Mlango wa 32
Malaika wanazungumza kwa uwezo wa Roho Mtakatifu—Wanadamu lazima wasali na kupokea ufahamu kwa wao wenyewe kutoka kwa Roho Mtakatifu. Karibia mwaka 559–545 K.K.
1 Na sasa, tazama, ndugu zangu wapendwa, nadhani kwamba mnawaza machache mioyoni mwenu kuhusu yale mtakayotenda baada ya kuingia kwa njia hiyo. Lakini, tazama, kwa nini mnawaza vitu hivi mioyoni mwenu?
2 Je, hamkumbuki kwamba niliwaambia kwamba baada ya akupokea Roho Mtakatifu mngezungumza kwa blugha ya malaika? Na sasa, vipi mngezungumza kwa lugha ya malaika bila Roho Mtakatifu?
3 aMalaika wanazungumza kwa uwezo wa Roho Mtakatifu; kwa hivyo, wanazungumza maneno ya Kristo. Kwa hivyo, niliwaambia, bshiriki maneno ya Kristo; kwani tazama, maneno ya Kristo yatawaelezea vitu vyote mnavyostahili kutenda.
4 Kwa hivyo, na sasa baada ya kuzungumza maneno haya, kama hamwezi kuyafahamu, ni kwa sababu ahamuombi, wala kubisha; kwa hivyo, hamjaletwa kwenye nuru, lakini lazima mwangamie gizani.
5 Kwani tazama, tena nawaambia kwamba kama mtaingia kwa njia hiyo, na kupokea Roho Mtakatifu, atawaonyesha vitu vyote ambavyo mnastahili kutenda.
6 Tazameni, haya ndiyo mafundisho ya Kristo, na hakutakuwa na mafundisho mengine yatakayotolewa hadi aatakapojidhihirisha kwenu katika mwili. Na atakapojithirihisha kwenu katika mwili, mtachunguza na kufanya vile vitu atakavyowaambia.
7 Na sasa mimi, Nefi, siwezi kuzungumza zaidi; Roho anayokomesha mazungumzo yangu, na ninaachwa kuomboleza kwa sababu ya akutoamini, na uovu, na ujinga, na majivuno ya wanadamu; kwani hawatatafuta ufahamu, wala kuelewa ufahamu wa juu, wanapoelezewa wazi bwazi, hata wazi vile neno linaweza kuwa.
8 Na sasa, ndugu zangu wapendwa, naona kwamba bado mnatafakari mioyoni mwenu; na inanihuzunisha kwamba lazima nizungumze kuhusu kitu hiki. Kwani ikiwa mtasikiliza Roho ambaye anawafundisha wanadamu akusali, mtajua kwamba lazima msali, kwani broho mchafu hawafundishi mwanadamu kusali, lakini humfundisha kwamba lazima asisali.
9 Lakini tazameni, nawaambia kwamba lazima amsali kila wakati, na msife moyo; na kwamba msifanye lolote kwa Bwana bila kumuomba Baba kwa bjina la Kristo, kwamba awatakasie matendo yenu, kwamba matendo yenu yawe ni kwa cajili ya ustawi wa nafsi yako.