Maandiko
Yakobo (KM) 1
iliyopita inayofuata

Kitabu cha Yakobo
Mdogo wa Nefi

Maneno aliyowahubiria ndugu zake. Anamfadhaisha mtu aliyetaka kupindua mafundisho ya Kristo. Maneno machache kuhusu historia ya watu wa Nefi.

Mlango wa 1

Yakobo na Yusufu wanatafuta kuwashawishi wanadamu kumwamini Kristo na kushika amri Zake—Nefi anafariki—Uovu unazidi miongoni mwa Wanefi. Karibia mwaka 544–421 K.K.

1 Kwani tazama, ikawa kwamba miaka hamsini na mitano ilikuwa imepita tangu Lehi atoke Yerusalemu; kwa hivyo, Nefi alinipatia mimi, aYakobo, bamri kuhusu mabamba yale cmadogo, ambako vitu hivi vimechorwa.

2 Na akanipatia mimi, Yakobo, amri kwamba niandike kwenye mabamba haya vitu vichache ambavyo nilivifikiria kuwa vyenye thamani; na kwamba nisiguse, ila kidogo tu, kuhusu historia ya hawa watu wanaoitwa watu wa Nefi.

3 Kwani alisema kwamba historia ya watu wake iandikwe kwenye yale mabamba yake mengine, na kwamba nihifadhi mabamba haya na kupokelezea uzao wangu, kutoka kizazi hadi kizazi.

4 Na kama kulikuwa na mahubiri yaliyo matakatifu, au ufunuo ulio mkuu, au kutoa unabii, kwamba nichore yaliyo muhimu katika mabamba haya, na niyagusie sana kama iwezekanavyo, kwa ajili ya Kristo, na kwa faida ya watu wetu.

5 Kwani kwa sababu ya imani na wasiwasi mwingi, kwa hakika tulidhihirishiwa, kuhusu vile vitu avitakavyowapata watu wetu.

6 Na pia tulikuwa na ufunuo mwingi, na roho ya unabii mwingi; kwa hivyo, tulijua kuhusu aKristo na ufalme wake, utakaokuja.

7 Kwa hivyo tulifanya kazi kwa bidii miongoni mwa watu wetu, kwamba tuwashawishi awaje kwa Kristo, na waonje wema wa Mungu, ili waingie katika bpumziko lake, na ili kwa njia yoyote asiape katika ghadhabu yake kwamba chawataingia ndani, kama walivyomtia dhasira katika siku za majaribio wakati wana wa Israeli walipokuwa enyikani.

8 Kwa hivyo, tunatamani kutoka kwa Mungu kama ingewezekana kwamba tungewashawishi wanadamu wote awasimwasi Mungu, kumtia bhasira, lakini kwamba watu wote wangemwamini Kristo, na kutafakari kuhusu kifo chake, na kubeba cmsalaba wake na kuchukua aibu ya ulimwengu; kwa hivyo, mimi, Yakobo, najichukulia kutimiza amri ya kaka yangu Nefi.

9 Sasa Nefi akaanza kuzeeka, na akajua kwamba anakaribia akufariki; kwa hivyo, bakamtia mtu mafuta awe mfalme na mtawala juu ya watu wake sasa, kulingana na utawala wa cwafalme.

10 Watu walikuwa wamempenda Nefi sana, kwa vile alikuwa mlinzi wao mkuu, na kuupunga aupanga wa Labani kwa ulinzi wao, na alikuwa ametumikia kwa ustawi wao katika maisha yake yote—

11 Kwa hivyo, watu walitaka kulikumbuka jina lake. Na yeyote atakayetawala baada yake watu walimwita, Nefi wa pili, Nefi wa tatu, na kadhalika, kulingana na utawala wa wafalme; na hivyo ndivyo walivyoitwa na watu, haidhuru jina lolote walilokuwa nalo.

12 Na ikawa kwamba Nefi alifariki.

13 Sasa wale watu ambao hawakuwa aWalamani walikuwa bWanefi; walakini, waliitwa Wanefi, Wayakobo, Wayusufu, cWazoramu, Walamani, Walemueli, na Waishmaeli.

14 Lakini mimi, Yakobo, hapa baadaye sitawapambanua kwa majina haya, lakini wale wanaotaka kuangamiza watu wa Nefi anitawaita Walamani, na wale ambao ni marafiki wa Nefi nitawaita bWanefi, au cwatu wa Nefi, kulingana na utawala wa wafalme.

15 Na sasa ikawa kwamba watu wa Nefi, chini ya utawala wa mfalme wa pili, walianza kuwa wagumu mioyoni mwao, na kujihusisha katika matendo maovu, kama vile Daudi wa kale wakitamani awake wengi na makahaba, na pia mwana wake, Sulemani.

16 Ndiyo, na hata pia wakaanza kutafuta dhahabu na fedha nyingi, na wakaanza kuinuliwa katika kiburi.

17 Kwa hivyo mimi, Yakobo, niliwapatia maneno haya nilipowafundisha katika ahekalu, nikiwa nimepokea kwanza bmwito wangu kutoka kwa Bwana.

18 Kwani mimi, Yakobo, na kaka yangu Yusufu tulikuwa atumetengwa tuwe makuhani na walimu kwa watu hawa, kwa mkono wa Nefi.

19 Na tuliadhimisha aofisi yetu kwa Bwana, tukijichukulia bjukumu, na wajibu wa dhambi za watu vichwani mwetu kama hatungewafundisha neno la Mungu kwa bidii yote; kwa hivyo, tulitumikia kwa uwezo wetu ili cdamu yao isiwe katika mavazi yetu; la sivyo, damu yao ingekuwa katika mavazi yetu, na hatungepatikana bila alama katika siku ile ya mwisho.