Misaada ya Kujifunza
TJS, Mathayo 9


TJS, Mathayo 9:18–21. Linganisha na Mathayo 9:16–17

Yesu anakataa ubatizo wa Mafarisayo; kwani hauna thamani kwa sababu wao hawamkubali Yeye. Yeye ana tangaza kwamba Yeye ndiye ambaye aliyewapa sheria ya Musa.

18 Kisha Mafarisayo wakamwambia, Kwa nini hutatupokea sisi na ubatizo wetu, kwani huoni tunashika sheria yote?

19 Lakini Yesu akawaambia, ninyi hamzishiki sheria. Kama mngalishika sheria mngelinipokea mimi, kwani mimi ndiye aliyetoa sheria hiyo.

20 Siwapokei ninyi na ubatizo wenu, kwa sababu hauwanufaishi chochote.

21 Kwani wakati kile ambacho ni kipya kikija, cha zamani tayari kutupwa.