Misaada ya Kujifunza
TJS, Mathayo 12


TJS, Mathayo 12:37–38. Linganisha na Mathayo 12:43–44; ona pia TJS, Luka 12:9–12

Yeyote yule anayempinga Roho Mtakatifu hatasamehewa.

37 Kisha wakaja baadhi ya waandishi na wakamwambia, Bwana, imeandikwa kwamba, Kila dhambi itasamehewa; lakini wewe unasema, Yeyote yule anayezungumza kumpinga Roho Mtakatifu hatasamehewa. Na walimwuliza, wakisema, Mambo haya yanakuwaje?

38 Na akawaambia, Wakati pepo mchafu anapomtoka mtu, huenda kupitia sehemu kavu, akitafuta sehemu ya mapumziko na huikosa; lakini wakati mtu anapompinga Roho Mtakatifu, yule anasema, nitarudi kwenye nyumba yangu ambako nimetoka; na anaporudi, anamkutaa mtupu, amesafishwa na kupambwa; kwani roho msafi kamwacha peke yake.