Maandiko Matakatifu
Yakobo (KM) 5


Mlango wa 5

Yakobo anamdondoa Zeno kuhusu fumbo la miti ya mizabibu ya kiasili na iliyofugwa—Ni mfano wa Israeli na Wayunani—Kutawanywa na kusanyiko la Israeli kunawaziwa mbele—Wanefi na Walamani na nyumba ya Israeli yote wanatajwa kijuujuu—Wayunani watapandikizwa katika Israeli—Hatimaye shamba la mizabibu litachomwa. Karibia mwaka 544–421 K.K.

1 Tazameni, ndugu zangu, hamkumbuki mliposoma maneno ya nabii aZeno, ambayo alizungumzia nyumba ya Israeli, akisema.

2 Sikilizeni, Ee ninyi nyumba ya Israeli, na msikie maneno yangu, nabii wa Bwana.

3 Kwani tazama, hivyo ndivyo asemavyo Bwana, nitakulinganisha, Ee nyumba ya aIsraeli, na bmzeituni uliochukuliwa na mtu na akaulisha cshambani mwake la mizabibu; na ukakua, na kuzeeka, na ukaanza dkuoza.

4 Na ikawa kwamba bwana wa shamba la mizabibu akaenda mbele, na akaona kwamba mzeituni wake ulianza kuoza; na akasema: Nitaupogoa, na kuupalilia, na kuulisha, ili pengine uchipuke matawi yaliyo mazuri, na usiangamie.

5 Na ikawa kwamba aliupogoa, na kuupalilia, na kuulisha kulingana na neno lake.

6 Na ikawa kwamba baada ya siku nyingi ukaanza kutoa matawi machache, machanga na yaliyo nyororo; lakini tazama, kilele chake kikaanza kuangamia.

7 Na ikawa kwamba mwenye shamba la mizabibu akaliona, na akamwambia mtumishi wake: inanihuzunisha kwamba nitaupoteza mti huu; kwa hivyo, nenda ukate matawi kutoka amchekele, na uyalete hapa kwangu; na tutayagoboa yale matawi yake ya kati ambayo yameanza kukauka, na tutayatia motoni ili yachomeke.

8 Na tazama, asema Bwana wa shamba la mizabibu, ninaondoa matawi haya mengi yaliyo machanga na miororo, na nitayapandikiza popote ninapotaka; na haidhuru kama mzizi wa mti huu utaangamia, Nitajihifadhia matunda yake; kwa hivyo, nitachukua matawi haya machanga na miororo, na nitayapandikiza popote nitakapo.

9 Chukua ewe matawi mchekele, na uyapandikize, abadala yake; na haya ambayo nimeyagoboa nitayatupa motoni na kuyachoma, ili yasikwaze mchanga wa shamba langu la mizabibu.

10 Na ikawa kwamba mtumishi wa Bwana wa shamba la mizabibu alitenda kulingana na neno la Bwana wa shamba, na akapandikiza matawi amchekele.

11 Na Bwana wa shamba la mizabibu akasababisha kwamba ipaliliwe, na ipogolewe, na ilishwe, akimwambia mtumishi wake: Inanihuzunisha kwamba nitaupoteza mti huu; kwa hivyo, ili pengine nihifadhi mizizi yake ili isiangamie, na ili nijihifadhie, nimetenda kitu hiki.

12 Kwa hivyo, fuata njia yako; chunga mti, na uulishe, kulingana na maneno yangu.

13 Na haya anitayaweka katika sehemu ya mbali shambani mwangu la mizabibu, mahali popote nitakapo, na haikuhusu wewe; na ninaitenda ili nijihifadhie matawi ya asili ya ule mti; na pia, kwamba nijiwekee, akiba ya matunda wakati wa majira; kwani inanihuzunisha kwamba nitapotelewa na mti huu na matunda yake.

14 Na ikawa kwamba Bwana wa shamba la mizabibu akaenda njia zake, na akaficha matawi ya kiasili ya ule mzeituni sehemu za mbali za shamba la mizabibu, mingine hapa na mingine pale, kulingana na nia yake na raha yake.

15 Na ikawa kwamba muda mrefu ukapita, na Bwana wa shamba la mizabibu akamwambia mtumishi wake: Njoo, hebu twende shambani la mizabibu, ili tufanye kazi shambani la mizabibu.

16 Na ikawa kwamba Bwana wa shamba la mizabibu, na pia yule mtumishi, walienda shambani la mizabibu kufanya kazi. Na ikawa kwamba yule mtumishi akamwambia bwana wake: Tazama, angalia hapa; tazama ule mti.

17 Na ikawa kwamba Bwana wa shamba la mizabibu aliangalia na kuona ule mti ambao yale matawi ya mchekele yalikuwa yamepandikizwa; na ulikuwa umeanza kuota na kuanza kuzaa amatunda. Na akaona kwamba ni mazuri; na matunda yake yalikuwa kama matunda ya kawaida.

18 Na akamwambia yule mtumishi: Tazama, matawi ya ule mti wa mwituni yametoa umande kutoka mzizi wake, kwamba mzizi wake umeleta nguvu nyingi; na kwa sababu ya nguvu hizo nyingi za mzizi yale matawi ya mwituni yamezaa matunda ya kinyumbani. Sasa, kama hatungepandikiza haya matawi, ule mti ungeangamia. Na sasa, tazama, nitaweka matunda mengi, ambayo yamezaliwa na ule mti; na matunda yake nitajiwekea akiba, kwa wakati wa majira.

19 Na ikawa kwamba Bwana wa shamba la mizabibu akamwambia mtumishi: Njoo, twende katika sehemu za mbali za shamba, na tutazame kama matawi ya mti hayajazaa matunda mengi pia, ili nijiwekee akiba, mimi mwenyewe.

20 Na ikawa kwamba walienda pale pahali ambapo yule bwana alikuwa ameficha matawi ya ule mti wa kawaida, na akamwambia yule mtumishi: Tazama haya; na akaona ule wa akwanza kwamba ulikuwa umezaa matunda mengi; na akaona pia kwamba yalikuwa mazuri. Na akamwambia yule mtumishi: Chukua matunda yake, na uyaweke kama akiba wakati wa majira, ili nijihifadhie, kwani tazama, akasema, nimeulisha kwa muda huu wote, na umezaa matunda mengi.

21 Na ikawa kwamba yule mtumishi akamwambia bwana wake: Kwa nini ulikuja kupanda mti huu hapa, au tawi la mti huu? Kwani tazama, palikuwa ndipo pahali pabovu katika shamba lako la mizabibu.

22 Na Bwana wa shamba la mizabibu akamwambia: Usinipatie mawaidha; nilijua kwamba palikuwa ni pahali pabovu shambani; ndivyo, nikakwambia, nimeulisha huu muda mrefu, na wewe unaona kwamba umezaa matunda mengi.

23 Na ikawa kwamba Bwana wa shamba la mizabibu akamwambia mtumishi wake: Tazama hapa; tazama nimepanda tawi lingine la mti pia; na wewe unajua kwamba pahali hapa ni pabovu zaidi ya pale pa mwanzo. Lakini, tazama mti. Nimeulisha kwa muda huu mrefu, na umezaa matunda mengi; kwa hivyo, uyavune, na uyaweke kama hazina wakati wa majira, ili nijiihifadhie mimi mwenyewe.

24 Na ikawa kwamba yule Bwana wa shamba la mizabibu akamwambia tena mtumishi wake: Tazama hapa; na uone atawi lingine, ambalo pia nimelipanda; tazama nimelilisha pia, na limezaa matunda.

25 Na akamwambia mtumishi: Tazama hapa na uone la mwisho. Tazama, nimepanda hili pahali apema pa shamba; na nimelilisha kwa muda huu mrefu, na sehemu moja pekee ya mti imezaa matunda ya kinyumbani, na sehemu bingine ya mti imezaa matunda ya mwituni; tazama, nimeulisha mti huu kama yale mengine.

26 Na ikawa kwamba Bwana wa shamba la mizabibu akamwambia mtumishi wake: Chuma yale matawi ambayo hayajazaa amatunda mema, na uyatupe motoni.

27 Lakini tazama, yule mtumishi akamwambia: Hebu tuupogoe, na tuupalilie, na tuulishe kwa muda mwingine mrefu kidogo tena, kwamba pengine utakuzalia matunda mema, yale ambayo unaweza kujiwekea akiba wakati wa majira.

28 Na ikawa kwamba yule Bwana wa shamba la mizabibu na mtumishi wa Bwana wa shamba walilisha matunda yote ya shamba la mizabibu.

29 Na ikawa kwamba muda mrefu ulipita, na Bwana wa shamba akamwambia amtumishi wake: Njoo, twende kule shambani la mizabibu, ili tufanye kazi tena shambani la mizabibu. Kwani tazama, bwakati unakaribia, na cmwisho unafika hivi karibuni; kwa hivyo, lazima nijiwekee akiba, wakati wa majira.

30 Na ikawa kwamba Bwana wa shamba la mizabibu na mtumishi wake walienda shambani; na wakafika kwenye ule mti ambao matawi yake ya kawaida yalivunjwa, na matawi ya mwituni kupandikizwa; na tazama matunda ya kila aaina yaliufunika ule mti.

31 Na ikawa kwamba yule Bwana wa shamba la mizabibu alionja yale matunda, kila aina kulingana na wingi wake: Na yule Bwana wa shamba la mizabibu akasema: Tazama, kwa muda huu mrefu tumeulisha mti huu, na nimejiwekea akiba kwa wakati wa majira.

32 Lakini tazama, wakati huu umezaa matunda mengi, na ahakuna yoyote ambayo ni mazuri. Na tazama, kuna kila aina ya matunda mabaya; na hainifaidi chochote, ingawa tumeuchokea sana; na sasa inanihuzunisha kwamba nitapoteza mti huu.

33 Na Bwana wa shamba la mizabibu akamwambia yule mtumishi: Tutaufanya nini mti huu, ili nijihifadhie mimi mwenyewe matunda mazuri?

34 Na yule mtumishi akamwambia bwana wake: Tazama, kwa sababu wewe ulipandikiza matawi ya mchekele, yamelisha mizizi, hata iwe hai na isiangamie; kwa hivyo wewe unaona kwamba bado ni mizuri.

35 Na ikawa kwamba Bwana wa lile shamba la mizabibu akamwambia mtumishi wake: Huu mti haunifaidi chochote, na mizizi yake hainifaidi chochote ikiwa utazaa matunda maovu.

36 Walakini, najua kwamba mizizi yake ni mizuri, na kwa shauri langu nimeihifadhi; na kwa sababu ya nguvu yao imezaa, kutoka kwa matawi ya mwituni, matunda mazuri.

37 Lakini tazama, yale matawi ya mwituni yamekua azaidi ya mizizi yake; na kwa sababu matawi ya mwituni yamezidi mizizi yake umezaa matunda mengi maovu; na kwa sababu umezaa matunda mengi maovu wewe unaona kwamba umeanza kuangamia; na utaoza hivi karibuni, na kutupwa motoni, tusipotenda jambo ili kuuhifadhi.

38 Na ikawa kwamba Bwana wa shamba akamwambia mtumishi wake: Twende kule sehemu za ndani ya shamba la mizabibu, na tuone kama matawi ya kawaida pia nayo yamezaa matunda maovu.

39 Na ikawa kwamba walienda katika sehemu za ndani za lile shamba. Na ikawa kwamba waliona kuwa yale matunda ya matawi ya kiasili pia nayo yalikuwa yameharibika; ndiyo ya akwanza na ya pili na ya mwisho pia; na yote yalikuwa yameharibika.

40 Na matunda ya amwituni ya ule wa mwisho yalizidi sehemu ile ya mti ambayo ilizaa matunda mema, hata kwamba lile tawi likanyauka na kuangamia.

41 Na ikawa kwamba yule Bwana wa shamba la mizabibu alilia, na akamwambia mtumishi wake: Je, ningefanya anini zaidi kuhusu shamba langu la mizabibu?

42 Tazama, nilijua kwamba matunda yote ya lile shamba la mizabibu, isipokuwa haya, yalikuwa yameharibika. Na sasa hii ambayo hapo awali ilizaa matunda mema pia imeharibika; na sasa miti yote ya shamba langu la mizabibu hainifaidi chochote ila kukatwa na kutiwa motoni.

43 Na tazama huu wa mwisho, ambao tawi lake limekauka, nilikuwa nimeupanda katika sehemu anzuri; ndiyo, hata ile ambayo ilikuwa ni bora zaidi ya sehemu zingine za shamba langu la mizabibu.

44 Na wewe uliona pia kwamba nilikata ile ailiyofunika sehemu hii, ili nipande mti huu pahala pake.

45 Na wewe uliona kwamba sehemu moja ilizaa matunda mema, na sehemu ingine ikazaa matunda ya mwituni; na kwa sababu sikungʼoa matawi yake na kuyatupa motoni, tazama, yamelemea tawi lile njema hata kwamba likakauka.

46 Na sasa, tazama, ingawa tulilitunza sana shamba langu la mizabibu, miti yake imeharibika, hata kwamba haizai matunda mema; na nilikuwa nimetarajia kuihifadhi, na kujiwekea hazina, wakati wa majira. Lakini, tazama, imekuwa kama ule mchekele, na haina faida ila tu akukatwa na kutupwa motoni; na inanihuzunisha kwamba nitaipoteza.

47 Lakini ningefanya nini zaidi shambani langu la mizabibu? Je nimelegeza mkono wangu, hata kwamba sikuulisha? Hapana, nimeulisha, na kuupalilia, na kuupogoa, na nimeutia mbolea; na animeunyosha mkono wangu karibu siku yote, na bmwisho unakaribia. Na inanihuzunisha kwamba nitakata miti yote ya shamba langu la mizabibu, na kuitupa motoni ili ichomeke. Ni nani aliyeharibu shamba langu la mizabibu?

48 Na ikawa kwamba yule mtumishi akamwambia bwana wake: Je, sio kiburi cha shamba lako la mizabibu—kwamba matawi yake yamezidi mizizi ambayo ni mizuri? Na kwa sababu yale matawi yamezidi mizizi yake, tazama yalikua zaidi ya nguvu ya mizizi, na kujichukulia nguvu. Tazama, nasema, je, si hii ndiyo sababu ya uharibifu wa miti ya shamba lako?

49 Na ikawa kwamba Bwana wa shamba la mizabibu akamwambia mtumishi wake: Hebu twende na tukate miti ile ya shamba la mizabibu na tuitupe motoni, ili isifunike ardhi ya shamba langu, kwani nimeshatenda yote. Je, ni yapi mengine ningeutendea shamba langu la mizabibu?

50 Lakini, tazama, yule mtumishi akamwambia Bwana wa shamba la mizabibu: Liache kwa amuda mdogo zaidi.

51 Na Bwana akasema: Ndiyo, nitaliacha kwa muda mdogo zaidi, kwani inanihuzunisha kwamba nitapoteza miti ya shamba langu la mizabibu.

52 Kwa hivyo, hebu tukate amatawi mengine ya hii ambayo nimepanda katika sehemu za ndani za shamba langu la mizabibu, na hebu tuyapandikize katika ule mti ambao yalitolewa; na hebu tungʼoe matawi kutoka ule mti ambao matunda yake ni machungu zaidi, na badala yake tupandikize matawi ya kawaida.

53 Na nitatenda haya ili ule mti usiangamie, ili, pengine, nijihifadhie mizizi yake kwa matumizi yangu.

54 Na, tazama, mizizi ya yale matawi ya mti ambao nimeupanda popote nipendapo bado ingali hai; kwa hivyo, ili nijihifadhie hayo pia kwa matumizi yangu mwenyewe, nitaondoa matawi ya mti huu, na anitayapandikiza ndani yake. Ndiyo, nitayapandikiza katika matawi ya mti mzazi wao, ili nijihifadhie pia hiyo mizizi, ili itakapopokea nguvu za kutosha pengine itanizalia matunda mema, na ili bado nitukuzwe na matunda ya shamba langu la mizabibu.

55 Na ikawa kwamba walichukua kutoka mti wa kawaida ambao ulikuwa umegeuka kuwa wa mwituni, na kupandikiza katika miti ya kawaida, ambayo pia ilikuwa imegeuka kuwa ya mwituni.

56 Na pia wakachukua kutoka miti ya kawaida ambayo ilikuwa imegeuka kuwa ya mwituni, na kupandikiza katika ule mti mzazi wao.

57 Na Bwana wa shamba la mizabibu akamwambia mtumishi wake: Usingʼoe yale matawi ya mwituni kutoka ile miti, ila tu yale ambayo ni machungu zaidi; na utapandikiza ndani yao kulingana na yale ambayo nimesema.

58 Na tutalisha tena ile miti ya shamba la mizabibu, na tutachenga matawi yake; na tutangʼoa kutoka hiyo miti yale matawi yaliyooza, ambayo lazima yaangamie, na kuyatupa motoni.

59 Na nitatenda haya ili, pengine, mizizi yake ipokee nguvu kwa sababu ya ubora wao; na kwa sababu ya mabadiliko ya matawi, kwamba wema uzidi ubaya.

60 Na kwa sababu ya kwamba nimehifadhi yale matawi ya kawaida na mizizi yake, na ya kwamba nimepandikiza matawi ya kawaida tena katika ule mti mzazi wao, na nimehifadhi mizizi ya ule mti mzazi wao, ili, pengine, miti ya shamba langu la mizabibu izae tena amatunda mema; na ili nishangilie tena kwa matunda ya shamba langu la mizabibu, na, ili, nishangilie zaidi ya kwamba nimehifadhi mizizi na matawi ya malimbuko—

61 Kwa hivyo, nenda, ulete awatumishi, ili tufanye bkazi shambani la mizabibu kwa bidii na kwa nguvu zetu, ili tuitayarishe njia, ili nirejeshe tena lile tunda la kawaida, tunda la kawaida ambalo ni bora zaidi ya matunda mengine yote.

62 Kwa hivyo, hebu twende na tutumike kwa nguvu zetu mara hii ya mwisho, kwani tazama mwisho unakaribia, na hii ndiyo mara ya mwisho ambayo nitapogoa shamba langu la mizabibu.

63 Pandikizeni matawi; anzeni na ya amwisho ili yawe ya kwanza, na kwamba ya kwanza yawe ya mwisho, na mlime miongoni mwa miti, iliyo mchanga na iliyokomaa, ya kwanza na ya mwisho; na ya mwisho na ya kwanza, ili yote ilishwe tena kwa mara ya mwisho.

64 Kwa hivyo, chimbeni miongoni mwao, na muipogoe, na kuitia mbolea mara nyingine, kwa mara ya mwisho, kwani mwisho unakaribia. Na kama haya mapandikizo ya mwisho yatakua, na kuzaa matunda ya kawaida, basi mtayatayarishia njia, ili yakue.

65 Na itakapoanza kukua mtaondoa matawi yanayozaa matunda machungu, kulingana na nguvu na kipimo cha uzuri wake; na ahamtaondoa yaliyo mabaya kwa ghafla, isiwe kwamba mizizi yake inazidi nguvu ya lile pandikizo, na pandikizo hilo liangamie, na nipoteze miti ya shamba langu la mizabibu.

66 Kwani inanihuzunisha kwamba nitapoteza miti ya shamba langu la mizabibu; kwa hivyo mtafyeka iliyo miovu kulingana na vile iliyo mizuri itakavyomea, ili mizizi na kilele ziwe na nguvu sawa, hadi iliyo nzuri izidi iliyo mbovu, na iliyo mbovu ikatwe na kutiwa motoni, ili isifunike ardhi ya shamba langu; na hivyo ndivyo nitaufagia uovu kutoka shamba langu.

67 Na matawi ya mti wa kawaida nitayapandikiza tena kwenye mti ule wa kawaida;

68 Na matawi ya mti wa kawaida nitayapandikiza katika matawi ya kawaida ya ule mti; na ndivyo nitakavyoiunganisha pamoja tena, ili izae matunda ya kawaida, na iwe kitu kimoja.

69 Na iliyo mbovu aitatupwa mbali, ndiyo, hata kutoka ardhi yote ya shamba langu la mizabibu; kwani tazama, ni kwa hii mara moja tu nitakayopogoa shamba langu la mizabibu.

70 Na ikawa kwamba Bwana wa shamba la mizabibu alimtuma amtumishi wake; na mtumishi akaenda na kutenda kulingana na vile alivyoamriwa na Bwana, na akaleta watumishi wengine; na walikuwa bwachache.

71 Na Bwana wa shamba la mizabibu akawaambia: Nendeni, na amkatumikie shamba la mizabibu, kwa uwezo wenu. Kwani tazama, hii ndiyo bmara ya mwisho nitakayolisha shamba langu la mizabibu; kwani mwisho unakaribia, na wakati unafika kwa haraka; na kama mtanitumikia na mimi kwa nguvu zenu cmtakuwa na shangwe katika matunda nitakayojiwekea kwa wakati unaokaribia.

72 Na ikawa kwamba watumishi walienda na kutumikia kwa nguvu zao; na Bwana wa shamba la mizabibu akatumikia shambani pia nao; na wakatii amri za Bwana wa shamba la mizabibu katika vitu vyote.

73 Na matunda ya kawaida yakaanza kukua tena pale shambani la mizabibu; na matawi ya kawaida yakaanza kukua na kufanikiwa sana; na matawi ya mwituni yakapobolewa na kutupwa mbali; na wakaweka mizizi yake na kilele chake kuwa sawa, kulingana na nguvu zake.

74 Na wakatumikia hivyo, kwa bidii zote, kulingana na amri za Bwana wa shamba la mizabibu, hadi iliyo mibovu ikatolewa shambani la mizabibu, na Bwana alikuwa amejihifadhia kwamba ile miti ilikuwa matunda ya kawaida tena; na ikawa kama akitu kimoja; na matunda yalikuwa sawa; na yule Bwana wa shamba la mizabibu alikuwa amejihifadhia mwenyewe matunda ya kawaida, ambayo yalikuwa bora zaidi tangu hapo mwanzoni.

75 Na ikawa kwamba wakati yule Bwana wa shamba la mizabibu alipoona kuwa matunda yake ni mazuri, na kwamba shamba lake la mizabibu halikuwa haribifu tena, aliwaita watumishi wake, na kuwaambia: Tazama, tumelilisha shamba langu la mizabibu kwa mara hii ya mwisho; na ninyi mmeona kwamba nimetenda kulingana na nia yangu; na nimehifadhi matunda ya kawaida, na ni mazuri, kama vile yalivyokuwa hapo mwanzoni. Na aheri ninyi; kwani kwa sababu mmekuwa na bidii katika kutumikia na mimi katika shamba langu la mizabibu, na mmetii amri zangu, na kuniletea tena matunda ya bkawaida, kwamba shamba langu sio bovu tena, na iliyo mibovu imetupwa mbali, tazama mtapokea shangwe na mimi kwa sababu ya matunda ya shamba langu la mizabibu.

76 Kwani tazama, kwa muda amrefu nitajiwekea matunda ya shamba langu la mizabibu kwa wakati wa majira, unaokaribia kwa haraka; na nimelisha shamba langu la mizabibu kwa mara ya mwisho, na kulipogoa, na kulilimia, na kulitia mbolea; kwa hivyo nitajiwekea matunda, kwa muda mrefu, kulingana na yale ambayo nimezungumza.

77 Na wakati ule utakapofika ambao matunda maovu yatakuja tena katika shamba langu la mizabibu, basi nitasababisha yale yaliyo mazuri na mabaya kukusanywa; na yale mazuri nitajiwekea, na yale mabaya nitayatupa mahali pake. Na kisha wakati wa amajira utafika na mwisho; na nitasababisha shamba langu la mizabibu blichomwe kwa moto.