Misaada ya Kujifunza
TJS, Warumi 8


TJS, Warumi 8:8. Linganisha na Warumi 8:8

Wale waishio kulingana na njia za mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

8 Hivyo basi wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

TJS, Warumi 8:29–30. Linganisha Warumi 8:29–30

Yesu Kristo aliwatakasa walio na haki katika kuwatayarisha kwa wokovu wao.

29 Kwa yeye ambaye alimjua kabla, pia alimjalia afanywe sawa na mfano wake, ili awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

30 Hata hivyo, yule ambaye alimjalia, yeye pia alimwita; na yeye ambaye alimwita, na yeye pia alimtakasa, na yeye aliyemtakasa yeye pia alimtukuza.