Misaada ya Kujifunza
TJS, Warumi 7


TJS, Warumi 7:5–27. Linganisha na Warumi 7:5–25

Ni Kristo pekee aliye nauwezo wa kufanya mageuzi ya kudumu ya roho za wanadamu.

5 Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, ambazo hazikuwako kulingana na sheria, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata kuzalia mauti matunda.

6 Bali sasa tumefunguliwa kutoka katika sheria tulimokuwa tumeshikiliwa, tukiwa tumekufa kwa sheria, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, na si katika hali ya zamani ya andiko.

7 Tusemeje basi? Sheria ni dhambi? Mungu anakataza. La, nisingalitambua dhambi, ila kwa sheria; kwa kuwa nisingalijua kutamani, kama sheria isingalisema, Usitamani.

8 Lakini dhambi, ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana pasipo sheria dhambi ilikuwa imekufa.

9 Maana nalikuwa hai hapo kwanza bila ya uvunjaji wa sheria, ila ilipokuja amri ya Kristo dhambi ilihuika, nami nikafa.

10 Nami nilipokosa kuamini amri ya Kristo iliyokuja, ambayo iliwekwa kwa uzima niliona kwangu mimi ilileta mauti.

11 Kwa maana dhambi, kwa kupata nafasi kwa ile amri na ikanidanganya; na kwa hiyo ikaniua.

12 Hata hivyo, niliona ya kuwa sheria ni takatifu, na ile amri kuwa ni takatifu, na ya haki, na njema.

13 Basi je ile iliyo njema ilifanya mauti kwangu mimi? Mungu anakataza. Bali dhambi, ilifanya mauti ndani yangu mimi ili ipate kuonekana dhambi kwa ile iliyo njema ikitenda mauti ndani yangu, ili dhambi, kwa ile amri izidi kuwa mbaya mno.

14 Kwa maana twajua ya kuwa amri ni ya kiroho; lakini nilipokuwa chini ya sheria, nilikuwa bado kimwili, niliyeuzwa chini ya dhambi.

15 Lakini sasa mimi ni wa kiroho; kwa maana kile niamriwacho kutenda, nakitenda; na kile niamriwacho kutokuruhusu, sikiruhusu.

16 Kwa maana kile nijuacho si sahihi, sitakifanya; kwa maana kile kilicho dhambi, ninakichukia.

17 Basi kama nikitenda lile ambalo nisingeliruhusu, naikiri ile sheria, ya kuwa ni njema; nami sihukumiwi.

18 Basi sasa, si mimi nafsi yangu ninayetenda dhambi; bali ninatafuta kuitiisha ile dhambi ikaayo ndani yangu.

19 Kwa maana ninajua ya kuwa ndani yangu, ambamo ni ndani ya mwili wangu, halikai jambo jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lile lililo jema sipati, isipokuwa tu kwa njia ya Kristo.

20 Kwa maana lile lililo jema ambalo ningelifanya nikiwa chini ya sheria, silioni kuwa ni jema; kwa hiyo, silitendi.

21 Bali lile ovu ambalo nisingelifanya chini ya sheria, ninaliona kuwa ni jema; hilo nalitenda.

22 Sasa kama nikitenda lile ambalo, kwa njia ya msaada wa Kristo, nisingelitenda chini ya sheria, mimi sipo chini ya sheria; na hivyo sitafuti tena kufanya mabaya, bali kuitiisha dhambi ile ikaayo ndani yangu.

23 Basi ninaona kwamba chini ya sheria, kwamba wakati ambapo ningelitenda jema ovu lilikuwa pamoja nami; kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani.

24 Na sasa ninaona sheria nyingine, hata amri ya Kristo, nayo imepigwa chapa akilini mwangu.

25 Lakini viungo vyangu vinapiga vita dhidi ya sheria ya akili yangu, na kunileta katika utumwa wa sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.

26 Na ikiwa siitishi ile dhambi iliyo ndani yangu, bali kwa mwili naitumikia sheria ya dhambi; Ole wangu maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa kutoka mwili huu wa mauti?

27 Namshukuru Mungu, kupitia Yesu Kristo Bwana wetu, basi, kama ni hivyo mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu.