Misaada ya Kujifunza
TJS, Warumi 4


TJS, Warumi 4:2–5. Linganisha na Warumi 4:2–5

Watu wanaweza tu kuokolewa kwa neema ya Yesu Kristo, sio kwa kutenda yale yanayo husiana na kushika sharia ya Musa.

2 Kwani kama Ibrahimu alihalalishwa na sheria ya matendo, analo la kujisifia; lakini sio lililo la Mungu.

3 Kwani maandiko yanasema nini? Ibrahimu alimwamini Mungu, na alihesabiwa mwenye haki.

4 Sasa kwa yule aliye halalishwa na sheria ya matendo, zawadi yake inahesabika, sio kama neema bali kama deni.

5 Lakini kwa yeye ambaye hatafuti kuhalalishwa na sheria ya matendo, lakini anamwamini asiye halalisha uovu, imani yake ina hesabiwa kuwa haki.

TJS, Warumi 4:16. Linganisha na Warumi 4:16

Vyote imani na matendo, kwa njia ya neema, ni muhimu kwa wokovu.

16 Kwa hiyo ninyi mnahesabiwa haki kwa imani na matendo, kwa njia ya neema, ili ahadi ipate kuwa imara kwa uzao wote; si kwa wale walio wa sheria tu, bali na kwa wale walio wa imani ya Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote,