Misaada ya Kujifunza
5. Mto Susquehanna


5. Mto Susquehanna

Picha
picha 5

Picha hii inaonyesha Mto Susquehanna katika Eneo la Mji wa Harmony, Pennsylvania.

Matukio Muhimu: Joseph Smith Mdogo, alikuja mara ya kwanza Harmony mwaka wa 1825 kutafuta ajira. Yeye na baba yake walikaa karibu na hapa katika nyumba ya Isaac Hale, mahali ambapo Joseph Smith alikutana kwa mara ya kwanza na Emma Hale, ambaye baadaye alikuja kuwa mke wake (JS—H 1:56–57). Joseph na Emma walioana 18 Januari 1827. Nabii alipokea mabamba ya dhahabu 22 Septemba 1827 huko Manchester, New York, na muda mfupi baada ya hapo alihama pamoja na Emma kwenda Harmony, mahali alikoanza kutafsiri mabamba hayo. Wakati wa tafsiri ya Kitabu cha Mormoni, Joseph Smith na Oliver Cowdery walitaka kujua zaidi juu ya ubatizo na wakatembea kuelekea msituni jirani na hapa ili kusali kwa Bwana kuhusu jambo hilo. Katika jibu la sala hii, Yohana Mbatizaji akawatokea mnamo 15 Mei 1829 (JS—H 1:66–74; M&M 13). Akawatunukia Joseph na Oliver Ukuhani wa Haruni. Kisha ndipo wakaingia ndani ya mto huu na wakabatizana kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Kisha Joseph na Oliver wakaelekezwa na Yohana Mbatizaji kutawazana wao kwa wao kwenye Ukuhani wa Haruni. Muda mfupi baadaye, Petro, Yakobo na Yohana walijitokeza kati ya Harmony na Colesville na kutunuku juu ya Joseph na Oliver Ukuhani wa Melkizedeki (M&M 27:12–13; 128:20).