Misaada ya Kujifunza
TJS, Mathayo 7


TJS, Mathayo 7:1–2. Linganisha na Mathayo 7:1–2

Msihukumu bila haki.

1 Sasa haya ni maneno ambayo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake ili wawaambie watu.

2 Msihukumu pasipo haki, ili msihukumiwe; lakini hukumu ni kwa hukumu ya haki.

TJS, Mathayo 7:4–8. Linganisha na Mathayo 7:3–5

Yesu anafundisha wanafunzi wake kuwakabili waandishi, Mafarisayo, makuhani, na Walawi kwa sababu ya unafiki wao.

4 Na tena, mtawaambia, Na mbona mwakitazama kibanzi ambacho kiko ndani ya jicho la ndugu yako, lakini hufikirii boriti lililopo kwenye jicho lako?

5 Au utasemaje kwa ndugu yako, Acha nitoe kibanzi ndani ya jicho lako; na kumbe huweza kutoa boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?

6 Na Yesu akawaambia wanafunzi wake, Jee, mmewaona waandishi, na Mafarisayo, na makuhani, na Walawi? Wanafundisha katika masinagogi yao, lakini hawafuati sheria, wala amri; na wamepotea, na wapo chini ya dhambi.

7 Enendeni mkawaambie, Kwa nini mnawafundisha watu sheria na amri, wakati ninyi wenyewe ni wana wa ufisadi?

8 Waambie, Nyie wanafiki, litoe kwanza lile boriti katika jicho lako; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

TJS, Mathayo 7:9–11. Linganisha na Mathayo 7:6

Yesu anawafundisha wanafunzi wake kuhubiri toba na siyo kutoa siri za ufalme kwa walimwengu.

9 Enendeni ulimwenguni, mkiwaambia wote, Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

10 Na siri za ufalme mtaziweka ndani yenu wenyewe; maana si vyema kuwapa mbwa kile kilicho kitakatifu; wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao.

11 Kwa maana ulimwengu hauwezi kupokea kile ambacho ninyi wenyewe hamwezi kukichukua; kwa hiyo msizitoe lulu zenu kwao, wasije wakawageuka tena na kuwararua.

TJS, Mathayo 7:12–17. Linganisha na Mathayo 7:7–8

Yesu anawafundisha wanafunzi wake kwamba Baba hutoa maono kwa wote wanao omba.

12 Waambie, Mwombeni Mungu; ombeni, na mptapewa; tafuteni na mtapata, bisheni, na mtafunguliwa.

13 Kwani kila mmoja ambaye huuliza, hupata; na yule anayetafuta, huvumbua; na yule ambaye hubisha hufunguliwa.

14 Na ndipo wanafunzi wake wakamwambia, Watatuambia, Sisi wenyewe ni wenye haki, hatuhitaji mtu yeyote kutufundisha. Mungu, tunajua, alimsikiliza Musa na baadhi ya manabii; lakini sisi hatatusikiliza.

15 Na watasema, Tuna sheria kwa ajili ya wokovu wetu, na hiyo inatutosha.

16 Kisha Yesu alijibu, na kusema kwa wanafunzi wake, Na hivi ndivyo mtakavyowaambia.

17 Nani miongoni mwenu, mwenye mwana, akiwa amesimama nje, na aseme Baba, fungua nyumba yako ili niweze kuingia na kula pamoja nawe, ambaye hatasema, Karibu, mwanangu; kilicho changu ni chako, na chako changu?