Mkutano Mkuu
Tumaini Tena
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2021


Tumaini Tena

Kumtumaini Mungu na kila mmoja wetu huleta baraka za mbinguni.

Wakati mmoja, nilipokuwa mdogo sana, kwa haraka nilifikiria juu ya kutoroka nyumbani. Kwa uelewa wa kijana mdogo, nilihisi hakuna mtu aliyenipenda.

Mama yangu mwangalifu alisikiliza na kunihakikishia. Nilikuwa salama nyumbani.

Je! umewahi kuhisi kama unatoroka nyumbani? Mara nyingi, kutoroka nyumbani kunamaanisha tumaini limepotea au kuvunjika—tumaini juu yetu sisi wenyewe, kwa kila mmoja wetu, kwa Mungu. Wakati tumaini linapojaribiwa, tunatafuta jinsi ya kutumaini tena.

Ujumbe wangu leo ni kwamba, iwe tunakuja nyumbani au tunakwenda nyumbani, Mungu anakuja kukutana nasi.1 Katika Yeye tunaweza kupata imani na ujasiri, hekima na utambuzi wa kutumaini tena. Vivyo hivyo, Yeye anatusihi tuangaze nuru kwa kila mmoja, tuwe wenye kusamehe zaidi na tusiojihukumu wenyewe na tusiohukumu wengine, ili Kanisa Lake liwe mahali ambapo tunahisi kuwa nyumbani, iwe tunakuja kwa mara ya kwanza au tunarejea.

Tumaini ni tendo la imani. Mungu hutunza imani pamoja nasi. Walakini, tumaini la mwanadamu linaweza kudhoofishwa au kuvunjika wakati:

  • Rafiki, mshirika wa biashara, au mtu tunayemtumaini anapokuwa si mkweli, anapotuumiza au anapotutumia kwa manufaa yake.2

  • Mwenzi wa ndoa si mwaminifu.

  • Pengine bila kutarajia, mtu tunayempenda anakabiliwa na kifo, jeraha, au ugonjwa.

  • Tunapokabiliwa na swali lisilotarajiwa la injili, pengine kitu kuhusu historia ya Kanisa au sera ya Kanisa na mtu anasema kanisa letu kwa njia fulani lilificha au halikusema ukweli.

Hali zingine zinaweza zisiwe maalumu sana lakini zinadhoofisha au kuvunja tumaini.

Pengine hatujioni katika Kanisa, hatuhisi kustahili, tunahisi kuhukumiwa na wengine.

Au, ingawa tumefanya kila kitu kinachotarajiwa, mambo bado hayajafanikiwa. Licha ya uzoefu wetu binafsi na Roho Mtakatifu, bado hatuwezi kuhisi kwamba tunajua Mungu yu hai au injili ni ya kweli.

Wengi leo wanahisi kuna hitaji kubwa la kurejesha tumaini kwenye mahusiano ya kibinadamu na jamii ya kisasa.3

Tunapotafakari juu ya tumaini, tunajua Mungu ni Mungu wa ukweli na “hawezi kusema uwongo.”4 Tunajua ukweli ni ujuzi wa mambo jinsi yalivyo, jinsi yalivyokuwa, na yatakayokuja.5 Tunajua ufunuo na msukumo endelevu wa kiungu hufaa kwenye ukweli usiobadilika katika hali zinazobadilika.

Tunajua maagano yaliyovunjika huvunja mioyo. “Nilifanya vitu vya kijinga,” anasema, “Unaweza kweli kunisamehe?” Mume na mke wanaweza kushikana mikono, wakitarajia kutumaini tena. Katika mazingira tofauti, mfungwa wa gerezani anakumbuka, “Ikiwa ningeshika Neno la Hekima, nisingekuwa hapa hivi leo.”

Tunajua kwamba furaha kwenye njia ya agano ya Bwana na miito ya kutumikia katika Kanisa Lake ni mwaliko wa kuhisi tumaini la Mungu na upendo kwetu na kwa kila mmoja. Waumini wa kanisa, pamoja na watu wazima waseja mara kwa mara hutumikia katika Kanisa na katika jamii zetu.

Kwa msukumo, askofu huwaita wanandoa vijana kuhudumu katika darasa la watoto kwenye kata. Mwanzoni, mume anakaa kwenye kona, akijitenga na kukaa mbali. Hatua kwa hatua, anaanza kutabasamu na watoto. Baadaye, wenzi hao wanatoa shukrani. Hapo awali, wanasema, mke alitaka watoto; mume hakutaka. Sasa, kutumikia kumewabadilisha na kumewaunganisha. Kumeleta pia furaha ya watoto katika ndoa na nyumba yao.

Katika jiji lingine, mama kijana aliye na watoto wadogo na mumewe wanashangazwa na kuzidiwa hisia lakini wanakubali wakati mama akiitwa kutumikia kama rais wa Muungano wa Usaidizi wa kata. Muda mfupi baadaye, tufani za barafu zinakata umeme, zikiacha rafu za maduka zikiwa tupu na nyumba zikiwa baridi kama maboksi ya kutunza barafu. Kwa sababu wana umeme na vyanzo vya joto, familia hii changa kwa ukarimu inafungua nyumba yao kwa familia kadhaa na watu binafsi kujikinga dhidi ya tufani.

tumaini huwa halisi wakati tunafanya mambo magumu kwa imani. Huduma na dhabihu huongeza uwezo na kusafisha mioyo. Kumtumaini Mungu na kila mmoja wetu huleta baraka za mbinguni.

Baada ya kupona saratani, kaka mwaminifu anagongwa na gari. Badala ya kujihurumia, kwa sala anajiuliza, “Ninaweza kujifunza nini kutokana na uzoefu huu?” Katika chumba chake cha wagonjwa mahututi, anahisi msukumo kumgundua muuguzi mwenye wasiwasi juu ya mumewe na watoto. Mgonjwa mwenye maumivu anapata majibu wakati anapomtumaini Mungu na kuwafikia wengine.

Wakati kaka mwenye tatizo la ponografia anasubiri nje ya ofisi ya rais wake wa kigingi, rais wa kigingi anasali kujua jinsi ya kumsaidia. Msukumo wa wazi unakuja:, “Fungua mlango na umruhusu aingie.” Kwa imani na tumaini kwamba Mungu atasaidia, kiongozi wa ukuhani anafungua mlango na kumkumbatia kaka yule. Kila mmoja anahisi upendo ubadilishao na tumaini kwa Mungu na kwa kila mmoja. Akiwa ameimarishwa, kaka anaweza kuanza kutubu na kubadilika.

Wakati hali zetu binafsi ni za kipekee, kanuni za injili na Roho mtakatifu anaweza kutusaidia kujua ikiwa, jinsi gani, na wakati gani wa kuwatumaini wengine tena. Wakati tumaini linapovunjwa au kusalitiwa, kuvunjika moyo na kukata tamaa vinakuwa vitu halisi; na hapo kuna hitaji la kupambanua ili kujua ni wakati gani imani na ujasiri vinastahili ili kutumaini tena katika mahusiano ya kibinadamu.

Walakini, kwa heshima kwa Mungu na ufunuo binafsi, Rais Russell M. Nelson anatuhakikishia, “Haupaswi kujiuliza ni nani unaweza kwa usalama kumtumaini.”6 Tunaweza kumtumaini Mungu kila wakati. Bwana anatujua vizuri na anatupenda kuliko tunavyojijua au kujipenda sisi wenyewe. Upendo Wake usio na kikomo na maarifa Yake kamili ya zamani, ya sasa, na ya baadaye hufanya maagano na ahadi Zake kuwa endelevu na za uhakika.

Tumaini kile ambacho maandiko huita “katika mchakato wa muda.”7 Kwa baraka za Mungu, mchakato wa muda, na imani endelevu na utii, tunaweza kupata azimio na amani.

Bwana anafariji:

“Kulia kunaweza kudumu kwa usiku mmoja, lakini furaha huja asubuhi.”8

“Tua mizigo yako kwa Bwana na tumaini utunzaji wake wa kila wakati.”9

“Dunia haina huzuni ambayo mbingu haiwezi kuponya.”10

Mtumaini Mungu11 na Miujiza Yake. Sisi tunaweza kubadilika na mahusiano yetu yanaweza kubadilika. Kupitia Upatanisho wa Kristo Bwana, tunaweza kuuvua ubinafsi wetu wa asili na kuwa mtoto wa Mungu, mpole, mnyenyekevu,12 aliyejawa imani na uaminifu unaofaa. Tunapotubu, tunapokiri na kuacha dhambi zetu, Bwana anasema hazikumbuki tena.13 Sio kwamba Yeye anasahau; badala yake, kwa njia ya kushangaza, inaonekana anachagua kutozikumbuka, nasi hatuhitaji kuzikumbuka.

Tumaini katika msukumo wa Mungu wa kutambua kwa busara. Tunaweza kuwasamehe wengine kwa wakati na njia sahihi, kama vile Bwana anavyotutaka,14 huku tukiwa “wenye busara kama nyoka, na wapole kama hua.”15

Wakati mwingine wakati mioyo yetu imevunjika na kupondeka, tunakuwa wazi zaidi kwa faraja na mwongozo wa Roho Mtakatifu.16 Hukumu na msamaha vyote vinaanza kwa kutambua kosa. Mara nyingi hukumu inazingatia yaliyopita. Msamaha huangalia siku zijazo. “Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”17

Mtume Paulo anauliza, “Ni nani atakayetutenganisha na upendo wa Kristo?” Anajibu, “Si mauti, wala uhai, … wala urefu, wala kina, … havitaweza kututenganisha na upendo wa Mungu, ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”18 Hata hivyo, kuna mtu ambaye anaweza kututenganisha na Mungu na Yesu Kristo—na mtu huyo ni ni sisi, sisi wenyewe. Kama vile Isaya anavyosema, “Dhambi zako zimeuficha uso wake kwako.”19

Kwa upendo wa kiungu na sheria ya kiungu, tunawajibika kwa chaguzi zetu na matokeo yake. Lakini upendo wa upatanisho wa Mwokozi wetu ni “usio na mwisho na wa milele.”20 Tunapokuwa tayari kurudi nyumbani, hata wakati bado tuko “mbali sana,”21 Mungu yuko tayari kwa huruma nyingi kutupokea, kwa furaha akitoa yaliyo bora Aliyonayo.22

Rais J. Reuben Clark alisema, “Ninaamini kwamba Baba yetu wa Mbinguni anataka kumwokoa kila mmoja wa watoto wake,… kwamba kwa haki na rehema yake atatupatia tuzo kubwa zaidi kwa matendo yetu, atatupatia kila awezacho kutoa, na kinyume chake, ninaamini kwamba yeye atatoa kwetu adhabu ya kiwango cha chini ambayo inawezekana kwake kutoa.”23

Msalabani, hata ombi la rehema la Mwokozi wetu kwa Baba Yake halikuwa na masharti “Baba, wasamehe,” bali “Baba, wasamehe; maana hawajui watendalo.”24 Haki yetu ya kujiamulia na uhuru vina maana kwa sababu tunawajibika mbele za Mungu na kwetu wenyewe kwa kile ambacho tumekuwa, kwa kile ambacho tunajua na kufanya. Kwa shukrani, tunaweza kutumaini haki kamili ya Mungu na rehema kamili kuhukumu kikamilifu nia na matendo yetu.

Tunahitimisha kama tulivyoanza—kwa huruma ya Mungu wakati tunaporejea Kwake nyumbani na kwa kila mmoja.

Je! unakumbuka mfano wa Yesu Kristo kuhusu mtu fulani ambaye alikuwa na wana wawili?25 Mwana mmoja aliondoka nyumbani na kupoteza urithi wake. Alipojirudi, mtoto huyu alitaka kurudi nyumbani. Mwana mwingine, akihisi alikuwa ameshika amri “tazama, miaka hii mingi,”26 hakutaka kumkaribisha kaka yake nyumbani.

Akina kaka na akina dada, tafadhali fikirieni kwamba Yesu anatuomba kufungua mioyo yetu, uelewa wetu, huruma, na unyenyekevu, na kujiona sisi wenyewe katika majukumu haya mawili.

Kama mwana au binti wa kwanza, tunaweza kutangatanga na baadaye kutafuta kurudi nyumbani. Mungu anasubiri kutupokea.

Na kama yule mwana au binti mwingine, Mungu anatuhimiza kwa upole kufurahi pamoja wakati kila mmoja anaporudi nyumbani Kwake. Anatualika kutengeneza mikusanyiko yetu, akidi, madarasa, na shughuli ziwe wazi, halisi, salama—nyumbani kwa kila mmoja. Kwa ukarimu, uelewa, na kuheshimiana, kila mmoja wetu tunamtafuta Bwana kwa unyenyekevu na kusali na kuzipokea baraka Zake za injili zilizorejeshwa kwa wote.

Safari zetu za maisha ni za mtu binafsi, lakini tunaweza kurudi tena kwa Mungu Baba yetu na Mwanawe Mpendwa kupitia kumtumaini Mungu, kila mmoja na sisi wenyewe.27 Yesu anasema “Usiogope, amini tu.”28 Kama vile alivyofanya Nabii Joseph, bila woga tuweze kutumaini utunzaji wa Baba yetu wa Mbinguni.29 Mpendwa kaka, mpendwa dada, mpendwa rafiki, tafadhali tafuta tena imani na tumaini—muujiza Anaokuahidi hivi leo. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.