Maandiko Matakatifu
3 Nefi 25


Mlango wa 25

Katika Ujio wa Pili, wenye kiburi na waovu watateketezwa kama makapi—Eliya atarejea kabla ya ile siku kubwa na ya kutisha—Linganisha Malaki 4. Karibia mwaka 34 B.K.

1 Kwani tazama, ile siku inakuja ambayo aitawaka kama tanuru; na wote wenye bkiburi, ndiyo, na wote wanaotenda maovu, watakuwa makapi; na ile siku inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa Majeshi, kwamba haitawaachia shina wala tawi.

2 Lakini kwenu mnaolicha jina langu, yule aMwana wa Haki atawashukia na uponyaji katika mabawa yake; na ninyi mtaenda mbele na bkukua kama cndama zizini.

3 Na amtakanyaga waovu; kwani watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu katika siku nitakayofanya hivi, asema Bwana wa Majeshi.

4 Kumbukeni ninyi sheria ya Musa, mtumishi wangu, niliyemwamuru huko aHorebu kwa ajili ya Waisraeli wote, na amri za hukumu.

5 Tazama, nitawatumia aEliya nabii kabla ya kuja kwa ile bsiku kubwa na ya kutisha ya Bwana.

6 Na aatageuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, nisije na kupiga dunia na laana.