Maelezo ya Jumla na Ufunguo
Mistari juu ya ramani hapo chini inaonyesha mahali panapoonekana vizuri kwa kila ramani iliyopewa namba ambayo inafuata. Ramani hizi zimeundwa kwa maeneo mapana na pia maeneo finyu kijiografia.
Ufuatao ni ufunguo wa kuelewa aina mbalimbali za alama na aina ya chapa zinazotumika kwenye ramani. Kwa nyongeza, ramani zinazojitegemea zinaweza kuwa na funguo na maelezo ya alama za ziada zinazohusiana na ramani hiyo.
- ■
-
Kisanduku cha rangi ya chungwa kinawakilisha jengo, biashara, au sura nyingine ya mji.
- ●
-
Nukta nyekundu huwakilisha jiji au mji.
- Bahari ya Atlantiki
-
Aina hii ya chapa imetumika kutaja maeneo ya kijiografia kama vile maziwa, mito, milima, nyika, na mabonde.
- Palmyra
-
Aina hii ya chapa imetumika kwa ajili ya majiji na miji.
- New York
-
Aina hii ya chapa imetumika kwa ajili ya maeneo madogo ya kisiasa, kama vile mikoa na majimbo na wilaya za Marekani.
- Kanada
-
Aina hili ya chapa imetumika kwa ajili ya maeneao makubwa zaidi kisiasa, kama vile mataifa, nchi, na mabara.