Misaada ya Kujifunza
TJS, Mathayo


TJS, Mathayo 3:4–6. Linganisha na Mathayo 2:4–6

Manabii walitabiri kwamba Bethlehemu patakuwa sehemu atakapozaliwa Masiha.

4 Na alipokwisha kuwakusanya makuhani wakuu wote, na waandishi wa watu pamoja, aliwaomba, akisema, Ni sehemu gani ambayo imeandikwa na manabii, ambapo Kristo atazaliwa? Kwani aliogopa sana, na bado hakuwaamini manabii.

5 Na wakamwambia, Imeandikwa na manabii, kwamba atazaliwa Bethlehemu ya Yudea, na hivyi ndivyo walivyosema,

6 Neno la Bwana lilitujia, likisema, Nawe Bethlehemu, iliyopo katika nchi ya Yudea, ndani yako atazaliwa mwana wa mfalme, ambaye hatakuwa mdogo miongoni mwa wana wa mfalme wa Yudea; kwani kutoka kwako atakuja Masiha, atakaye waokoa watu wangu Israeli.

TJS, Mathayo 3:24–26. Linganisha na Mathayo 2:23

Yesu anakuwa na kumsubiria Bwana kabla ya kuanza kwa huduma Yake.

24 Na ikawa kwamba Yesu alikua pamoja na ndugu zake, na kuwa mwenye nguvu, na akasubiri kwa Bwana kwa ajili ya wakati wa huduma yake kufika.

25 Naye alitumikia chini ya baba yake, naye hakuzungumza kama watu wengine, wala hakuweza kufundishwa; kwani hakuhitaji mtu yeyote amfundishe.

26 Na baada ya miaka mingi, saa ya huduma yake ikasogea karibu.

TJS, Mathayo 3:34–36. Linganisha na Mathayo 3:8–9

Wale waliokataa ujumbe wa Yohana Mbatizaji walimkataa Kristo. Mungu anaweza kuwafanya watu wa maagano wale wasio Waisraeli.

34 Kwa nini hampokei mahubiri ya yeye ambaye Mungu amemtuma? Kama hamyapokei haya katika mioyo yenu, hamnipokei mimi; na kama hamnipokei mimi, hamumpokei yeye ambaye amenituma kutoa taarifa, na kwa ajili ya dhambi zenu hamna kitu kinachoficha.

35 Kwa hiyo, tubuni, na mzae matunda kwa ajili ya toba;

36 Na msifikirie mioyoni mwenu na kusema, Sisi ni watoto wa Ibrahimu, na tuna uwezo tu wa kuleta uzao kwa baba yetu Ibrahimu; kwani nasema kwenu kwamba Mungu anaweza kufanya mawe haya kuwa watoto kwa Ibrahimu.

TJS, Mathayo 3:38–40. Linganisha na Mathayo 3:11–12

Yohana Mbatizaji anashuhudia kwamba Yesu ana uwezo wa kubatiza kwa Roho Mtakatifu na moto.

38 Kwa kweli mimi nawabatiza ninyi kwa maji, baada ya toba yenu; na wakati yeye ninaye mtolea taarifa atakapokuja, mwenye uwezo mkubwa kuliko mimi, ambaye viatu vyake mimi siwezi kufunga gidamu zake, (au sehemu yake siwezi kuijaza,) kama nilivyosema, kwa kweli nawabatiza ninyi kabla hajaja, ili wakati atakapo kuja aweze kuwabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu na moto.

39 Na ni yeye nitakayetoa taarifa zake, ambaye pepeo yake itakuwa mikononi mwake, na atasafisha kikamilifu sakafu yake, na kukusanya ngano yake na kuiweka ghalani; lakini baada ya muda wake kutimia atayachoma makapi na moto usiozimika.

40 Ndivyo alivyokuja Yohana, akihubiri na kubatiza katika mto Yorudani; akitoa taarifa kwamba yule aliyekuwa anakuja baada yake alikuwa na uwezo wa kubatiza kwa Roho Mtakatifu na moto.

TJS, Mathayo 3:43–46. Linganisha na Mathayo 3:15–17

Yesu alibatizwa na Yohana kwa kuzamishwa ana mwona Roho Mtakatifu akishuka kama hua, na anaisikia sauti ya Baba.

43 Na Yesu, akajibu, akamwambia, Kubali mimi kubatizwa na wewe, kwani hivyo ndivyo yatupasa sisi kutimiza haki yote. Basi akamkubali.

44 Naye Yohana akaingia majini na akambatiza.

45 Na Yesu alipobatizwa, alipanda kutoka majini; na Yohana aliona, na lo, mbingu zikamfunukia, naye akamwona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na radi juu ya Yesu.

46 Na lo, akasikia sauti kutoka mbinguni, ikisema, Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye. Msikilizeni yeye.