Misaada ya Kujifunza
TJS, Mathayo 16


TJS, Mathayo 16:25–29. Linganisha na Mathayo 16:24–26

Yesu anaelezea ina maana gani kusema mtu “kujichukulia msalaba wake”: ni kukataa maovu yote na kila tamaa ya dunia na kushika amri Zake.

25 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, Kama mtu yeyote atanifuata, na wacha ajikane mwenyewe, na kuchukua msalaba wake na kunifuata.

26 Na sasa kwa mtu kuchukua msalaba wake, ni kukana mwenyewe maovu yote, na kila tamaa ya kiulimwengu, na kushika amri zangu.

27 Msivunje amri zangu kwa ajili ya kuokoa maisha yenu; kwa yeyote atakayeokoa maisha yake katika ulimwengu huu, atayapoteza katika ulimwengu ujao.

28 Na yeyote yule atakaye poteza maisha yake katika ulimwengu huu, kwa ajili yangu, atayapata katika ulimwengu ujao.

29 Kwa hiyo, achaneni na ulimwengu, na muokoe roho zenu; kwani binadamu ananufaika nini, kama atapata ulimwengu wote, na kupoteza nafsi yake? Au binadamu atatoa nini kubadilishana na nafsi yake?