Misaada ya Kujifunza
TJS, Marko 9


TJS, Marko 9:3. Linganisha na Marko 9:4

Yohana Mbatizaji akiwa katika Mlima wa Kugeuka Sura.

3 Na pale wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, au katika maneno mengine, Yohana Mbatizaji na Musa; nao walikuwa wakiongea pamoja na Yesu.

TJS, Marko 9:40–48. Linganisha na Marko 9:43–48

Yesu analinganisha kuukata mkono au mguu unaokukosesha ili kuvunja uhusiano ambao unaweza kumpotosha mtu.

40 Kwa hiyo, kama mkono wako ukikukosesha, ukate; au kama nduguyo akikukosesha na hatubu wala kuacha, atakatiliwa mbali. Ni heri kwako wewe kuingia katika uzima ukiwa kilema, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanamu.

41 Maana ni heri kwako kuingia katika uzima bila ndugu yako, kuliko wewe na ndugu yako mkatupwa jehanamu; katika moto ambao kamwe hautazimika, ambamo mafunza wake hawafi, na moto hauzimiki.

42 Na tena, kama mguu wako ukikukosesha, ukate; maana yeye ambaye ni mfano wako, ambao unaenenda, kama atakuwa mvunja sheria, atakatiliwa mbali.

43 Ni heri kwako, kuingia katika uzima u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili na kutupwa jehanamu; katika moto ambao kamwe hautazimika.

44 Kwa hiyo, acha kila mtu asimame au aanguke, mwenyewe, na siyo kwa sababu ya mwingine; au mtu asimtumainie mwingine.

45 Ombeni kwa Baba yangu, na itafanyika saa ile ile kile mwombacho, kama mkiomba kwa imani, mkiamini kuwa mtapata.

46 Na ikiwa jicho lako ambalo huona kwa ajili yako, yule ambaye ameteuliwa kukuongoza kukuonyesha nuru, akiwa mvunja sheria na akakukosesha, mngʼoe.

47 Ni heri kwako kuingia katika ufalme wa Mungu, ukiwa na jicho moja, kuliko na macho mawili na ukatupwa katika moto wa jehanamu.

48 Maana ni heri kwamba wewe mwenyewe uokolewe, kuliko kutupwa katika jehanamu pamoja na ndugu yako, ambamo funza wake hawafi, na ambamo moto wake hauzimiki.