Misaada ya Kujifunza
TJS, Warumi 3


TJS, Warumi 3:5–8. Linganisha na Warumi 3:5–8

Paulo anafundisha kwamba mtu hawezi kufanya uovu kusababisha mema.

5 Lakini kama tutabaki katika kutokuwa kwetu waadilifu na kutukuza uadilifu wa Mungu, tunawezaje kuwa na ujasiri wa kusema, Mungu sio mwadilifu anayelipa kisasi? (Ninazungumza kama mtu amwogopae Mungu,)

6 Mungu na aepushe; kwani Mungu atahukumu vipi ulimwengu?

7 Kwani kama ukweli wa Mungu umesheheni kupitia uongo wangu, (kama wanavyoita Wayahudi,) katika utukufu wake; kwa nini bado mimi pia nahukumiwa kama mwenye dhambi? Na sipokelewi? Kwa sababu sisi tumeripotiwa kikashfa;

8 Na baadhi wanakiri kile tunachosema, (ambao laana yao ni ya haki,) Wacha tufanye dhambi ili mema yaweze kuja. Lakini huu ni uongo.