Misaada ya Kujifunza
9. Hekalu la Kirtland


9. Hekalu la Kirtland

Picha
picha 9

Hekalu la Kirtland liko katika Kirtland, Ohio.

Matukio muhimu: Hekalu la Kirtland ndilo la kwanza kujengwa katika kipindi hiki (M&M 88:119; 95). Katika hekalu hili, Joseph Smith aliona ono la ufalme wa selestia (M&M 137). Liliwekwa wakfu mnamo 27 Machi 1836 (M&M 109). Mnamo 3 Aprili 1836, Mwokozi alitokea na kulikubali hekalu kama mahali ambamo angelifunua neno Lake kwa watu Wake (M&M 110:1–10). Baada ya kuonekana huko, Joseph Smith na Oliver Cowdery walitembelewa na Musa, Elia, na Eliya, ambao wote waliwapa funguo fulani za ukuhani na taarifa muhimu (M&M 110:11–16). Hekalu hili liliwahudumia Watakatifu kwa kiasi cha miaka miwili kabla hawajaikimbia Kirtland kwa sababu ya mateso.