Misaada ya Kujifunza
TJS, Marko 8


TJS, Marko 8:37–38. Linganisha na Marko 8:35

Yeyote aliye tayari kufa kwa ajili ya Yesu atapokea wokovu.

37 Kwa yeyote yule atakayeokoa maisha yake, atayapoteza; au yeyote yule atakaye okoa maisha yake, atakuwa tayari kuyatoa kwa ajili yangu; na kama hayupo tayari kuyatoa kwa ajili yangu, atayapoteza.

38 Lakini yeyote yule atakayekuwa tayari kuyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, na injili, huyo atayaokoa.

JST, Marko 8:42–43. Linganisha na Marko 8:38

Watu wanaomwonea aibu Kristo hawana nafasi katika ufufuo wa kwanza, bali hao walio tayari kufa kwa ajili ya Kristo watakuja pamoja naye katika utukufu wake.

42 Na hawatakuwa na nafasi katika ufufuo ule wakati atakapokuja.

43 Kwa kweli nawaambieni, Kwamba atakuja; na yule atakaye toa maisha yake kwa ajili yake na ya injili, atakuja pamoja naye, na atavikwa na utukufu wake katika wingu, kwenye mkono wa kuume wa Mwana wa Mtu.