu hivi? Nawaambia ninyi, hakuna yeyote ambaye banaelewa hivi vitu, isipokuwa wenye kutubu.

22 Ndiyo, yule ambaye aanatubu na kutimiza bimani, na kutenda kazi nzuri, na kuomba wakati wote bila kikomo—kwa hawa wamepewa kujua csiri za Mungu; ndiyo, kwa hawa wamepawa kufunua vitu ambavyo havijawahi kufunuliwa; ndiyo, na watapaswe kupewa maelfu ya nafsi kwenye toba, kama vile tulivyopewa sisi kuwaleta ndugu zetu hawa kwenye toba.

23 Sasa mnakumbuka, ndugu zangu, kwamba tuliwaambia ndugu zetu kwenye nchi ya Zarahemla, tunaenda kwenye nchi ya Nefi, tuhubirie ndugu zetu, Walamani, na wakatucheka kwa madharau?

24 Kwani walituambia: Mnafikiri kwamba mnaweza kuwafahamisha Walamani ukweli? Mnafikiri mnaweza kuwasadikisha Walamani makosa ya adesturi za babu zao, wakiwa watu wenye bshingo ngumu vile walivyo; ambao mioyo yao hufurahia kwa umwagaji wa damu; ambao siku zao zimetumika kwa maovu mabaya sana; ambao njia zao zimekuwa njia za mhalifu tangu mwanzo? Sasa ndugu zangu, mnakumbuka kwamba hii ndiyo ilikuwa lugha yao.

25 Na tena walisema: Acha tuchukue silaha dhidi yao, ili tuwaangamize na maovu yao kutoka nchini, kwa maana wanaweza kutupita na kutuua.

26 Lakini tazama, ndugu zangu wapendwa, tulikuja nyikani sio na nia ya kuwaangamiza ndugu zetu, lakini nia ilikuwa labda tungeponya wachache wao.

27 Sasa wakati mioyo yetu ilihuzunishwa, na tukawa karibu kurudi, tazama, Bwana aalitufariji, na kusema: Nendeni miongoni mwa ndugu zenu, Walamani, na mvumilie bmateso yenu kwa csubira, na nitawapatia mafanikio.

28 Na sasa tazama, tumekuja, na tumekuwa miongoni mwao; na tumekuwa wavumilivu kwenye maumivu yetu, na tumevumilia aina yote ya masumbuko; ndiyo, tumesafiri kutoka nyumba hadi nyingine, tukitegemea huruma ya walimwengu—sio huruma ya walimwengu pekee lakini juu ya huruma za Mungu.

29 Na tumeingia kwenye nyumba zao na kuwafundisha, na tumewafundisha kwenye njia za miji yao; ndiyo, na tumewafundisha kwenye vilima vyao; na pia tumeingia kwenye hekalu zao na masinagogi yao na kuwafundisha; na tumetupwa nje, na kufanyiwa mzaha, na kutemewa mate, na kupigwa kwenye mashavu ya uso; na tumepigwa na mawe, na kuchukuliwa na kufungwa kwa kamba za nguvu, na kutupwa gerezani; na kupitia kwa nguvu na hekima wa Mungu tumekombolewa tena.

30 Na tulivumilia aina yote ya mateso, na tulifanya haya yote, kwamba labda tungepata njia ya kuponya watu; na tulifikiri kwamba ashangwe yetu ingejaa ikiwa labda tungekuwa na njia ya kuwaokoa wengine.

31 Sasa tazama, tungeweza kuona mbele na kuona matunda ya kazi zetu, na ni wachache? Ninawaambia: Hapana, ni awengi; ndiyo, na tunaweza kushuhudia uaminifu wao, kwa sababu ya mapenzi yao juu ya ndugu zao na pia sisi.

32 Kwani tazama, awangejitolea dhabihu maisha yao kuliko kuwaua adui wao; na bwamezika silaha zao za vita udongoni, kwa sababu ya mapenzi yao juu ya ndugu zao.

33 Na sasa tazama, nawaambia ninyi, kumewahi kuwa na mapenzi makuu hivi nchini kote? Tazama, nawaambia, La, hakujakuwepo, hata miongoni mwa Wanefi.

34 Kwani tazama, wangechukua silaha dhidi ya ndugu zao; hawangevumilia wenyewe wauawe. Lakini tazameni ni wangapi baina ya hawa ambao wametoa maisha yao; na tunajua kwamba wameenda kwa Mungu wao, kwa sababu ya mapenzi yao na kwa sababu ya chuki yao kwa dhambi.

35 Sasa si tunayo sababu ya kufurahi? Ndiyo, nasema kwenu, hakujakuwa na watu ambao walikuwa na sababu kubwa hivyo ya kufurahi kama sisi, tangu mwanzo wa dunia; ndiyo, na shangwe yangu imenichukua mbali, hata kwa majivuno kwa Mungu wangu; kwani ana auwezo wote, hekima yote, na akili yote; banaelewa vitu vyote, na ni Kiumbe cha churuma, hata kwenye wokovu, kwa wale ambao watatubu na kuamini kwa jina lake.

36 Sasa kama hii ni kujivuna, na hata iwe hivyo nitajivuna; kwani haya ni maisha yangu na mwangaza wangu, shangwe yangu na wokovu wangu, na ukombozi wangu kutoka kwa taabu usio na mwisho. Ndiyo, libarikiwe jina la Mungu wangu, ambaye amewajali watu hawa, ambao ni atawi la mti wa Israeli, na limepotea kutoka kwenye shina lake kwenye nchi ngeni; ndiyo, ninasema, heri jina la Mungu wangu, ambaye amekuwa mwangalifu kwetu, bwazururaji kwenye nchi geni.

37 Sasa ndugu zangu, tunaona kwamba Mungu ni mwangalifu kwa kila awatu, nchi yoyote ambayo wangekuwa ndani; ndiyo, huhesabu watu wake, na ana huruma za kutosha kwa ulimwengu wote. Sasa hii ndiyo shangwe yangu, na shukrani yangu nyingi; ndiyo, na nitatoa shukrani kwa Mungu wangu milele. Amina.