Kuwaimarisha Waumini Wapya
Fanya Urafiki na Waumini wa Kata Yako


“Fanya Urafiki na Waumini wa Kata Yako,” Njia Yangu ya Agano (2020)

“Fanya Urafiki na Waumini wa Kata Yako,” Njia Yangu ya Agano

Picha
wanawake wakicheka pamoja

Fanya Urafiki na Waumini wa Kata Yako

Mtume Paulo alifundisha kwamba mnapojiunga na kusanyiko la Watakatifu, ninyi sio “wageni na wapitaji, lakini ni wenyeji” (Waefeso 2:19).

Kila kusanyiko la waumini wa Kanisa ni kama familia pana ambapo utapokea urafiki na msaada. Tenga muda wa kufanya urafiki na baadhi ya waumini wengine!

  • Ikiwa una simu ya mkononi, pakua aplikesheni ya Member Tools. Kama unatumia kifaa cha Android, unaweza kupakua aplikesheni kutoka Google Play store. Kama unatumia kifaa cha iOS, unaweza kupakua aplikesheni kutoka Apple App store. Baada ya kupakua Member Tools, ingia kwa kutumia akaunti yako ya Kanisa. Katika aplikesheni hii, unaweza kutafuta taarifa za mawasiliano za watu wa kata yako.

  • Kutoka kwenye Member Tools, angalia akaunti yako, sasisha taarifa zako za mawasiliano, na ongeza picha yako mwenyewe. Hakikisha unarejelea na kusasisha yaliyomo katika Maendeleo ya Njia Yangu ya Agano.

  • Fahamiana vyema na viongozi wako (askofu, rais wa akidi ya wazee, rais wa Muungano wa Usaidizi, rais wa Msingi, na viongozi wa akidi za Ukuhani wa Haruni na viongozi wa Wasichana) na washiriki wa darasa lako au akidi. Ongea nao juu ya shughuli zijazo, masomo ya baadaye na fursa za kuhudumu.