Maandiko
Yakobo (KM) 3
iliyopita inayofuata

Mlango wa 3

Walio safi moyoni wanapokea neno la kupendeza la Mungu—Utakatifu wa Walamani unazidi ule wa Wanefi—Yakobo anaonya kuhusu uasherati, tamaa, na kila dhambi. Karibia mwaka 544–421 K.K.

1 Lakini tazama, mimi, Yakobo, nitawazungumzia wale walio safi moyoni. Mtegemeeni Mungu kwa mawazo yenu yote, na mmuombe, kwa imani kuu, na atawafariji katika mateso yenu, na atatetea kesi yenu, na kuwateremshia hukumu wale wanaotaka kuwaangamiza.

2 Ee ninyi nyote mlio safi moyoni, inueni vichwa vyenu na kupokea neno la kupendeza la Mungu, na kusherekea upendo wake; kwani mnaweza, kama mawazo yenu yatakuwa aimara, daima.

3 Lakini, ole, ole, kwa ninyi msio safi moyoni, wale ambao ni awachafu mbele ya Mungu leo; kwani msipotubu nchi italaaniwa kwa sababu yenu; na Walamani, ambao sio wachafu kama ninyi, walakini bwamelaaniwa kwa laana kali, watawadhulumu hadi wawaangamize.

4 Na wakati unafika haraka, kwamba msipotubu watamiliki nchi yenu ya urithi, na Bwana Mungu aatawaondoa wenye haki miongoni mwenu.

5 Tazameni, Walamani ndugu zenu, ambao mnawachukia kwa sababu ya uchafu wao na laana ambayo imeshika ngozi zao, ni watakatifu zaidi yenu; kwani ahawajasahau amri ya Bwana, ambayo ilipewa kwa baba yetu—kwamba waoe mke mmoja pekee, na wasiwe na makahaba, na wasitende uasherati miongoni mwao.

6 Na sasa, wanatii amri hii kwa bidii; kwa hivyo, kwa sababu ya huu utiifu, katika kuweka amri hii, Bwana Mungu hatawaangamiza, lakini aatawarehemu; na siku moja watakuwa watu wenye baraka.

7 Tazama, mabwana zao awanawapenda wake zao, na wake zao wanawapenda mabwana zao; na mabwana zao na wake zao wanawapenda watoto wao; na kutoamini kwao na chuki yao kwenu ni kwa sababu ya uovu wa baba zao; kwa hivyo, je, ninyi ni wema zaidi yao, machoni pa Muumba wenu mkuu?

8 Enyi ndugu zangu, nawahofia kwamba msipotubu dhambi zenu ngozi zao zitakuwa nyeupe zaidi yenu, mtakapoletwa pamoja na wao mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.

9 Kwa hivyo, nawapa amri, ambayo ni neno la Mungu, kwamba msiwachukie tena kwa sababu ya weusi wa ngozi zao; wala hamtawachukia kwa sababu ya uchafu wao; lakini mtakumbuka uchafu wenu wenyewe, na kukumbuka kwamba uchafu wao ulitokana na baba zao.

10 Kwa hivyo, mtakumbuka awatoto wenu, jinsi mlivyodhulumu mioyo yao kwa sababu ya mfano mliowapatia; na pia, kumbukeni kwamba mnaweza, kwa sababu ya uchafu wenu, kuwatia watoto wenu katika maangamizo, na dhambi zao zitakuwa vichwani vyenu katika siku ya mwisho.

11 Ee ndugu zangu, sikilizeni maneno yangu; amsheni fahamu za nafsi zenu; jitingisheni ili amuamke kutoka katika usingizi wa kifo; na mjifungue kutoka katika uchungu wa bjehanamu ili msiwe cmalaika wa ibilisi, na kutupwa katika ziwa la moto na kiberiti ambalo ni dmauti ya pili.

12 Na sasa mimi, Yakobo, niliwazungumzia watu wa Nefi vitu vingi zaidi nikiwaonya wasitende auasherati na btamaa, na kila aina ya dhambi, na kuwaelezea matokeo yao.

13 Na haiwezekani kuandika hata asilimia moja ya yale yaliotendwa na watu hawa, ambao waliongezeka kuwa wengi, katika amabamba haya; lakini matendo yao mengi yameandikwa katika yale mabamba makubwa, na vita vyao, na mabishano yao, na utawala wa wafalme wao.

14 Mabamba haya yanaitwa mabamba ya Yakobo, na yalitengenezwa kwa mkono wa Nefi. Na ninakoma kuzungumza maneno haya.