Misaada ya Kujifunza
TJS, Wagalatia


TJS, Wagalatia 3:19–20. Linganisha na Wagalatia 3:19–20

Musa ndiye mpatanishi wa agano la kwanza, au sheria. Yesu Kristo ndiye mpatanishi wa agano jipya.

19 Kwa hiyo basi, sheria iliongezwa kwa sababu ya uvunjaji wa sheria hadi aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi katika torati iliyotolewa kwa Musa, aliyetawazwa kwa mkono wa malaika kuwa mpatanishi wa agano hili la kwanza, (sheria.)

20 Sasa huyu mpatanishi hakuwa mpatanishi wa agano jipya; bali yupo mpatanishi mmoja wa agano jipya, ambaye ni Kristo, kama ilivyoandikwa katika sheria kuhusu ahadi zilizofanywa kwa Ibrahimu na uzao wake. Sasa Kristo ndiye mpatanishi wa uzima; kwa maana hii ndiyo ahadi ambayo Mungu aliifanya kwa Ibrahimu.