“Jifunze kuhusu Ukuhani wa Haruni na Programu ya Wavulana,” Njia Yangu ya Agano (2020)
“Jifunze kuhusu Ukuhani wa Haruni na Programu ya Wavulana,” Njia Yangu ya Agano
Jifunze kuhusu Ukuhani wa Haruni na Programu ya Wavulana
Ukuhani ni nguvu na mamlaka ya Mungu yaliyotolewa kwa watumishi Wake duniani na hutumiwa kuwabariki watoto Wake, wote wanawake na wanaume. Wanaume wanaostahili wa umri wa miaka 11 na zaidi wanaweza kupokea Ukuhani wa Haruni ndani ya wiki moja baada ya kuthibitishwa. Wanapoendelea katika njia ya agano, wanaume wanaostahili wanaweza kupokea Ukuhani wa Melkizedeki.
-
Jifunze kuhusu mamlaka ya ukuhani na jinsi waumini wote wanavyobarikiwa na ukuhani. Ikiwa wewe ni mwanaume, zingatia sana maagano na majukumu yanayohusiana na Ukuhani wa Haruni na jinsi gani programu ya Wavulana inavyofanya kazi. Fikiria kutumia:
-
“What Does It Mean to Be Ordained to the Priesthood?” katika Families and Temples (kijitabu, 2016), 5–6.
-
“The Oath and Covenant of the Priesthood Is Relevant to Women,” Women and Priesthood Power (2021), ChurchofJesusChrist.org.
-
“Akidi za Ukuhani wa Haruni,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 10.1, ChurchofJesusChrist.org.
-
Urejesho wa Injili ya Yesu Kristo (kijitabu, 2008)
-
Introductory Guide for Children and Youth of The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints (2019), ikiwa kinapatikana.
-
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo kwa ajili ya Kufanya Chaguzi (2022).
-
-
Ikiwa wewe ni mwanaume na una umri wa miaka 11 au zaidi, zungumza na askofu au katibu wake mtendaji kuandaa usaili ili upokee Ukuhani wa Haruni.