Misaada ya Kujifunza
5. Missouri, Illinois, na Iowa Eneo la Marekani


5. Missouri, Illinois, na Iowa Eneo la Marekani

Picha
ramani ya historia ya Kanisa 5

Kask.

Winter Quarters

Council Bluffs (Kanesville)

Mlima Pisgah

Iowa

Mto Platte

Nauvoo

Garden Grove

Ramus

Montrose

Himaya Wahindi Wakendu

Mto Missouri

Mto Grand

Carthage

Mto Chariton

Springfield

Quincy

Adamu-ondi-Amani

Mto Mississippi

Illinois

Gallatin

Shoal Kijito

Hawn’s Mill

Mto Fishing

Far West

DeWitt

Missouri

Liberty

Richmond

McIlwaine’s Bend

Fort Leavenworth

Independence

Mto Missouri

St. Louis

Wilaya ya Jackson

Kilomita

0 50 100 150 200

A B C D E F G H

1 2 3 4

1

2

3

4

5

6

7

8

9

  1. Independence Panatambulika kama kitovu cha Sayuni (ona M&M 57:3). Kiwanja cha hekalu kiliwekwa wakfu 3 Agosti 1831. Watakatifu walifukuzwa kutoka Wilaya ya Jackson katika mwaka 1833.

  2. Mto Fishing Joseph Smith na Kambi ya Sayuni walisafiri kutoka Kirtland, Ohio, hadi Missouri katika mwaka 1834 ili kuwarejesha Watakatifu wa Wilaya ya Jackson kwenye ardhi yao. M&M 105 ilifunuliwa juu ya kingo za mto huu.

  3. Far West Hapa palikuwa makazi makubwa zaidi ya Wamormoni katika Missouri. Kiwanja kwa ajili ya hekalu kiliwekwa wakfu katika eneo hili (ona M&M 115). Hapa mnamo 8 Julai 1838, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ilipokea wito kutoka kwa Bwana wa kutumikia misheni katika Visiwa vya Uingereza (ona M&M 118).

  4. Adamu-ondi-Amani Bwana alilitambulisha eneo hili katika Missouri ya juu kama mahali ambapo kusanyiko kuu la baadaye litafanyika wakati Yesu Kristo atakapokuja kukutana na Adamu na uzao wake wenye haki (ona M&M 78:15; 107:53–57; 116).

  5. Gereza la Liberty Joseph Smith na wengine walifungwa gerezani hapa kwa mashtaka yasiyo ya haki kuanzia Desemba 1838 hadi Aprili 1839. Katikati ya nyakati za matatizo kwa Kanisa, Joseph alimwitia Bwana kwa mwongozo naye alipokea M&M 121–123.

  6. Nauvoo Iko katika Mto Mississippi, eneo hili lilikuwa mahali pa kukusanyika kwa Watakatifu kuanzia 1839 mpaka 1846. Hapa hekalu lilijengwa, na ibada kama vile ubatizo kwa ajili ya wafu, endaomenti, na kuunganishwa kwa familia zilianza. Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama wa Kanisa ulianzishwa katika mwaka 1842. Mafunuo yaliyopokelewa yanajumuisha M&M 124–129.

  7. Carthage Hapa Nabii Joseph Smith na kaka yake Hyrum waliuawa kifo cha kishahidi mnamo 27 Juni 1844 (ona M&M 135).

  8. Winter Quarters Makazi ya muda makubwa zaidi kwa Watakatifu (1846–1848) wakiwa njiani kwenda Bonde la Salt Lake. Kambi ya Israeli iliundwa kwa ajili ya safari ya kuelekea magharibi (ona M&M 136).

  9. Council Bluffs (Kanesville) Urais wa Kwanza ulikubalika na Kanisa hapa mnamo 27 Desemba 1847, Brigham Young akiwa Rais.