Misaada ya Kujifunza
7. Duka la Newel K. Whitney na Wenzake


7. Duka la Newel K. Whitney na Wenzake

Picha
picha 7

Duka hili la Newl K. Whitney lilikuwa na nafasi muhimu katika historia ya Kanisa katika Kirtland. Joseph na Emma Smith waliishi hapa kwa muda mfupi. Mafunuo muhimu kadhaa yalikuwa yamepokelewa hapa. Shule ya Manabii ilifanyika katika duka hili kuanzia 24 Januari 1833 hadi wakati fulani katika Aprili 1833.

Matukio muhimu: Nabii Joseph alipokea ufunuo juu ya Neno la Hekima (M&M 89). Alifanya sehemu kubwa ya kazi ya tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia (TJS) hapa.