Misaada ya Kujifunza
TJS, Marko 7


TJS, Marko 7:10–12. Linganisha na Marko 7:10

Yesu awalaani wale wanao wakataa manabii na hawatii sheria ya Musa.

10 Imeandikwa vizuri na kwa ukamilifu kwa ajili yenu, na manabii ambao mmewakataa.

11 Walishuhudia vitu hivi vya kweli, na damu yao itakuwa juu yenu.

12 Hamkuzitii ibada za Mungu; kwani Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako; na yeyote anaye mlaani baba au mama, mwache afe kifo cha mhalifu, kama ilivyoandikwa katika sheria yenu; lakini hamtii sheria.