Mkutano Mkuu
Amani Binafsi katika Nyakati zenye Changamoto
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2021


Amani Binafsi katika Nyakati zenye Changamoto

Kamwe haijawa muhimu zaidi kutafuta amani binafsi.

Hivi karibuni niliteuliwa kuweka wakfu sehemu ya kihistoria ya Nauvoo. Kama sehemu ya uteuzi, niliweza kutembelea Jela ya Liberty iliyopo Missouri. Nilipoiangalia jela, nilitafakari matukio ambayo yaliifanya iwe sehemu ya muhimu mno ya historia ya Kanisa. Maisha ya watakatifu yalitishiwa kutokana na amri ya kuangamiza iliyotolewa na gavana wa Missiouri. Kwa nyongeza, Nabii Joseph na wenzi wachache teule walikuwa wamefungwa bila haki katika jela ya Liberty. Moja ya sababu ya upinzani mkali sana kwa waumini wenzetu ilikuwa karibu wote walikuwa wanapinga utumwa.1 Mateso haya makali ya Joseph Smith na wafuasi wake yanaanzisha mfano mkubwa mno wa matumizi maovu ya haki ya kujiamulia ambayo yanaweza athiri watu waadilifu. Muda wa Joseph ndani ya Jela ya Liberty unaonesha kwamba dhiki si ushahidi wa Bwana kutotupenda, au uondoaji wa baraka Zake.

Nilihamasika sana niliposoma kile nabii Joseph Smith alichotamka aliokuwa amezuiliwa ndani ya Jela ya Liberty: “ Ee Mungu, uko wali? Na ni wapi lilipo hema lifichalo mahali pako pa kujificha?”2 Joseph aliuliza mpaka lini watu wa Bwana “watateseka mabaya haya na mateso kinyume cha sheria.”3

Picha
Mzee Cook akitembelea Jela ya Liberty

Nilipokuwa nimesimama ndani ya Jela ya Liberty, niliguswa sana niliposoma jibu la Bwana: “Mwanangu, amani iwe katika nafsi yako; taabu yako na mateso yako yatakuwa kwa muda mfupi; na halafu, kama utastahimili vyema, Mungu atakuinua juu.”4 Ni wazi kwamba upinzani unaweza kututakasa kwa ajili ya majaliwa ya milele selestia.5

Maneno ya thamani ya Mwokozi “Mwanagu, amani iwe katika nafsi yako”6 yanavuma ndani yangu binafsi na yana umuhimu mkubwa kwa siku zetu. Yananikumbusha juu ya mafundisho Yake kwa wafuasi wa Yesu wakati wa Huduma Yake duniani.

Kabla ya mateso ya Kristo katika bustani ya Gethsemane na juu ya msalaba, Aliwaamuru mitume Wake “kupendana wao kwa wao; kama nilivyo wapenda”7 na kwa hiyo aliwafariji na maneno haya: “Amani nawaachieni, amani yangu nawapeni: sio kama ulimwengu utoavyo, niwapavyo Mimi. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.”8

Moja ya majina yaliyohifadhiwa kwa upendo mkubwa ya Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, ni Mwana Mfalme wa Amani.”9 Hatimaye ufalme Wake utaanzishwa pamoja na amani na upendo milele.10 Tunatazamia utawala wa milenia wa Masiya.

Bila kujali ono hili la utawala wa milenia, tunajua kwamba amani ya dunia na upatanifu hazijaenea katika siku zetu.11 Katika maisha yangu, kamwe sijawahi kuona ukosefu mkubwa wa unyenyekevu. Tunashambuliwa na lugha ya hasira, ukinzani na kuchukiza, matendo ya kuharibu ambayo yanaharibu amani na utulivu.

Amani ulimwenguni haijaahidiwa wala kudhibitishwa mpaka Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Mwokozi aliwafunza Mitume Wake kwamba kazi Yake ya duniani haitafanikisha amani kwa watu wote. Alifundisha, “Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani.”12 Amani duniani kote haikuwa sehemu ya kwanza ya kazi ya Mwokozi duniani. Amani ya kilimwengu haipo siku hizi.

Hata hivyo, amani binafsi inaweza kupatikana licha ya hasira, ubishi, na mgawanyiko ambao unaharibu na kuchafua ulimwengu wetu leo. Kamwe haijawa muhimu zaidi kutafuta amani binafsi. Wimbo mpya mzuri na pendwa ulioandikwa kwa ajili ya vijana wa leo na Kaka Nik Day uitwao “Peace in Christ” unatamka, “Wakati hakuna amani duniani, kuna amini katika Kristo.”13 Tulibarikiwa kuwa na wimbo huu kabla tu ya janga la ulimwenguni kote COVID-19.

Wimbo huu unaakisi katika mtindo mzuri hamu kwa ajili ya amani na kwa kufaa unasisitiza amani ile imetia nanga katika maisha na kazi ya Yesu Kristo. Rais Joseph F. Smith alitamka , “Kamwe haiwezekani kuwepo duniani Roho yule wa amani na upendo … hadi wanadamu watakapopokea ukweli wa Mungu na ujumbe wa Mungu … na kuutambua uwezo na mamlaka yake ambayo ni ya kimungu.”14

Wakati kamwe hatutarudi nyuma kutoka kutoka juhudi za kufanikisha amani ulimwenguni kote, tumehakikishiwa kwamba tunaweza kuwa na amani binafsi, kama waalimu wa Kristo. Kanuni hii imewekwa katika Mafundisho na Maagano: “Lakini, jifunzeni kwamba yule afanyaye kazi za haki atapokea ujira wake, hata amani katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao.”15

Ni zipi baadhi ya “kazi za uadilifu” ambazo zitatusaidia kushughulikia mabishano, na kupunguza ukinzani na kupata amani katika ulimwengu huu. Mafundisho yote ya Kristo yanaonesha kwenye mwelekeo huu. Nitataja chache ambazo ninaamini kwa kipekee ni muhimu.

Kwanza: Mpende Mungu, Ishi Amri Zake, na Samehe Kila Mtu

Rais George Albert Smith akawa Rais wa Kanisa mnamo mwaka 1945. Alikuwa anajulikana wakati wa miaka yake kama Mtume kama kiongozi mpenda-amani. Katika miaka 15 iliyotangulia kabla hajawa Rais, changamoto na majaribu ya mdororo mkubwa kwa kiuchumi ulimwenguni kote, ukifuatiwa na kifo na uharibifu wa Vita vya Dunia II, ulikuwa chochote bali amani.

Mwishoni mwa Vita vya Dunia II, wakati wa mkutano wake wa kwanza kama Rais mnamo mwezi wa Oktoba mwaka 1945, Rais Smith aliwakumbusha Watakatifu juu ya mwito wa Mwokozi kuwapenda majirani zao na kuwa samehe maadui zao na kisha alifundisha, “Hio ndio roho Watakatifu wote wa Siku za Mwisho wanapaswa kuitafuta kuwa nayo kama wana matumaini siku moja kusimama katika uwepo Wake na kupokea kwenye mikono yake mitukufu karibu nyumbani.”16

Pili: Tafuta matunda ya Roho

Mtume Paulo katika waraka wake kwa Wagalatia aliweka mbele mgawo wa sehemu mbili kati ya kazi za uadilifu ambazo zinatufanya tustahili kurithi ufalme wa Mungu na kazi ambazo zinaweza, bila kutubu, kutubatilisha. Miongoni mwa hizo ambazo zinatustahilisha ni matunda ya roho “upendo, furaha, amani, uvumilivu, uungwana, hisani, imani, upole, [na] kiasi.”17 Paulo pia inajumuisha kuubeba mzigo wa mwenzio na kutokuchoka katika kutenda mema.18 Miongoni mwa kazi hizo ambazo sio adilifu anajumuisha chuki, ghadhabu, na hasira, na ugomvi.19

Moja ya masomo makuu katika kipindi cha Agano la Kale alilihusisha Baba Ibrahimu. Ibahimu na Lutu, mpwa wake, walikuwa matajiri, bali wakakuta hawakuweza kuishi pamoja. Kuondoa ugomvi, Ibrahimu alimruhusu Lutu kuchagua arthi aliyoipenda. Lutu alichagua uwanda wa Yordani, ambao ulikuwa na maji mengi na mzuri. Ibrahimu alichukuwa uwanda wenye rutuba chache wa Mamre. Maandiko yanasema kwamba Ibrahimu kisha akapiga hema yake na alijenga “madhabahu kwa Bwana.”20 Lutu, kwa upande mwingine, “alipiga hema yake kuelekea Sodoma.”21 Kuwa na mahusiano ya amani, somo ni wazi tunapaswa kuwa tayari kukubaliana kuondoa ugomvi kuhusu mambo ambayo hayahusishi uadilifu. Kama Mfalme Benyamin alivyofundisha, “Hutakuwa na nia ya kuumizana, bali kuishi kwa amani.”22 Bali kwa tabia inayohusiana na uadilifu na masharti ya kimafundisho, tunahitaji thabiti na imara.

Kama tunataka kuwa na amani ambayo ni zawadi ya kazi za uadilifu, hatuta piga hema zetu kuelekea ulimwengu. Tutapiga hema zetu kuelekea hekaluni.

Tatu: Tumia Uhuru wa Kujiamulia Kuchagua Uadilifu

Amani na uhuru wa kujiamulia zimesokotana kama vitu muhimu kwa mpango wa wokovu. Kama ilivyoelezwa katika makala ya Mada ya Injili kwenye “Uhuru wa Kujiamulia na Uwajibikaji,” “Uhuru wa kujiamulia ni uwezo na heshima Mungu anayotupa kuchagua na kutenda kwa ajili yetu wenyewe.”23 Kwa hiyo, uhuru wa kujiamulia ni moyo wa ukuaji binafsi na uzoefu ambao unatubariki sisi tunapomfuata Mwokozi.24

Uhuru wa kujiamulia ulikuwa swala la kanuni katika baraza la kabla ya kuja duniani kule mbinguni na vita kati ya wale waliochagua kumfuata Kristo na wafuasi wa Shetani.25 Kuacha kiburi na kuongoza na kumchagua Mwokozi kutaturuhusu kuwa na nuru Yake na amani Yake. Bali amani binafsi ingetiwa changamoto wakati watu walipotumia uhuru wao wa kujiamulia katika njia ya kudhuru na kuchukiza.

Nina imani kwamba uhakika wa amani tuliohisi katika mioyo yetu uliimarishwa na uelewa tuliokuwa nao wa nini Mwokozi wa ulimwengu angekamilisha kwa niaba yetu. Hii imewekwa kwa uzuri katika Hubiri Injili Yangu: Tunapotegemea juu ya upatanisho wa Yesu Kristo, Yeye anaweza kutusaidia kuvumilia majaribu yetu, magojwa, na uchungu wetu. Tunaweza kujazwa na furaha, amani, na faraja. Yale yote ambayo si haki juu ya maisha yanaweza kufanywa sahihi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.”26

Nne: Jenga Sayuni katika Mioyo Yetu na Majumbani

Sisi ni watoto wa Mungu na sehemu ya familia Yake. Sisi pia ni sehemu ya familia ambayo tumezaliwa. Taasisi ya familia ni msingi kwa vyote furaha na amani. Rais Russell M. Nelson ametufundisha—na wakati janga hili tumejifunza—kwamba Kanisa lenye kiini-nyumbani-linalosaidiwa kanuni za dini, linaweza “kuachia huru nguvu za familia … kubadilisha [nyumba] [zetu] mahali patakatifu pa imani.”27 Kama tuna kanuni hizi za dini katika nyumba zetu, pia tutakuwa na amani ya Mwokozi.28 Tunafahamu kwamba wengi wenu hamna baraka za nyumba adilifu na kushindana mara kwa mara na wale wanaochagua uovu. Mwokozi anaweza kutoa ulinzi na amani kukuongoza wewe hatimaye kwenye usalama na kimbilio kutoka tufani za maisha.

Ninawakikishieni kwamba furaha, upendo, na kuridhika kunakopatikana katika familia yenye upendo na adilifu hutoa vyote amani na furaha. Upendo na huruma viko kwenye kiini cha kuwa na Sayuni katika mioyo yetu na majumbani.29

Tano: Kufuata Onyo la Sasa la Nabii Wetu

Amani yetu imeongozwa kwa wingi wakati tunapomfuata nabii wa Bwana, Rais Russell M. Nelson. Punde tutakuwa na fursa ya kusikia kutoka kwake. Alijitayarisha kutoka mwanzo wa ulimwengu kwa ajili ya wito huu. Matayarisho Yake binafsi yamekuwa yasiyo na kifani.30

Ametufundisha kwamba tunaweza “kuhisi kuvumilia amani na furaha hata nyakati za ghasia” tunapojitahidi kuwa zaidi kama Mwokozi wetu, Yesu Kristo.31 Ametushauri “kutubu kila siku” kupokea utakaso wa Bwana, uponyaji, na nguvu ya kutuimarisha.32 Mimi ni shahidi binafsi kwamba ufunuo umepokelewa na unaendelea kupokelewa kutoka mbinguni na nabii wetu mpendwa.

Wakati tunaheshimu na kumkubali kama nabii wetu, tunamwabudu Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Tunahudumiwa na Roho Mtakatifu.

Ninashuhudia na kutoa ushahidi wangu binafsi wa kitume kwamba Yesu Kristo, Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu, analiongoza na kulilinda Kanisa Lake la urejesho. Maisha yake na kazi ya upatanisho ni vyanzo vya kweli vya amani. Yeye ni Mwana Mfalme wa Amani. Ninatoa ushahidi wangu wa uhakika na dhati kwamba Yeye Anaishi. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. “Watu katika Independence hawakutaka kwamba Watakatifu walihubiri kwa Wahindi na hawakupendelea utumwa” (Saints: The Story of the Church of Jesus Christ in the Latter Days, vol. 1, The Standard of Truth, 1815–1846 [2018], 172).

  2. Mafundisho na Maagano 121:1.

  3. Mafundisho na Maagano 121:3.

  4. Mafundisho na Maagano 121:7–8.

  5. Ona 2 Nefi 2:11–15.

  6. Mafundisho na Maagano 121:7.

  7. Yohana 13:34.

  8. Yohana 14:27.

  9. Isaya 9:6; 2 Nefi 19:6. “Mwokozi katika ibada yake ya kubariki pia alifundisha,”Heri wote walio wapatanishi: kwani wataitwa watoto wa Mungu.” (Mathayo 5:9).

  10. “Kwa hukumu na kwa haki … hata milele” (ona Isaya 9:6–7; 2 Nefi 19:6–7; ona pia Wagalatia 5:22).

  11. Ona Mafundisho na Maagano 1:35. Rais Wilford Woodruff alitangaza hivi katika mwaka wa 1894 na tena katika 1896 (ona Hotuba za Wilford Woodruff, ed. G. Homer Durham (19460), 251–52; ona pia Marion G.Romney, katika Repoti ya Mkutano Mkuu, Apr.1967, 79–82; Ezra T. Benson, “Nguvu ya Neno,” Ensign, Apr. 1986, 79–80; Dallin H. Oaks, “Matayarisho kwa ajili ya Ujio wa Pili,” Liahona, Mei 2004, 9.

  12. Mathayo 10:34.

  13. Nik Day, “Peace in Christ,” 2018 Mutual theme song, Liahona, Jan. 2018, 54–55; New Era, Jan. 2018, 24–25. Wimbo “Peace in Christ” unafundisha:

    Tunapoishi Yeye Alivyoishi

    Kuna amani katika Kristo.

    Anatupa

    Tumaini linapopotea

    Yeye hutupa nguvu

    Tuzidiwapo.

    Yeye hutupa Hifadhi

    Penye dhoruba maishani.

    Amani itowekapo duniani.

    Kuna amani katika Kristo.

  14. Teachings of Presidents of the Church: Joseph F. Smith (1998), 400.

  15. Mafundisho na Maagano 59:23.

  16. Ona George Albert Smith, katika Ripoti ya Mkutano, Oktoba 1945, 169-70.

  17. Wagalatia 5:22–23

  18. Ona Wagalatia 6:2, 9.

  19. Ona Wagalatia 5:20.

  20. Mwanzo 13:18.

  21. Mwanzo 13:12.

  22. Mosiah 4:13.

  23. Mada za Injili, “Uhuru wa Kujiamulia na Uwajibikaji,” topics.ChurchofJesusChrist.org

  24. Tupo “huru kuchagua uhuru na maisha ya millele, kupitia mpatanishi mkuu wa watu wote.”2 Nefi 2:27 Uhuru wa Kuchagua tena unarusu kuharibu chaguzi ovu za wengine kusababisha maumivu na kuteseka na wakati mwingine kifo. Maandiko yanaweka wazi kwamba Bwana Mungu alitoa uhuru wa kuchagua ili kwamba mtu aweze kuchagua mema au uovu.2 Nefi 2:16

  25. Mada za Injili, “Uhuru wa Kujiamulia na Uwajibikaji,” topics.ChurchofJesusChrist.org

  26. Preach My Gospel: A Guide to Missionary Service (2019), 52–108

  27. Russell M. Nelson, “Kuwa Watakatifu wa Siku za Mwisho wa Mfano,” Liahona, Nov. 2018, 113.

  28. Ona Mafundisho na Maagano 19:23.

  29. Nlikuwa na bahati ya kukulia katika nyumba ambayo amani ilienea. i Hii ilikuwa kimsingi kutokana na ushawishi wa mama yetu ambaye alikuwa muumini mwaminifu wa Kanisa. Baba yangu alikuwa wa kipekee kwa kila njia lakini alikuwa asiye shiriki kikamilifu. Mama alimheshimi baba yetu na aliepuka mabishano. Alitufundisha sisi kama watoto kudali na kuhudhuria Kanisani. Pia alitufundisha kupenda na kuhudumiana (ona Mosia 4:14-15). Kukua katika katika nyumba kama ile kulileta amani na kumekuwa baraka kubwa katika maisha yangu.

  30. Russell M. Nelson alihitimu kutoma Chuo kikuu cha Utah Shule ya Tiba wa kwanza katika darasa lake akiwa na umri wa miaka22. Muda mrefu amekuwa akitamani kuwa mganga mpasuaji na alipata mafunzo yaliyopatikana kwenye vyuo vikubwa vya matibabu. Kwa uamunifu alitimiza majukumu ya jeshi Korea na Japan. Kwa miaka mingi alikuwa mwanzilishi katika upasuaji wa wazi wa moyo na alitambulika ulimwengunu kote. Kwa kusifika kama maandalizi haya yalikuwa ya kubariki watu ulimwengunu kote kwa utaalamu wake wa kitibabu, matayarisho ya kiroho ya Rais Nelson yalikuwa muhimu zaidi ya hapo. Yeye ni baba wa familia kubwa, wajukuu, na vitukuu. Kwa uaminifu amehudumia familia yake na kanisa maisha yake.

  31. Russell M. Nelson, “Ujumbe wa Ufunguzi,” Liahona, Mei. 2020, 6; ona pia Russell M. Nelson, “Furaha na Wokovu wa Kiroho,” Liahona, Nov. 2016, 81-84.

  32. Russell M. Nelson, “Ujumbe wa Ufunguzi,” 6.