Mkutano Mkuu
Kuwa Zaidi katika Kristo: Mfano wa Mteremko
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2021


Kuwa Zaidi katika Kristo: Mfano wa Mteremko

Kwa wakati wa Bwana, siyo mahali gani tunapoanzia, bali ni wapi tunaelekea ndiyo muhimu zaidi.

Nikiwa mvulana mdogo, nilikuwa na matamanio makubwa. Siku moja baada ya shule niliuliza, “Mama, napaswa kuwa nani nikiwa mkubwa: mchezaji wa kulipwa wa mpira wa kikapu au mwanamuziki?” Kwa bahati mbaya, Clark “asiye na meno” hakuonyesha dalili za uanamichezo wa baadaye au utukufu wa muziki. Na licha ya juhudi nyingi, nilikuwa nikikataliwa kuruhusiwa kwenye programu ya juu ya masomo ya shule yangu. Walimu wangu mwishowe walipendekeza nibaki kwenye darasa la kawaida. Baada ya muda, nilijenga tabia za kuridhisha za kujisomea. Lakini haikuwa hivyo mpaka wakati wa misheni yangu huko Japani kwamba nilihisi uwezekano wangu wa kiakili na kiroho ukianza kujitokeza. Niliendelea kufanya kazi kwa bidii. Lakini kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, nilimshirikisha Bwana katika ukuaji wangu, na ilileta mabadiliko.

Picha
Mzee Gilbert akiwa mvulana mdogo
Picha
Mzee Gilbert akiwa mmisionari

Akina kaka na akina dada, katika Kanisa hili, tunaamini katika uwezekano wa kiungu wa watoto wote wa Mungu na katika uwezo wetu wa kuwa kitu zaidi katika Kristo. Kwa wakati wa Bwana, siyo mahali gani tunapoanzia, bali ni wapi tunaelekea ndiyo muhimu zaidi.1

Ili kuonyesha kanuni hii, nitatumia hesabu kadhaa za muhimu. Sasa, usiogope kusikia neno hesabu katika mkutano mkuu. Kitivo chetu cha hesabu cha BYU–Idaho kinanihakikishia kwamba hata anayeanza atashika wazo hili kuu. Linaanza na kanuni ya mstari. Kituo kikuu, kwa ajili ya lengo letu, ni mwanzo wa mstari wetu. Kituo kikuu kinaweza kuwa na mahali pa juu au pa chini pa kuanzia. Mteremko wa mstari kisha unaweza kupinda kwa njia hasi au chanya.

Picha
Slopes and intercepts

Sisi sote tuna vituo tofauti vikuu katika maisha—tunaanzia sehemu tofauti tofauti tukiwa na talanta tofauti na vipawa totauti vya maisha. Wengine huzaliwa na vituo vikuu vya juu, vilivyojaa fursa. Wengine wanakabiliwa na mazingira ya mwanzo ambayo yana changamoto na yanaonekana kutokuwa sawa.2 Kisha tunaendelea kwenye mteremko wa maendeleo binafsi. Baadaye yetu itaamuliwa kidogo sana na mahali petu pa kuanzia na itaamuliwa zaidi na mteremko wetu. Yesu Kristo anaona uwezekano wa kiungu bila kujali wapi tunaanzia. Aliuona kwa mwombaji, mwenye dhambi, na mtu dhaifu. Aliuona kwa mvuvi, mtoza ushuru, na hata yule aliyeshika sana dini. Haijalishi tunaanzia wapi, Kristo anazingatia kile tunachofanya kwa kile tunachopewa.3 Wakati ulimwengu unafokasi kwenye kituo chetu kikuu, Mungu hufokasi kwenye mteremko wetu. Katika hesabu za Bwana, Atafanya kila awezalo kutusaidia kugeuza miteremko yetu kuelekea mbinguni.

Kanuni hii inapaswa kutoa faraja kwa wale wanaosumbuka na kusita kidogo na kufikiri kwa wale wanaoonekana kuwa na kila faida. Acha nianze kwa kuwazungumzia watu walio na mazingira magumu ya kuanzia, ikiwa ni pamoja na umasikini, fursa finyu ya elimu na hali zenye changamoto za kifamilia. Wengine hukabiliana na changamoto za kimwili, vizuizi vya afya ya akili au changamoto kali za kimaumbile.4 Kwa yeyote anayepambana na hatua ya kuanzia yenye ugumu, tafadhali tambua kwamba Mwokozi anafahamu mapambano yako. Yeye “alijichukulia juu yake unyonge [wetu], ili moyo wake [uweze] kujaa rehema, … ili yeye [aweze] kujua … jinsi ya kutusaidia [sisi] kulingana na unyonge [wetu].”5

Acha nishiriki maeneo mawili ya kutia moyo kwa wale wanaokabiliwa na mazingira magumu ya kuanzia. Kwanza, fokasi kule uendako na siyo ulikoanzia. Itakuwa vibaya kupuuza hali zako—ni za kweli na zinahitaji kushughulikiwa. Lakini kufokasi zaidi kwenye hatua ngumu ya kuanzia kunaweza kusababisha hatua hiyo ikufafanue wewe ni nani na pengine kuzuia uwezo wako wa kuchagua.6

Picha
wavulana huko Boston

Miaka kadhaa iliyopita, nilihudumu na kikundi cha vijana wa jiji la Boston, Massachusetts, ambao walikuwa wageni katika injili na kwenye matarajio ya Kanisa. Ilikuwa rahisi kukanganya huruma yangu na kujali kwangu hali zao na hamu ya kushusha viwango vya Mungu.7 Hatimaye niligundua kwamba njia yenye nguvu zaidi ya kuonyesha upendo wangu ilikuwa ni kutopunguza kamwe matarajio yangu. Kwa kila kitu nilichofahamu kufanya, tulifokasi pamoja kwenye uwezekano wao na kila mmoja wao alianza kuinua miteremko yao. Ukuaji wao katika injili ulikuwa wa taratibu lakini imara. Leo wamehudumu misheni, wamehitimu chuo, wamefunga ndoa hekaluni, na wanaishi maisha mazuri binafsi na kwenye kazi.

Picha
Wavulana kutoka Boston wakiwa wamekua

Pili, mshirikishe Bwana katika mchakato wa kuinua mteremko wako. Wakati nikihudumu kama rais wa BYU–Pathway Ulimwenguni, nakumbuka nikiwa nimeketi katika ibada kubwa huko Lima, Peru, ambapo Mzee Carlos A. Godoy alikuwa mnenaji. Alipotazama nje kwenye mkutano huo, alionekana kuzidiwa hisia kuona wanafunzi wengi waaminifu wa chuo kikuu wa kizazi cha kwanza. Pengine akitafakari juu ya njia yake mwenyewe kupitia hali ngumu kama hizo, Mzee Godoy alisema kwa hisia: Bwana “atakusaidia zaidi ya unavyoweza kujisaidia. [Hivyo] mshirikishe Bwana katika mchakato huu.”8 Nabii Nefi alifundisha “kwamba ni kwa neema kwamba tunaokolewa, baada ya kutenda yote tunayoweza.”9 Lazima tufanye kwa jitihada zetu zote,10 ikiwa ni pamoja na toba, lakini ni kupitia neema ya Bwana kwamba tunaweza kutambua uwezekano wetu wa kiungu.11

Picha
Ibada ya BYU–Pathway huko Lima, Peru
Picha
Mzee Godoy akizungumza huko Lima, Peru

Mwisho, acha nishiriki maeneo mawili ya ushauri kwa wale walio na mahala palipoinuka pa kuanzia. Kwanza, je! Tunaweza kuonyesha unyenyekevu kwa hali ambazo hatukuzitengeneza sisi? Kama Rais wa zamani wa BYU Rex E. Lee alivyonukuu kwa wanafunzi wake, “Sote tumekunywa kutoka kwenye visima ambavyo hatukuvichimba na kupata joto kwa mioto ambayo hatukuiukoka.”12 Kisha aliwaomba wanafunzi wake warudishe fadhila hiyo na kujaza visima vya elimu ambavyo waanzilishi wa kale walikuwa wamevijenga. Kushindwa kupanda tena mashamba yaliyopandwa na wengine inaweza kuwa sawa na kurudisha talanta bila ongezeko.

Pili, kufokasi kwenye hatua ya juu ya kuanzia mara nyingi kunaweza kututega kwenye kuhisi kwamba tunastawi wakati kwa kweli, mteremko wetu wa ndani unaweza kuwa umedumaa kabisa. Profesa wa Havard Clayton M. Christensen alifundisha kuwa watu waliofanikiwa zaidi ni wanyenyekevu sana kwa sababu wana ujasiri wa kutosha kurekebishwa na kujifunza kutoka kwa mtu yeyote.13 Mzee D. Todd Christofferson alitushauri “kwa hiari [tutafute njia] za kukubali na hata kutafuta kusahihishwa.”14 Hata wakati mambo yanaonekana kuwa yanakwenda sawa, lazima tutafute fursa za kuwa bora kupitia sala ya kusihi.

Haijalishi ikiwa tunaanza katika hali nzuri au ngumu, tutatambua uwezekano wetu wa juu pale tu tutakapomfanya Mungu kuwa mwenzi wetu. Hivi karibuni nilikuwa na mazungumzo na mwalimu maarufu wa kitaifa ambaye alikuwa akiuliza juu ya mafanikio ya wanafunzi wa BYU-Pathway. Alikuwa mwerevu na swali lake lilikuwa la dhati, lakini kwa hakika alitaka majibu yasiyo ya kidini. Nilishiriki naye mipango yetu ya uhifadhi na juhudi za unasihi. Lakini nilihitimisha kwa kusema, “Haya yote ni mazoea mazuri, lakini sababu halisi ya wanafunzi wetu kuendelea ni kwa sababu tunawafundisha uwezekano wao wa kiungu. Fikiria ikiwa maisha yako yote, uliambiwa huwezi kufanikiwa kamwe. Kisha fikiria matokeo ya kufundishwa kwamba wewe ni mwana au binti halisi wa Mungu mwenye Uwezekano wa kiungu.” Alitulia, kisha akajibu kwa upole, “Hiyo ina nguvu.”

Akina kaka na akina dada, moja ya miujiza ya hili, Kanisa la Bwana, ni kwamba kila mmoja wetu anaweza kuwa kitu zaidi katika Kristo. Sifahamu taasisi nyingine yoyote ambayo huwapa waumini wake fursa zaidi za kutumikia, kurudisha, kutubu, na kuwa watu bora. Iwe tunaanza katika hali nzuri au ngumu, acha tuweke macho yetu na miteremko yetu kuelekea mbinguni. Tunapofanya hivyo, Kristo atatuinua mahali pa juu. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona Clark G. Gilbert, “The Mismeasure of Man” (BYU–Pathway Worldwide devotional, Jan. 12, 2021), byupathway.org/speeches. Katika ujumbe huu nilichunguza jinsi ambavyo ulimwengu mara nyingi hukosea kupima uwezekano wa binadamu. Hata watu waliosifika wanaotumia kazi muhimu ya wanasaikolojia wanaoongoza ambao hutetea dhana za ujasiri (Angela Duckworth) na mawazo ya ukuaji (Carol S. Dweck) hudharau uwezo halisi wa kibinadamu wanapotegemea tu mifumo waliyojifunza na kupuuza uwezekano wetu wa kiungu katika Kristo.

  2. Ona Dale G. Renlund, “Ya Kukasirisha Yasiyo Haki,” Liahona, Mei 2021, 41–45.

  3. Ona Mathayo 25:14–30. Katika mfano wa talanta, kila mtumishi alipokea idadi tofauti ya talanta kutoka kwa bwana wao. Lakini hukumu haikuamuliwa kwa kile walichopokea bali kwa jinsi kilivyosimamiwa. Ilikuwa ni ongezeko ambalo lilimwongoza Bwana kusema, “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu: ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi” (Mathayo 25:21).

  4. Ona Mosia 3:19. Maana moja inaweza kuwa kwamba kufichua kwetu mvuto wa mwanadamu wa tabia ya asili kunaweza kuwa tofauti kutokana na utofauti wa kimaumbile. Kama vile ambavyo kila mmoja amepewa vipawa tofauti, pia tuna changamoto tofauti za mwili, akili, na hisia ambazo lazima tujifunze kuzisimamia na kuzishinda.

  5. Alma 7:11–12. Kristo siyo tu anatusaidia kushinda dhambi zetu kupitia toba, lakini anajua jinsi ya kutufariji katika shida za maisha yetu kwa sababu kupitia Upatanisho amehisi na kushinda mateso yote ya wanadamu.

  6. Mzee David A. Bednar anatukumbusha kwamba sisi ni mawakala na kwamba tunapaswa kujitendea. Tunapojitambulisha kwa vitambulisho vya ulimwengu, tunazuia uwezekano wetu wa kiungu na, kwa kufanya hivyo, tunazuia uwezo wetu wa kuchagua. (Ona David A. Bednar, “Na Hakuna Kitakachowakwaza,” Liahona, Nov. 2006, 89–92.)

  7. Ona Russell M. Nelson, “The Love and Laws of God” (Brigham Young University devotional, Sept. 17, 2019), speeches.byu.edu. Katika ibada hii ya BYU, Rais Nelson anafundisha kwamba kwa sababu Mungu na Mwanaye wanatupenda, wametupatia sheria na matarajio ambayo yatatusaidia. “Sheria za Mungu zinaonyesha upendo wake mkamilifu kwa kila mmoja wetu. Sheria zake zinatuweka salama kiroho na zinatusaidia kuendelea milele” (ukurasa wa 2).

  8. Carlos A. Godoy, BYU–Pathway Connections Conference, Lima, Peru, Mei 3, 2018.

  9. 2 Nefi 25:23.

  10. Wazazi wangu walianzisha kauli mbiu ya familia ya Gilbert ya “FANYA KWA JUHUDI ZAKO ZOTE.” Njia nyingine ya kuuongelea mfano huu wa mteremko ni kusisitiza kwamba kama tutafanya kwa juhudi zetu zote, tunaweza kuamini kwamba Bwana ataingilia na kuleta tofauti.

  11. Ona Clark G. Gilbert, “From Grit to Grace” (BYU–Pathway Worldwide devotional, Sept. 25, 2018), byupathway.org/speeches. Katika ujumbe huu ninatafiti wazo kwamba ingawa lazima tujifunze kufanya kazi kwa bidii na kukuza mifumo madhubuti ya nidhamu, kutambua uwezekano wetu wa kweli katika Yesu Kristo, lazima tujifunze kutumia neema Yake.

  12. Rex E. Lee, “Some Thoughts about Butterflies, Replenishment, Environmentalism, and Ownership” (Brigham Young University devotional, Sept. 15, 1992), 2, speeches.byu.edu; ona pia Kumbukumbu la Torati 6:11.

  13. Ona Clayton M. Christensen, “How Will You Measure Your Life?,” Harvard Business Review, July–Aug. 2010, hbr.org. Ujumbe huu ulitolewa hapo awali kama hotuba ya Siku ya Darasa iliyotolewa kwenye mahafali ya Kitivo cha Biashara cha Havard. Katika ujumbe huu, profesa Christensen aliwatahadharisha wanafunzi wake kutotenganisha ujasiri na unyenyekevu, akiwakumbusha kwamba ili kuendelea kusonga mbele katika maisha watahitaji kuwa wanyenyekevu kiasi cha kutosha kutafuta marekebisho na kujifunza kutoka kwa wengine.

  14. D. Todd Christofferson, “Wengi Kadiri Niwapendao, Ninawarudi na Kuwakemea,” Liahona, Mei 2011, 97.