Maandiko Matakatifu
Moroni 6


Mlango wa 6

Watu waliotubu wanabatizwa na kushirikishwa—Washiriki wa Kanisa wanaotubu wanasamehewa—Mikutano inaendeshwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Karibia mwaka 401–421 B.K.

1 Na sasa ninazungumza kuhusu aubatizo. Tazama, wazee, makuhani, na walimu walibatizwa; na hawangebatizwa kama hawangezaa matunda byapasayo toba.

2 Wala hawakumpokea yeyote kwenye ubatizo kama hangekuja na moyo auliopondeka na roho iliyovunjika, na kushuhudia kwa kanisa kwamba wametubu kwa kweli kutoka kwenye dhambi zao.

3 Na hakuna waliopokelewa kwenye ubatizo isipokuwa awajivike juu yao jina la Kristo na kukata kauli kumtumikia hadi mwisho.

4 Na baada ya hao kupokewa kwenye ubatizo, na kupokelewa na akusafishwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, walihesabiwa miongoni mwa watu wa kanisa la Kristo; na bmajina yao yalichukuliwa ili wakumbukwe na kulishwa na neno nzuri la Mungu, kuwaweka kwenye njia nzuri, kuwaweka cwaangalifu siku zote kwenye sala, dwakitegemea tu katika nguvu ya wokovu wa Kristo, ambaye alikuwa emwanzilishi na mtimizaji wa imani yao.

5 Na washiriki wa akanisa walikutana pamoja bmara kwa mara, ckufunga na kuomba, na kuzungumza mmoja na mwingine kuhusu ustawi wa nafsi zao.

6 Na walikutana pamoja mara kwa mara kushiriki kwa mkate na divai, katika kumkumbuka Bwana Yesu.

7 Na walikuwa waangalifu kwamba akusiwe na uovu miongoni mwao; na yeyote aliyepatikana akitenda uovu, na mashahidi bwatatu wa kanisa waliwahukumu mbele ya cwazee, na kama hawakutubu, na dhawakukiri, majina yao eyalitolewa nje, na hawakuhesabiwa miongoni mwa watu wa Kristo.

8 Lakini kila amara walipotubu na kutafuta msamaha, na kusudi halisi, bwalisamehewa.

9 Na mikutano yao ailiendeshwa na kanisa kulingana na njia ambayo Roho aliwaongoza, na kwa uwezo wa bRoho Mtakatifu; kwani vile uwezo wa Roho Mtakatifu ulivyowaongoza kuhubiri, au kuhimiza, au kuomba, hata hivyo ndivyo ilivyofanywa.