Maandiko
1 Nefi 12
iliyopita inayofuata

Mlango wa 12

Nefi anaona katika ono nchi ya ahadi; haki, uovu, na uangamizo wa wenyeji wake; kuja kwa Mwanakondoo wa Mungu miongoni mwao; jinsi wale Wanafunzi Kumi na Wawili pamoja na wale Mitume Kumi na Wawili watahukumu Israeli; na hali ya machukizo na uchafu ya wale ambao wanafifia katika kutoamini. Karibia mwaka 600–592 K.K.

1 Na ikawa kwamba malaika akaniambia: Angalia, na uone uzao wako, na pia uzao wa kaka zako. Na nikaangalia na kuona anchi ya ahadi; na nikaona vikundi vya watu, ndiyo, hata hesabu yao ilikuwa nyingi kama mchanga wa bahari.

2 Na ikawa kwamba niliona vikundi vimekusanyika pamoja kupigana, moja dhidi ya mwingine; na nikaona avita, na uvumi wa vita, na mauaji makuu kwa upanga miongoni mwa watu wangu.

3 Na ikawa kwamba niliona vizazi vingi vikipita, baada ya vita vya namna hii na mabishano katika nchi; na nikaona miji mingi, ndiyo, hata sikuihesabu.

4 Na ikawa kwamba niliona aukungu bmweusi usoni mwa nchi ya ahadi; na nikaona umeme, na nikasikia radi, na mitetemeko ya ardhi, na aina zote za misukosuko na makelele; na nikaona ardhi, na miamba, kwamba ilipasuka; na nikaona milima ikivunjika vipande vipande; na nikaona tambarare za ardhi, kwamba zilipasuka; na nikaona miji mingi cimezama; na nikaona mingi iliyochomwa kwa moto; na nikaona mingi iliyoanguka chini, kwa sababu ya ile mitetemeko.

5 Na ikawa baada ya kuona vitu hivi, nikaona ule aukungu wa giza, ukitoweka kutoka usoni mwa ulimwengu; na tazama, nikaona makundi ya wale ambao hawakuanguka kwa sababu ya hukumu kuu ya kuhofisha kwa Bwana.

6 Na nikaona mbingu zikifunguka, na aMwanakondoo wa Mungu akiteremka kutoka mbinguni; na akashuka chini na akajionyesha kwao.

7 Na pia niliona na ninashuhudia kwamba Roho Mtakatifu aliwashukia wengine akumi na wawili; na walichaguliwa na kuteuliwa, na Mungu.

8 Na malaika akanizungumzia, na kusema: Tazama wale wanafunzi kumi na wawili wa Mwanakondoo, ambao wameteuliwa kuhudumia uzao wako.

9 Na akaniambia: Je, unawakumbuka wale amitume kumi na wawili wa Mwanakondoo? Tazama ni wao bwatakaohukumu yale makabila kumi na mawili ya Israeli; kwa hivyo, wale wahudumu kumi na wawili wa uzao wako watahukumiwa na wao; kwani ninyi ni wa nyumba ya Israeli.

10 Na hawa awahudumu kumi na wawili uwaonao watahukumu uzao wako. Na, tazama, wao ni watakatifu milele; kwa sababu ya imani yao katika Mwanakondoo wa Mungu bmavazi yao yanafanywa kuwa meupe kwa damu yake.

11 Na malaika akaniambia: Angalia! Na nikaangalia, na kuona vizazi avitatu vikiishi kwa haki; na mavazi yao yalikuwa meupe kama ya Mwanakondoo wa Mungu. Na malaika akaniambia: Hawa wamefanywa kuwa weupe kwa damu ya Mwanakondoo, kwa sababu ya imani yao kwake.

12 Na mimi, Nefi, pia nikaona wengi katika kizazi cha anne wakiishi katika haki.

13 Na ikawa kwamba niliona vikundi vya dunia vimekusanyika pamoja.

14 Na malaika akaniambia: Tazama uzao wako, na pia uzao wa kaka zako.

15 Na ikawa kwamba niliangalia na kuona watu wa uzao wangu wamekusanyika pamoja katika vikundi akupigana na uzao wa kaka zangu; na walikusanyika pamoja wapigane vita.

16 Na malaika akanizungumzia, akisema: Tazama chemchemi ya maji amachafu ambayo baba yako aliiona; ndiyo, hata bmto ambao aliuzungumzia; na kilindi chake ni kilindi cha cjehanamu.

17 Na aukungu wa giza ni majaribio ya ibilisi, byanayopofusha macho, na ambayo yanashupaza mioyo ya watoto wa watu, na kuwaelekeza kwenye cnjia pana, ili waangamie na kupotea.

18 Na ajengo kubwa na pana, ambalo baba yako aliliona, ni bmawazo yasiyofaa na ckiburi cha watoto wa watu. Na dshimo kubwa la kuhofisha linawagawanya; ndiyo, hata neno la ehaki la Mungu wa Milele, na Masiya ambaye ni Mwanakondoo wa Mungu, ambaye anashuhudiwa na Roho Mtakatifu, tangu mwanzo wa ulimwengu hadi sasa, na tangu sasa hadi milele.

19 Na wakati malaika alipokuwa akisema maneno haya, nikatazama na kuona kwamba uzao wa kaka zangu walichokozana na uzao wangu, kulingana na maneno ya malaika; na kwa sababu ya kiburi cha uzao wangu, na amajaribio ya ibilisi, nikaona kwamba uzao wa kaka zangu bwaliwashinda watu wa uzao wangu.

20 Na ikawa kwamba nilitazama, na kuona kwamba watu wa uzao wa kaka zangu waliwashinda uzao wangu; na wakendelea mbele katika vikundi kwenye uso wa nchi.

21 Na nikawaona wamekusanyika pamoja katika vikundi; na nikaona avita na uvumi wa vita miongoni mwao; na nikaona vizazi vingi vikiishi kwenye vita na uvumi wa vita.

22 Na malaika akaniambia: Tazama hawa awatafifia katika kutoamini.

23 Na ikawa kwamba niliona, baada ya wao kufifia katika kutoamini wakawa watu wa agiza, wenye makuruhu, wenye buchafu, waliojaa cuzembe na namna zote za machukizo.