Maandiko Matakatifu
1 Nefi 17


Mlango wa 17

Nefi anaamriwa kujenga merikebu—Kaka zake wanampinga—Anawasihi kwa kuwaelezea vile Mungu alivyoitendea Israeli katika historia—Nefi anajazwa na nguvu za Mungu—Kaka zake wanakatazwa wasimguse, au sivyo watanyauka kama nyasi iliyokauka. Karibia mwaka 592–591 K.K.

1 Na ikawa kwamba tulianza safari yetu tena nyikani; na tulisafiri tukielekea mashariki tangu tangu wakati ule na kuendelea. Na tulisafiri na kupitia mateso mengi huko nyikani; na wanawake zetu walizaa watoto nyikani.

2 Na baraka kuu za Bwana zilikuwa nasi, kwamba wakati tulipoishi kwa nyama ambichi huko nyikani, wanawake wetu walitoa maziwa mengi ya kutosha ya kunyonyesha watoto wao, na walikuwa na nguvu, ndiyo, hata kama wanaume; na wakaanza kusafiri bila kunungʼunika.

3 Na hivyo tunaona kwamba lazima amri za Mungu zitimizwe. Na kama watoto wa watu awatatii amri za Mungu atawalisha, na kuwatia nguvu, na kuwapatia uwezo ili wakamilishe kitu ambacho amewaamuru; kwa hivyo, balitupatia uwezo tulipopitia nyikani.

4 Na tulipitia nyikani kwa muda wa miaka mingi, ndiyo, hata miaka minane nyikani.

5 Na tulifika nchi ambayo tuliita Neema, kwa sababu ya matunda yake mengi na asali ya mwitu; na vitu hivi vyote vilitayarishwa na Bwana ili tusiangamie. Na tukaona bahari, ambayo tuliita Ireantumu, ambayo, maana yake, ni maji mengi.

6 Na ikawa kwamba tulipiga hema zetu pwani, ingawaje tulipata amateso na masumbuko mengi, ndiyo, hata mengi zaidi kwamba hatuwezi kuandika yote, tulishangilia sana wakati tulipofika pwani; na tukaita pahali pale Neema, kwa sababu ya matunda yake mengi.

7 Na ikawa kwamba baada ya mimi, Nefi, kuwa katika nchi ya Neema kwa muda wa siku nyingi, sauti ya Bwana ikanijia na kuniambia: Ondoka, na uende mlimani. Na ikawa kwamba niliinuka na kwenda mlimani, na nikamlilia Bwana.

8 Na ikawa kwamba Bwana akanizungumzia, na kusema: Wewe utajenga merikebu, kulingana na avile nitakavyokuonyesha, ili niwavushe watu wako maji haya.

9 Na nikasema: Bwana, ni wapi nitakapoenda ili nipate mawe yenye madini ya kuyeyusha, ili nijenge vifaa vya kutengenezea merikebu jinsi vile umenionyesha?

10 Na ikawa kwamba Bwana akanieleza pa kwenda ili nipate mawe yenye madini, ili nijenge vifaa.

11 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, nilitengeneza mivuo ya kupuliza moto, kwa ngozi za wanyama; na baada ya kutengeneza mivuo, ya kupuliza moto, niligongesha mawe mawili pamoja ili nipate moto.

12 Kwani Bwana hakuturuhusu tuwashe moto mwingi, tulipokuwa tukisafiri nyikani; kwani alisema: Nitafanya chakula chenu kiwe kitamu, hata ahamtakipika;

13 Na pia nitakuwa nuru yenu huko nyikani; na anitawatayarishia njia, kama mtatii amri zangu; kwa hivyo, vile mtakavyotii amri zangu mtaongozwa hadi kwenye bnchi ya ahadi; na cmtajua kwamba ni mimi ninayewaongoza.

14 Ndiyo, na Bwana pia akasema kwamba: Baada ya kuwasili katika nchi ya ahadi, amtajua kwamba mimi, Bwana, ndiye bMungu; na kwamba mimi, Bwana, niliwakomboa kutoka maangamizoni; ndiyo, kwamba niliwatoa kutoka nchi ya Yerusalemu.

15 Kwa hivyo, mimi, Nefi, nilijaribu kutii amri za Bwana, na nikawasihi kaka zangu wawe waaminifu na wenye jitihada.

16 Na ikawa kwamba nilitengeneza vifaa kutoka kwa mawe yenye madini ambayo nilikuwa nimeyayeyusha kutoka kwenye mwamba.

17 Na wakati kaka zangu walipoona kwamba niko karibu akujenga merikebu, walianza kunungʼunika dhidi yangu, na kusema: Ndugu yetu ni mjinga, kwani anafikiri kuwa anaweza kujenga merikebu; ndiyo, na anafikiri pia kwamba anaweza kuvuka maji haya makuu.

18 Na hivyo ndivyo kaka zangu walilalamika dhidi yangu, na hawakutaka kufanya kazi, kwani hawakuamini kwamba ningejenga merikebu; wala hawakuamini kuwa nilifundishwa na Bwana.

19 Na sasa ikawa kwamba mimi, Nefi, nilikuwa na huzuni zaidi kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, na sasa walipoona kwamba nilianza kuwa na huzuni walifurahi mioyoni mwao, hata awakanishangilia kwa kusema: Tulijua kwamba huwezi kujenga merikebu, kwani tulijua ulipungukiwa na mawazo; kwa hivyo, wewe huwezi kutimiza kazi kubwa hivyo.

20 Nawe uko kama baba yetu, aliyepotoshwa na amawazo ya ujinga moyoni mwake; ndiyo, ametutoa kutoka nchi ya Yerusalemu, na tumezunguka nyikani kwa hii miaka mingi; na wanawake wetu wamefanya kazi ya kuchosha, wakiwa wajawazito; na wamezaa watoto nyikani na kuteseka kwa vitu vyote, ila kifo tu; na ingekuwa vyema wafe kabla ya kutoka Yerusalemu badala ya kuteseka na haya masumbuko.

21 Tazama, hii miaka mingi tumeteseka nyikani, na pengine huu wakati tungefurahia mali yetu na nchi yetu ya urithi; ndiyo, na pengine tungekuwa na furaha.

22 Na tunajua kwamba wale watu waliokuwa katika nchi ya Yerusalemu walikuwa watu awatakatifu; kwani walitii masharti na hukumu za Bwana, na amri zake zote, kulingana na sheria ya Musa; kwa hivyo, tunajua kwamba ni watu watakatifu; na baba yetu amewahukumu, na ametupotosha kwa sababu tulisikiza maneno yake; ndiyo, na kaka yetu ni kama yeye. Na kwa lugha kama hii, kaka zangu walinungʼunika na kulalamika dhidi yetu.

23 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, nikawazungumzia nikasema: Je, mnaamini kwamba baba zetu, ambao walikuwa wana wa Israeli, wangekombolewa kutoka mikononi mwa Wamisri kama hawakutii maneno ya Bwana?

24 Ndiyo, mnadhania kwamba wangetolewa utumwani, kama Bwana hakumwamuru Musa aawatoe utumwani?

25 Sasa mnajua kwamba wana wa Israeli walikuwa autumwani; na mnajua kwamba walikuwa na bmizigo mizito, ambayo ilikuwa migumu kuvumilia; kwa hivyo, mnajua kwamba lazima iwe ilikuwa kitu kizuri kwao, kutolewa utumwani.

26 Sasa mnajua kwamba aMusa aliamriwa na Bwana kutenda ile kazi kuu; na mnajua kwamba kwa bmaneno yake, maji ya Bahari ya Shamu yaligawanyika huku na kule, na wakapitia nchi kavu.

27 Lakini mnajua Wamisri walizama katika Bahari ya Shamu, ambao walikuwa majeshi la Farao.

28 Na pia mnajua kwamba walilishwa kwa amana kutoka mbinguni huko nyikani.

29 Ndiyo, na pia mnajua kwamba Musa, kwa neno lake kulingana na nguvu za Mungu ambazo alikuwa nazo, aaligonga mwamba, na pakatiririka maji, ili wana wa Israeli watulize kiu yao.

30 Na ijapokuwa waliongozwa, na Bwana Mungu wao, Mkombozi wao, akiwatangulia, akiwaongoza mchana na kuwapatia nuru usiku, na kuwafanyia yote ayaliyompasa mwanadamu kupokea, waliposhupaza mioyo yao na kupofusha mawazo yao, na bwakamtusi Musa pamoja na Mungu anayeishi na wa kweli.

31 Na ikawa kwamba aaliwaangamiza kulingana na neno lake; na bakawaongoza kulingana na neno lake; na aliwatendea vitu vyote kulingana na neno lake; na hakuna lolote lililotendwa ila tu kulingana na neno lake.

32 Na baada ya kuvuka mto Yordani aliwatia nguvu za akuwafukuza wana wa nchi ile, ndiyo, hata kuwatawanya kwa maangamizo.

33 Na sasa, mnadhani kuwa wana wa nchi hii, waliokuwa kwenye nchi ya ahadi, waliofukuzwa na babu zetu, mnadhani kuwa walikuwa watakatifu? Tazama, nawaambia, Hapana.

34 Je, mnadhania kwamba Baba zetu wangekuwa bora zaidi yao, kama wangekuwa watakatifu? Ninawaambia, Hapana.

35 Tazama, Bwana anawapenda awatu wote sawa sawa; yule ambaye ni bmtakatifu canapendelewa na Mungu. Lakini tazama, hawa watu walikataa kila neno la Mungu, na walikuwa wamekomaa kwenye maovu; na utimilifu wa ghadhabu ya Mungu ulikuwa juu yao; na Bwana akalaani nchi dhidi yao, na akaibariki kwa babu zetu; ndiyo, alitamka laana dhidi yao kwa maangamizo yao, na akaibariki kwa baba zetu ili wapate mamlaka juu yake.

36 Tazama, Bwana aameumba bdunia ili watu cwaishi ndani yake; na ameumba wanawe ili wairithi.

37 Na ahuinua taifa takatifu, na kuangamiza mataifa maovu.

38 Na anawaongoza watakatifu kwenye anchi za thamani, na waovu banawaangamiza, na kulaani nchi kwa sababu yao.

39 Anatawala juu mbinguni, kwani ndicho kiti chake cha enzi, na dunia ni akiti chake cha kuegemesha miguu.

40 Na anawapenda wale ambao watamkubali awe Mungu wao. Tazama, aliwapenda baba zetu na aakaagana nao, ndiyo, hata na Ibrahimu, bIsaka, na cYakobo; na akakumbuka maagano aliyoagana nao; kwa hivyo, akawatoa kutoka nchi ya dMisri.

41 Na aliwanyosha kwa fimbo yake huko nyikani; kwani awalishupaza mioyo yao, hata kama ninyi; na Bwana aliwanyosha kwa sababu ya uovu wao. Aliwatumia bnyoka wakali warukao miongoni mwao; na baada ya wao kuumwa akawatayarishia njia ya ckuponywa; na lile waliopaswa kutenda ni kutazama; na kwa sababu ya dwepesi wa njia, au urahisi wake, kulikuwa na wengi walioangamia.

42 Na walishupaza mioyo yao mara kwa mara, na awakamwasi bMusa, na pia Mungu; walakini, mnajua kuwa waliongozwa kwa nguvu zake zisizoshindikana hadi wakafika katika nchi ya ahadi.

43 Na sasa, baada ya vitu hivi vyote, wakati umefika kwamba wamekuwa waovu, ndiyo, kupita kiasi; na nafikiri inawezekana leo wanakaribia kuangamizwa; kwani najua siku itafika ambayo lazima waangamizwe, ila tu wachache, ambao watapelekwa utumwani.

44 Kwa hivyo, Bwana aalimwamuru baba yangu kukimbilia nyikani; na Wayahudi pia wakajaribu kumtoa uhai; ndiyo, bnanyi pia mmejaribu kumtoa uhai wake; kwa hivyo, ninyi ni wauaji mioyoni mwenu na ninyi mnafanana na wao.

45 Ninyi ni awepesi kwa kutenda maovu lakini wanyonge kumkumbuka Bwana Mungu wenu. Mmeona bmalaika, na akawazungumzia; ndiyo, mmesikia sauti yake mara kwa mara; na amewazungumzia kwa sauti ndogo tulivu, lakini mlikuwa mmekufa cganzi, kwamba hamkupata yale maneno yake; kwa hivyo, amewazungumzia kwa sauti kama radi, ambayo ilisababisha dunia kutetemeka kama ambayo inapasuka.

46 Na pia mnajua kwamba kwa anguvu za neno lake kuu anaweza kusababisha dunia imalizike; ndiyo, na mnajua kwamba kwa neno lake anaweza kusababisha palipopotoka pawe pamenyooka, na paliponyooka pavunjike. Je, kwa nini, basi, muwe wagumu mioyoni mwenu?

47 Tazama, nafsi yangu imevunjwa na uchungu kwa sababu yenu, na moyo wangu unaumwa; nina hofu kwamba mtatupwa milele. Tazama, animejazwa na Roho mtakatifu wa Mungu, hata kwamba kiwiliwili changu bhakina nguvu.

48 Na sasa ikawa kwamba nilipozungumza maneno haya walinikasirikia, na walitaka kunitupa katika kilindi cha bahari; na walipokuja kunikamata nikawazungumzia, nikisema: Katika jina la Mwenyezi Mungu, ninawaamuru amsiniguse, kwani nimejazwa na bnguvu za Mungu, hata kwamba kiwiliwili changu chaweza kuungua; na yeyote atakayenigusa catakauka kama nyasi iliyokauka; na atakuwa bure mbele ya nguvu za Mungu, kwani Mungu atamwadhibu.

49 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, niliwaambia wasilalamike tena juu ya baba yao; wala wasikatae kunitumikia, kwani Mungu aliniamuru nijenge merikebu.

50 Na nikawaambia: aKama Mungu aliniamuru kutenda vitu vyote ningevifanya. Kama ataniamuru niyaambie maji haya, yawe ardhi, yangekuwa ardhi; na kama nikisema, ingetendeka.

51 Na sasa, ikiwa Bwana anazo nguvu nyingi hivyo, na amefanya miujiza mingi miongoni mwa watoto wa watu, je, kwa nini hawezi akunishauri, kwamba nijenge merikebu?

52 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, niliwaambia kaka zangu vitu vingi, mpaka wakafadhaishwa wasiweze kubishana na mimi; wala hawakuthubutu kunigusa kwa mikono yao au vidole vyao, kwa muda wa siku nyingi. Sasa hawakuthubutu kufanya hivyo ili wasikauke mbele yangu, kwani aRoho ya Mungu alikuwa na nguvu nyingi; hata wakaguswa.

53 Na ikawa kwamba Bwana aliniambia: Nyosha mkono wako tena kwa kaka zako, na hawatakauka mbele yako, lakini nitawashitua, asema Bwana, na nitafanya hivi, ili wajue kwamba mimi ndimi Bwana Mungu wao.

54 Na ikawa kwamba niliwanyoshea kaka zangu mkono wangu, na hawakukauka mbele yangu; lakini Bwana aliwashitua, kulingana na neno ambalo alikuwa amelizungumza.

55 Na sasa, wakasema: Tunajua kwa hakika kwamba Bwana yuko nawe, kwani tunajua kwamba ni nguvu za Bwana zimetushitua. Na wakainama mbele yangu, na walikuwa karibu akuniabudu, lakini sikuwaruhusu, nikisema: Mimi ni mdogo wenu, ndiyo, hata mdogo wenu mdogo; kwa hivyo, mwabuduni Bwana Mungu wenu, na mheshimu baba yenu na mama yenu, ili bmaisha yenu yawe marefu katika nchi ambayo Bwana Mungu wenu atawapatia.