Kuwaimarisha Waumini Wapya
Pokea Kibali cha Hekaluni kwa ajili ya Ubatizo kwa Niaba ya Wafu na Uthibitisho


“Pokea Kibali cha Hekaluni kwa ajili ya Ubatizo kwa Niaba ya Wafu na Uthibitisho,” Njia Yangu ya Agano (2020)

“Pokea Kibali cha Hekaluni kwa ajili ya Ubatizo kwa Niaba ya Wafu na Uthibitisho,” Njia Yangu ya Agano

Picha
msichana na mvulana wakiangalia kadi za mahekalu

Pokea Kibali cha Hekaluni kwa ajili ya Ubatizo kwa Niaba ya Wafu na Uthibitisho

Ndani ya hekalu, unaweza kuwasaidia mababu zako kupokea baraka za injili ya Yesu Kristo kwa kubatizwa kwa niaba yao. Ili kuingia hekaluni, utahitaji kibali cha hekaluni, ambacho kinaweza kupatikana kwa kukutana na askofu.

  • Jifunze kuhusu umuhimu wa mahekalu na kuwa na kibali cha hekaluni. Fikiria kutumia:

  • Ongea na askofu au katibu wake mtendaji ili kupanga usaili kwa ajili ya kupokea kibali chako cha hekaluni kwa ajili ya ubatizo kwa niaba ya wafu na kuthibitishwa. Katika usaili, utaulizwa maswali sawa na yale uliyoulizwa kabla ya kubatizwa kwako. Hata kama huishi jirani na lilipo hekalu, kuwa na kibali kunaweza kukusaidia wewe kujiandaa kwa ajili ya wakati ambao utakwenda. Yafahamu maswali haya kutoka kwa Rais Russell M. Nelson (ona “Maneno ya Kuhitimisha,” Liahona, Nov. 2019, 121).

  • Ikiwezekana, panga tarehe ya kutembelea hekalu ili kufanya ubatizo kwa niaba ya mababu zako waliokufa.