Maandiko
Etheri 4
iliyopita inayofuata

Mlango wa 4

Moroni anaamrishwa kuyafungia maandishi ya kaka wa Yaredi—Hayatafunuliwa mpaka watu wote watakapokuwa na imani kama ya kaka wa Yaredi—Kristo anaamuru watu wote waamini maneno Yake, na yale ya wanafunzi Wake—Watu wanaamriwa watubu, waamini injili, na waokolewe.

1 Na Bwana alimwamuru kaka wa Yaredi aende chini kutoka mlimani kutoka kwenye uwepo wa Bwana, na aaviandike vitu alivyokuwa ameviona; na vilikatazwa kuonekana na watoto wa watu bmpaka atakapoinuliwa juu ya msalaba; na kwa sababu hii mfalme Mosia alivificha, kwamba visijulikane duniani mpaka Kristo atakapojidhihirisha kwa watu wake.

2 Na baada ya Kristo kujidhihirisha kwa ukweli kwa watu wake aliamrisha kwamba vijulikane.

3 Na sasa, baada ya hayo, wote wamefifia katika kutoamini; na hakuna yeyote isipokuwa Walamani, na wamekataa injili ya Kristo; kwa hivyo nimeamriwa kwamba anivifiche tena ardhini.

4 Tazama, nimeandika juu ya mabamba haya vitu vivyo hivyo ambavyo kaka wa Yaredi aliviona; na hakujakuwa vitu vikubwa vilivyoonyeshwa kuliko hivyo ambavyo vilionyeshwa kwa kaka wa Yaredi.

5 Kwa hivyo Bwana ameniamuru niviandike; na nimeviandika. Na aliniamuru kwamba anivifunge; na pia ameniamuru kwamba nifungie btafsiri yake; kwa hivyo nimeifungia tafsiri, kulingana na amri ya Bwana.

6 Kwani Bwana aliniambia: Havitawaendea Wayunani mpaka siku watakapotubu uovu wao, na kuwa safi mbele ya Bwana.

7 Na katika siku hiyo watakapofanya imani kwangu, asema Bwana, hata kama kaka wa Yaredi alivyofanya, kwamba awatakaswe kupitia kwangu, ndipo nitawaonyesha vitu ambavyo kaka wa Yaredi aliviona, hata kwa kuwakunjulia ufunuo wangu wote, anasema Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, bBaba wa mbingu na wa dunia, na vitu vyote vilivyomo.

8 Na yule ambaye aatapingana na neno la Bwana, acha alaaniwe; na yule ambaye batakana vitu hivi, acha alaaniwe; kwani kwao, csitaonyesha vitu vikubwa zaidi, anasema Yesu Kristo; kwani ni mimi ninayezungumza.

9 Na kwa amri yangu mbingu hufunguliwa na akufungwa; na kwa neno langu bdunia itatetemeka; na kwa amri yangu wakazi wake watakufa, kama waliochomwa na moto.

10 Na yule ambaye haamini maneno yangu, haamini wanafunzi wangu; na ikiwa hivyo kwamba sisemi, hukumu wewe; kwani utajua kwamba ni mimi ninayezungumza, katika asiku ya mwisho.

11 Lakini yule aaaminiye maneno haya ambayo nimesema, yeye nitamtembelea na ufunuo wa Roho yangu, na atajua na kushuhudia. Kwani kwa sababu ya Roho yangu batafahamu kwamba vitu hivi ni vya ckweli; kwani huwashawishi watu kutenda mema.

12 Na kitu chochote ambacho hushawishi watu kutenda mema ni changu; kwani amema hayatoki kwa yeyote isipokuwa kwangu. Mimi ni yule yule ambaye huongoza watu kwa wema wote; yule ambaye bhataamini maneno yangu hataniamini—kwamba ni mimi; na yule ambaye hataniamini hatamwamini Baba ambaye alinituma. Kwani tazama, mimi ni Baba, mimi ni cmwangaza, na dmaisha, na ukweli wa dunia.

13 aNjooni kwangu, Ee ninyi Wayunani, na nitawaonyesha vitu vikuu zaidi, ufahamu ambao umefichwa kwa sababu ya kutoamini.

14 Njooni kwangu, Ee ninyi nyumba ya Israeli, na itafanywa akujulikana kwenu jinsi Baba alivyoweka vitu kwenu, kutokea msingi wa dunia; na haijawafikia, kwa sababu ya kutoamini.

15 Tazama, wakati mtakapopasua lile pazia la kutoamini ambalo linawasababisha kubaki katika hali yenu ya kutisha ya uovu, na ugumu wa moyo, na upofu wa akili, ndipo vitu vikubwa na vya kustaajabisha ambavyo avilifichwa kutokea mwanzo wa dunia kutoka kwenu—ndiyo, wakati mtakapomlingana Baba katika jina langu, na moyo uliopondeka na roho iliyovunjika, ndipo mtajua kwamba Baba amekumbuka agano ambalo alifanya na babu zenu, Ee nyumba ya Israeli.

16 Na ndipo aufunuo wangu ambao nimesababisha kuandikwa na mtumishi wangu Yohana utakunjuliwa machoni mwa watu wote. Kumbuka, wakati mtakapoona vitu hivi, mtajua kwamba wakati uko karibu kwamba vitafanywa kuwa wazi kabisa.

17 Kwa hivyo, amtakapopokea maandishi haya mjue kwamba kazi ya Baba imeanza juu ya uso wa nchi.

18 Kwa hivyo, atubuni enyi miisho ya dunia, na mje kwangu, na mwamini katika injili yangu, na bmbatizwe katika jina langu; kwani yule ambaye anaamini na kubatizwa atakombolewa; lakini yule ambaye haamini atalaaniwa; na cishara zitaonyeshwa kwa wale ambao wanaamini katika jina langu.

19 Na ana baraka yule atakayepatikana akiwa amwaminifu kwa jina langu katika siku ya mwisho, kwani atainuliwa kuishi katika ufalme uliotayarishwa bkutokea mwanzo wa dunia. Na tazama ni mimi ambaye nimezungumza. Amina.