Maandiko Matakatifu
Alma 36


Amri za Alma kwa mwana wake Helamani.

Yenye milango ya 36 na 37.

Mlango wa 36

Alma anashuhudia kwa Helamani uongofu wake baada ya kuona malaika—Alivumilia maumivu ya roho iliyolaaniwa; akamwomba Yesu, na ndipo akazaliwa katika Mungu—Shangwe tamu iliijaza roho yake—Aliona makundi ya malaika yakimsifu Mungu—Wengi waliobadilika wameonja na kuona vile amevyonja na kuona. Karibia mwaka 74 K.K.

1 aMwana wangu, sikiliza maneno yangu; kwani naapa kwako, kwamba kadiri utakavyoweka amri za Mungu ndivyo utafanikiwa katika nchi.

2 Ningetaka kwamba ufanye vile nimevyofanya, kwa kukumbuka autumwa wa babu zetu; kwani walikuwa katika utumwa, na hapakuwa na yeyote ambaye angewaokoa isipokuwa awe bMungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo; na kwa kweli aliwakomboa katika mateso yao.

3 Na sasa, Ee mwana wangu Helamani, tazama, wewe ni kijana, na kwa hivyo, nakuomba wewe kwamba usikilize maneno yangu na ujifunze kutoka kwangu; kwani najua kwamba wote watakaoweka imani yao katika Mungu watasaidiwa kwa amajaribio yao, na taabu zao, na mateso yao, na bwatainuliwa juu katika siku ya mwisho.

4 Na sitaki kwamba ufikiri kwamba animejua mwenyewe—sio kwa bkimwili lakini kwa kiroho, sio kwa mawazo ya kimwili lakini ya Mungu.

5 Sasa, tazama, nakwambia, ikiwa anisingezaliwa kwa Mungu bnisingekuwa nimejua vitu hivi; lakini Mungu, kwa mdomo wa malaika wake mtakatifu, amethibitisha vitu hivi kwangu, sio kwa sababu ya cwema wangu;

6 Kwani nilienda na wana wa Mosia, nikinuia akuharibu kanisa la Mungu; lakini tazama, Mungu alimtuma malaika wake mtakatifu kutuzuia tulipokuwa njiani.

7 Na tazama, alituzungumzia, kwa sauti kama ya radi, na ardhi yote ailitetemeka chini ya miguu yetu; na sisi sote tuliinama kwenye ardhi, kwani bhofu ya Bwana ilitujia.

8 Lakini tazama, sauti iliniambia: Amka. Na niliamka na kusimama wima, na nikaona malaika.

9 Na akaniambia: Ikiwa hutaki kuangamizwa mwenyewe, usijaribu tena kuangamiza kanisa la Mungu.

10 Na ikawa kwamba niliinama kwenye ardhi; na ilikuwa kwa muda wa siku atatu usiku na mchana kwamba nisingefungua kinywa changu, wala kutumia viungo vyangu.

11 Na malaika alinizungumzia vitu vingi zaidi, ambavyo vilisikika na ndugu zangu, lakini mimi sikuvisikia; kwani wakati niliposikia maneno—Ikiwa hutaki kujiangamiza mwenyewe, usijaribu tena kuliangamiza kanisa la Mungu—Nilipigwa na woga mwingi sana na mshangao kwa hofu kwamba ningeangamizwa, kwamba niliinama kwenye ardhi na sikusikia tena.

12 Lakini nilisumbuliwa na adhabu ya amilele, kwani roho yangu iliteseka kwa kiasi kikubwa sana na kuadhibiwa kwa dhambi zangu zote.

13 Ndiyo, nilikumbuka dhambi zangu zote na uovu, kwa ajili hiyo aniliadhibiwa na uchungu wa jehanamu; ndiyo, niliona kwamba nimeasi dhidi ya Mungu wangu, na kwamba sikuwa nimetii amri zake.

14 Ndiyo, na nilikuwa nimeua watoto wake wengi, au kwa usahihi zaidi niliwaelekeza kwenye maangamizo; ndiyo, na kwa ufupi uovu wangu ulikuwa mwingi sana kwamba ile fikira ya kukaribia uwepo wa Mungu wangu iliiadhibu nafsi yangu kwa hofu kuu isiyoelezeka.

15 Ee, nilifikiri, kwamba aningefukuzwa na kutokuwepo kwa nafsi wala mwili, kwamba nisingeletwa kusimama kwenye uwepo wa Mungu wangu, kuhukumiwa kwa bvitendo vyangu.

16 Na sasa, kwa siku tatu usiku na mchana niliteseka, hata na uchungu wa anafsi iliyolaaniwa.

17 Na ikawa kwamba wakati nilipoteseka na maumivu mabaya, wakati anilihuzunishwa na ufahamu wa dhambi zangu nyingi, tazama, nilikumbuka pia kusikia baba yangu akitoa unabii kwa watu kuhusu kuja kwa mmoja aitwaye Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, kulipia dhambi za ulimwengu.

18 Sasa, nilipofikiria wazo hili, nililia ndani ya moyo wangu: Ee Yesu, wewe Mwana wa Mungu, nihurumie, mimi ambaye anina uchungu, na nimezungukwa na bminyororo ya kifo kisicho na mwisho.

19 Na sasa, tazama, nilipofikiri hivi, sikukumbuka uchungu wangu tena; ndiyo, asikuteseka na ufahamu wa dhambi zangu tena.

20 Na Ee, ni ashangwe gani, na ni mwangaza gani wa ajabu niliouona; ndiyo, nafsi yangu ilijazwa na shangwe ya ajabu kama vile ulivyokuwa uchungu wangu!

21 Ndiyo, nakwambia, mwana wangu, kwamba hakungekuwa na chochote kilichokuwa kikali vile na kichungu vile ulivyokuwa uchungu wangu. Ndiyo, na tena ninakwambia, mwana wangu, kwamba upande mwingine, hapawezi kuwa na kitu kizuri hivyo na kitamu kama vile ilivyokuwa shangwe yangu.

22 Ndiyo, nilidhani niliona, hata vile babu yetu aLehi alivyomwona, Mungu akiketi kwenye kiti chake cha enzi, akizungukwa na umati usiohesabika wa malaika, kwa hali ya kuimbia na kumsifu Mungu wao; ndiyo, na nafsi yangu ilitamani kuwa hapo.

23 Lakini tazama, viungo vyangu vilipata anguvu tena, na nilisimama kwa miguu yangu, na nikajidhihirisha kwa watu kwamba bnimezaliwa kwa Mungu.

24 Ndiyo, na tangu wakati huo hata hadi sasa, nimefanya kazi bila kukoma, kwamba nilete nafsi za watu kutubu; kwamba ningewaleta wapate akuonja shangwe kuu ambayo niliiona; ili nao pia wazaliwe ndani ya Mungu, na bwajazwe na Roho Mtakatifu.

25 Ndiyo, na sasa tazama, Ee mwana wangu, Bwana hunipa shangwe kuu kwa matokeo ya kazi yangu;

26 Kwani kwa sababu ya aneno ambalo amenipatia, tazama, wengi wamezaliwa kwa Mungu, na wameonja vile nilivyoonja, na wameona macho kwa macho kama vile nilivyoona; kwa hivyo wanajua kuhusu vitu hivi ambavyo nimezungumzia, vile ninavyojua; na elimu ambayo ninayo ni ya Mungu.

27 Na nimesaidiwa wakati wa majaribio na taabu za kila aina, ndiyo, na kwa kila aina ya mateso; ndiyo, Mungu amenikomboa kutoka gerezani, na kutoka kufungwa, na kutoka kifo; ndiyo, na ninaweka tumaini langu ndani yake, na aatanikomboa.

28 Na ninajua kwamba aataniinua katika siku ya mwisho, kuishi na yeye kwenye butukufu; ndiyo, na nitamsifu milele, kwani camewaleta babu zetu kutoka ya Misri, na amewameza dWamisri ndani ya Bahari ya Shamu; na aliwaongoza na uwezo wake hadi kwenye nchi ya ahadi; ndiyo, na amewakomboa kutoka kifungoni na utumwa mara kwa mara.

29 Ndiyo, na amewaleta babu zetu kutoka nchi ya Yerusalemu; na pia kwa uwezo wake usio na mwisho, aamewakomboa kutoka kifungoni na utumwa wao, mara kwa mara hadi wakati huu; na daima nimehifadhi ukumbusho wa utumwa wao; ndiyo, na ninyi pia inawapasa kuhifadhi ukumbusho wa utumwa wao, kama vile nilivyofanya.

30 Lakini tazama, mwana wangu, hii si yote; kwani unapaswa kujua kama vile ninavyojua kwamba akadiri utakavyoshika amri za Mungu utafanikiwa nchini; na unapaswa kujua pia kwamba, kadiri utakavyoacha kutii amri za Mungu utatolewa kwenye uwepo wake. Sasa hii ni kulingana na neno lake.