Misaada ya Kujifunza
14. Duka la Matofali Mekundu la Joseph Smith Mdogo


14. Duka la Matofali Mekundu la Joseph Smith Mdogo

Picha
picha 14

Hili duka na ofisi iliyojengwa upya ya Joseph Smith Mdogo iko katika Nauvoo, Illinois. Ilikuwa ni moja ya majengo muhimu zaidi katika Kanisa wakati wa kipindi cha Nauvoo. Siyo tu lilitumika kama duka la rejareja, pia lilikuwa kituo cha kijamii, kiuchumi, kisiasa, na shughuli za kidini. Joseph Smith alikuwa na ofisi katika ghorofa ya pili.

Matukio muhimu: Kabla hekalu halijakamilika, chumba cha orofani cha duka kilitumika kama chumba cha ibada, mahali ambapo endaomenti kamili za kwanza zilitolewa. Mnamo, 17 Machi 1842, Nabii Joseph aliwaandaa wanawake wa Kanisa katika Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama wa Kanisa.