Misaada ya Kujifunza
11. Kiwanja cha Hekalu cha Far West


11. Kiwanja cha Hekalu cha Far West

Picha
picha 11

Makazi ya Far West, Missouri, yalikuja kuwa makazi kwa Watakatifu 3,000 hadi 5000 waliotafuta kimbilio kutokana na mateso katika Wilaya za Jackson na Clay. Mnamo mwaka 1838 Bwana aliwaamuru Watakatifu kujenga hekalu hapa (ona M&M 115:7–8) Mateso waliyofanyiwa na kundi la waovu yaliwazuia wao kufanya hivyo. Mnamo 31 Oktoba ya mwaka huo, Joseph Smith Nabii na viongozi wengine wa Kanisa waliwekwa rumande na, baada ya kusikilizwa mashtaka katika Richmond, wakafungwa gerezani la Liberty. Wakati wa majira ya baridi ya mwaka 1838–1839, Watakatifu wa Siku za Mwisho walifukuzwa kutoka Far West na maeneo mengine katika Missouri na wakahamia makao mapya katika Ilinois.

Matukio muhimu: Eneo la hekalu liliwekwa wakfu na mawe ya msingi yakawekwa. Mafunuo saba yaliyochapishwa katika Mafundisho na Maagano yalipokelewa (sehemu ya 113–15; 117–120). Joseph F. Smith, Rais wa sita wa Kanisa, alizaliwa 13 Novemba 1838 katika Far West. Kwa muda mfupi Far West ilitumika kama makao makuu ya Kanisa chini ya Joseph Smith Nabii.