Maandiko Matakatifu
1 Nefi 16


Mlango wa 16

Waovu wanachukua ukweli kuwa mgumu—Wana wa Lehi wanaoa mabinti za Ishmaeli—Liahona inawaongoza njiani huko nyikani—Ujumbe kutoka kwa Bwana unaandikwa kwenye Liahona mara kwa mara—Ishmaeli anafariki; jamii yake inanungʼunika kwa sababu ya masumbuko. Karibia mwaka 600–592 K.K.

1 Na sasa ikawa kwamba baada ya mimi, Nefi, kumaliza kuwazungumzia kaka zangu, tazama wakaniambia: Wewe umetuelezea vitu vigumu, kuliko tunavyoweza kuvumilia.

2 Na ikawa kwamba niliwaambia kuwa nilijua kwamba nilikuwa nimezungumza vitu vigumu kinyume cha waovu, kulingana na ukweli; na nilikuwa nimewathibitisha wenye haki, na kushuhudia kwamba watainuliwa katika siku ya mwisho; kwa hivyo, wenye ahatia huchukua bukweli kuwa mgumu, kwani chuwakata hadi sehemu zao za ndani.

3 Na sasa kaka zangu, kama ninyi mngekuwa watakatifu na mngetaka kusikiza ukweli, na kuufuata, ili amtembee imara mbele ya Mungu, basi hamngenungʼunika kwa sababu ya ukweli, mkisema: Unazungumza vitu vigumu dhidi yetu.

4 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, niliwasihi kaka zangu, kwa bidii zote, watii amri za Bwana.

5 Na ikawa kwamba awalijinyenyekeza kwa Bwana; hata kwamba nikawa na shangwe na matumaini mengi, kwamba watatembea katika njia za haki.

6 Sasa, vitu hivi vyote vilizungumziwa na kufanyika vile baba yangu alipoishi kwenye hema katika bonde aliloliita Lemueli.

7 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, nilimchukua abinti mmoja wa Ishmaeli kuwa bmke wangu, na pia kaka zangu wakaoa mabinti za Ishmaeli; na pia cZoramu akamwoa binti mkubwa wa Ishmaeli.

8 Na hivyo baba yangu alitimiza amri zote ambazo alipewa na Bwana. Na pia, mimi, Nefi, nilibarikiwa na Bwana zaidi.

9 Na ikawa kwamba sauti ya Bwana ikazungumza na baba yangu usiku, na kumwamuru kwamba kesho yake aanze kusafiri nyikani.

10 Na ikawa kwamba wakati baba yangu alipoamka asubuhi, na akaenda mlangoni mwa hema, kwa mshangao wake mkuu, akaona hapo chini ampira wa ufundi maalumu; na ulikuwa wa shaba nyeupe ya hali ya juu. Na ndani ya huu mpira kulikuwa na mishale miwili; na moja ilionyesha njia tutakayofuata nyikani.

11 Na ikawa kwamba tulikusanya pamoja vitu ambavyo tungebeba nyikani, na pia mabaki ya maakuli ambayo Bwana alikuwa ametupatia; na tukachukua mbegu za kila aina ili tubebe nyikani.

12 Na ikawa kwamba tulichukua hema zetu na kuelekea nyikani, na tukavuka ngʼambo ya mto Lamani.

13 Na ikawa kwamba tulisafiri kwa muda wa siku nne, tukielekea karibu upande wa kusini-kusini-mashariki, na tukapiga hema zetu tena; na tukaita mahali pale Shazeri.

14 Na ikawa kwamba tulichukua pinde zetu na mishale yetu, na kwenda nyikani kuwindia jamii zetu; na baada ya kuwindia jamii zetu chakula tulirejea tena kwa jamii zetu huko nyikani, mahali palipoitwa Shazeri. Na tulisafiri tena nyikani, tukielekea upande ule ule, tukifuata sehemu ambazo zilikuwa nzuri nyikani, ambazo zilikuwa mipakani mwa aBahari ya Shamu.

15 Na ikawa kwamba tulisafiri kwa muda wa siku nyingi, tukiwinda chakula chetu njiani, kwa pinde zetu na mishale yetu na mawe yetu na kwa kombeo zetu.

16 Na tulifuata amajira ya ule mpira, ambayo ilituelekeza katika sehemu zenye rutuba zaidi nyikani.

17 Na baada ya kusafiri kwa muda wa siku nyingi, tukapiga hema zetu kwa muda mfupi, ili tujipumzishe tena na tutafutie jamii zetu chakula.

18 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, nilipoenda kuwinda, tazama, nikavunja upinde wangu, ambao ulikuwa umetengenezwa kwa achuma nyororo; na baada ya kuvunja upinde wangu, tazama, ndugu zangu walinikasirikia kwa kupotelewa na upinde wangu, kwa sababu hatukupata chakula chochote.

19 Na ikawa kwamba tulirudi kwa jamii zetu bila chakula, na wakiwa wamechoka zaidi, kwa sababu ya kusafiri, waliteseka sana kwa kutaka chakula.

20 Na ikawa kwamba Lamani na Lemueli na wana wa Ishmaeli walianza kunungʼunika zaidi, kwa sababu ya mateso yao na masumbuko huko nyikani; na pia baba yangu alianza kumnungʼunikia Bwana, Mungu wake; ndiyo, na wote walikuwa na huzuni zaidi, hata wakamnungʼunikia Bwana.

21 Sasa ikawa kwamba mimi, Nefi, nikiwa nimeumizwa na kaka zangu kwa sababu ya kupotelewa na upinde wangu, na pinde zao zikiwa zimelegea na zimenyumbuka, ilianza kuwa shida zaidi, ndiyo, hata tukakosa chakula.

22 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, niliwazungumzia kaka zangu, kwa sababu walikuwa wameshupaza mioyo yao tena, hata awakamnungʼunikia Bwana Mungu wao.

23 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, nikatengeneza upinde kutoka kwa mbao, na kutoka kwa kijiti kinyoofu, nikatengeneza mshale; kwa hivyo, nikajiami kwa upinde, na mshale, kombeo na mawe. Na nikamuuliza ababa yangu: Niende kuwinda wapi?

24 Na ikawa kwamba aakamuomba Bwana, kwani walijinyenyekeza kwa sababu ya maneno yangu; kwani niliwaambia vitu vingi kwa nguvu za nafsi yangu.

25 Na ikawa kwamba sauti ya Bwana ikamjia baba yangu; na aakakemewa kwa kweli kwa kumnungʼunikia Bwana, hadi akadhilika kwa huzuni nyingi.

26 Na ikawa kwamba sauti ya Bwana ikamwambia: Angalia kwenye ule mpira, na uone vitu vilivyoandikwa.

27 Na ikawa kwamba wakati baba yangu alipoona vitu vilivyoandikwa kwenye mpira, aliogopa na kutetemeka sana, pia na kaka zangu, na wana wa Ishmaeli na wake zetu.

28 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, niliona kwamba vile vyuma vilivyokuwa kwenye mpira, vilifanya kazi kulingana na aimani na bidii na utiifu, ambao tulivipatia.

29 Na pia paliandikwa juu yao maandishi mengine mapya, ambayo yalikuwa rahisi kwa kusomwa, ambayo yalitupatia aufahamu kuhusu njia za Bwana; na yaliandikwa na kubadilishwa mara kwa mara, kulingana na imani na bidii ambayo tuliipatia. Na hivyo tunaona kwamba kwa njia bndogo Bwana anaweza kuleta vitu vikubwa.

30 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, nilienda juu ya mlima, kulingana na maelezo yaliyokuwa kwenye mpira.

31 Na ikawa kwamba niliwinda wanyama wa mwitu, hata nikapata chakula cha jamii zetu.

32 Na ikawa kwamba nilirudi kwenye hema zetu, nikibeba wanyama ambao niliwinda; na sasa walipoona nilikuwa nimepata chakula, walifurahia sana! Na ikawa kwamba walijinyenyekeza kwa Bwana, na wakamtolea shukrani.

33 Na ikawa kwamba tulianza safari yetu tena, tukisafiri kwa majira karibu kama mwanzoni, na baada ya kusafiri kwa muda wa siku nyingi tulipiga hema zetu tena, ili tukae kwa muda.

34 Na ikawa kwamba aIshmaeli alifariki, na akazikwa mahali palipoitwa Nahomu.

35 Na ikawa kwamba mabinti za Ishmaeli waliomboleza zaidi, kwa sababu ya kifo cha baba yao, na kwa sababu ya amasumbuko yao nyikani; na wakamnungʼunikia baba yangu, kwa sababu aliwatoa nchi ya Yerusalemu, wakisema: Baba yetu amekufa; ndiyo, na tumezunguka sana nyikani, na tumepata masumbuko mengi, njaa, kiu, na uchovu; na baada ya haya mateso yote tutaangamia nyikani kwa njaa.

36 Na hivyo wakalalamika dhidi ya baba yangu, na pia dhidi yangu; na wakataka kurudi tena Yerusalemu.

37 Na Lamani akamwambia Lemueli na pia wana wa Ishmaeli: Tazama, atumuue baba yetu, na pia ndugu yetu Nefi, ambaye amejifanya kuwa bmtawala na mwalimu wetu, sisi ambao ni kaka zake wakubwa.

38 Na sasa, anasema kwamba Bwana amemzungumzia, na pia kwamba amalaika wamemhudumia. Lakini tazama, tunajua kwamba anatudanganya; na anatuambia vitu hivi, na anatenda vitu vingi kwa ujanja wake, ili atufunike macho yetu, akidhani, kwamba, labda atatuelekeza kwenye nyika ya ugeni; na baada ya kufanya hivyo, amepanga kujifanya mfalme na mtawala wetu, ili atutendee kulingana na nia na mapenzi yake. Na jinsi hii ndivyo kaka yangu Lamani alivyochochea hasira mioyoni mwao.

39 Na ikawa kwamba Bwana alikuwa pamoja nasi, ndiyo, hata sauti ya Bwana ikaja na akuwazungumzia maneno mengi, na ikawakemea zaidi; na baada ya kukemewa na sauti ya Bwana wakaacha hasira yao, na wakatubu dhambi zao, hata kwamba Bwana akatubariki tena kwa chakula, kwamba hatukuangamia.