2020
Imarisha Ushuhuda Wako Kupitia Ono la Kwanza
Aprili 2020


Imarisha Ushuhuda Wako Kupitia Ono la Kwanza

Ninaomba kwamba mtafuata mtindo wa Joseph wa kusali, mjifunze kweli alizojifunza, na muimarishe imani yenu katika Baba wa Mbinguni na Mwana Wake, Yesu Kristo.

Picha
Teenaged Elder Anderson shares his beliefs with friends Illustration of Elder Neil Anderson when he was 16 years old at a conference he traveled to the east coast to attend. He is in a informal group of people and he is explaining his beliefs to the group.

Wakati nilipokuwa na umri wa miaka 16, nilisafiri kutoka nyumbani kwetu Idaho kuhudhuria mkutano uliokuwa Pwani ya Mashariki ya Marekani, uliohudhuriwa na wavulana na wasichana kutoka majimbo yote 50 na mataifa takriban 40. Kabla ya hapo, ni mara chache nilikuwa katika hali ambapo imani na misimamo yangu vilinitofautisha.

Jioni moja katika mazingira yasiyo rasmi ya kikundi, mjadala ulitokea kuhusu baadhi ya imani na desturi za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kikundi kikubwa cha wanafunzi kilinigeukia na kuanza kuuliza maswali, baadhi ambayo yalikosoa imani yetu.

Hilo lilitokea ghafla. Lakini baada ya kutafakari kwa muda, nilianza kushiriki baadhi ya kanuni za msingi. Nilieleza kwamba tuna Baba wa Mbinguni, kwamba sisi ni wana na mabinti Zake, na kwamba tuko duniani kukuza imani katika Yesu Kristo na kujithibitisha kwa kuchagua wema dhidi ya uovu.

Kushiriki kanuni hizi kulinielekeza kwenye ushuhuda wa Joseph Smith. Wanafunzi wengine hawakuwa wameuliza kuhusu Joseph Smith, lakini nilijikuta nikielekea kwenye asili ya kwa nini niliamini kile nilichoamini. Nilipokuwa nikielezea juu ya kuonekana kwa Baba na Mwana katika Msitu Mtakatifu, ghafla kila mtu alinyamaza. Hisia takatifu ilipenya ndani ya chumba, na hisia kubwa ya nguvu za kiroho ilishuka juu yangu na juu ya maneno yangu.

Baadaye, wanafunzi kadhaa walinishukuru kwa ajili ya imani yangu thabiti. Baadhi hata walitaka maelezo zaidi kuhusu Kanisa. Nilipokuwa nikirudi chumbani kwangu usiku huo, niligundua kwamba mtu ambaye tukio hili lilikuwa na ushawishi mkubwa juu yake alikuwa mimi. Nilikuwa nimehisi mimi mwenyewe nguvu za kutoa ushuhuda wa Mungu Baba, Yesu Kristo, na Ono la Kwanza.

Tangu tukio hilo zaidi ya miaka 50 iliyopita, nimeshuhudia nyakati nyingi kuhusu Baba, Mwana, na Nabii Joseph Smith. Katika matukio haya, nimehisi siku zote ushahidi wa kuthibitisha wa Roho Mtakatifu.

Ningependa kushiriki kanuni tatu ambazo nimejifunza kutoka kwenye uelewa wangu wa kiroho wa Ono la Kwanza. Kanuni hizi zimeimarisha imani yangu katika na tamaa yangu kumfuata Baba yetu wa Mbinguni na Mwana Wake Mpendwa. Ninatumaini zitawaimarisha pia.

Picha
An illustration of the First Vision

1. Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu Ni Viumbe Tofauti

Kwa karne nyingi, wasomi wa kidini na wanafalsafa walikuwa wamefanya mdahalo wa asili ya Mungu Baba, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu. Wengi waliamini Walikuwa kiumbe mmoja. Kwa sababu ya tukio la Joseph katika Msitu Mtakatifu miaka 200 iliyopita, tunajua ukweli halisi kuhusu asili ya Mungu.

Kwanza kabisa, Yu Hai! Pili, Baba na Mwana ni viumbe wawili tofauti, watukufu, waliofufuka, wenye upekee. Baadaye, Joseph alifunza kwamba “Roho Mtakatifu hana mwili wa nyama na mifupa, bali ni mtu wa Kiroho. Kama isingekuwa hivyo, Roho Mtakatifu asingeweza kukaa ndani yetu” (Mafundisho na Maagano 130:22).

2. Sisi ni Wana na Mabinti za Mungu

Kupitia Ono la Kwanza na matukio mengine, nabii Joseph Smith alijifunza kwamba Mungu si nguvu kutoka mbali ambaye aliumba ulimwengu na wakazi wake na kisha kuwasahau. Kiuhalisia, kila moja wetu ni “binti mpendwa [au mwana] wa wazazi wa mbinguni.”1

Tangazo juu ya familia linasema: “Wanadamu wote—wanaume na wanawake—wameumbwa katika mfano wa Mungu. Kila mmoja ni mwana au binti mpendwa wa kiroho wa wazazi wa mbinguni, na, kama hivyo, kila mmoja ana asili takatifu na takdiri.”2 Baba yetu ametangaza wazi takdiri hiyo: “Hii ni kazi yangu na utukufu wangu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39).

Utambulisho wetu uko na Mungu, na tuko hapa duniani kuwa zaidi kama Yeye. Uelewa huu kutoka Ono la Kwanza uliniruhusu mimi kama mvulana kujua kwamba nilikuwa na Baba wa Mbinguni binafsi ambaye alinipenda na alinitaka nirudi Kwake.

3. Tunaweza Kusamehewa Dhambi Zetu

Mojawapo ya wasiwasi mkubwa wa Joseph ilikuwa msamaha wa dhambi zake. Katika simulizi moja ya Ono la Kwanza, Bwana alimwambia mtafutaji huyo mdogo wa ukweli: “Joseph, mwanangu, dhambi zako zimesamehewa. Enenda zako, enenda katika hukumu zangu, na ukazishike amri zangu. Tazama, mimi ni Bwana wa utukufu. Nilisulubiwa kwa ajili ya ulimwengu, ili wote watakaoliamini jina langu waweze kupata uzima wa milele.”3

Joseph alijifunza kwamba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, angeweza kusamehewa dhambi zake na kuwa msafi na bila doa mbele za Mungu. Alipewa ufahamu thabiti kwamba Yesu Kristo alijichukulia juu Yake dhambi na mizigo ya wale wote ambao waliwahi kuishi na watakaoishi duniani.

Kutokana na Ono la Kwanza, tunajifunza kwamba kwa sababu ya neema ya Mwokozi, Yesu Kristo, sisi pia tunaweza kusamehewa dhambi zetu na siku moja kusimama tukiwa wasafi mbele za Baba.

4. Baba Yetu wa Mbinguni Husikia na Kujibu Sala Zetu

Msituni siku ile katika mwaka 1820, Joseph alijifunza kwamba Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala. Baadaye, Joseph alisema, “Nilikuwa na imani kamili katika kupata mafunuo matakatifu, kama ambavyo awali nilikuwa nimepata” (Historia ya—Joseph Smith 1:29). Mfano wake unatufundisha kwamba tunaweza kumkaribia Baba yetu wa Mbinguni kupitia sala ili kupokea majibu yetu wenyewe.

Joseph alirudia mtindo huu wa sala tena na tena. Alikuwa na imani kwamba Baba wa Mbinguni angelisikia na kujibu sala zake. Alisali kuhusu vitu ambavyo inawezekana umesali juu yake.

Alisali kwa ajili ya hekima (ona Historia ya—Joseph Smith 1:12–13).

Alisali kwa ajili ya ubatizo (ona Historia ya—Joseph Smith 1:68).

Alisali kwa ajili ya uponyaji (ona Mafundisho na Maagano 121:1–4).

Alisali kwa ajili ya wamisionari (ona Mafundisho na Maagano 109:22).

Alisali kwa ajili ya Kanisa, waumini wake, na voingozi wake (ona Mafundisho na Maagano 109:71–76).

Na alisali kwa ajili ya familia yake (ona Mafundisho na Maagano 109:68–69).

Huu ni mtindo kwa ajili yetu Joseph aliotuonesha kwamba sote tunaweza kwenda kwa Baba yetu katika sala?

5. Baba na Mwana Wanatufahamu Kibinafsi

Kutoka Ono la Kwanza, tunajifunza kwamba Viumbe hawa wa Selestia wanatufahamu kibinafsi, jinsi vile walivyomfahamu Joseph. Baba alimwita Joseph kwa jina na, “akimwonesha mwingine kwa kidole,” akasema, “Huyu ni Mwanangu Mpendwa. Msikilize Yeye!” (Historia ya—Joseph Smith 1:17).

Baba na Mwana walifahamu mahitaji, wasiwasi, na matamanio ya Joseph, jinsi vile Wanavyofahamu yetu. Pia wanajua mafanikio na huzuni yetu.

Katika ujana wangu, nilisali kwa ajili ya vitu vingi. Ninapotazama nyuma sasa, baadhi ya vitu hivyo si muhimu sana. Lakini vilikuwa muhimu kwangu wakati huo, na nilielewa tangu umri mdogo kwamba nilikuwa na Baba wa Mbinguni ambaye alinisikiliza mimi. Sikupata siku zote jibu la haraka, lakini nilihisi kwamba katika wakati Wake na njia Yake Angejibu ombi langu katika njia iliyokuwa sawa kwa ajili yangu.

Kuwa na imani kwamba Mungu atazungumza nawe. Amini katika hizo hisia ambazo huja ndani kwa kina kwenye moyo wako. Nilikuja kuamini katika sala na kuelewa uwezo wake kwa sababu nilijua uzoefu wa Nabii Joseph Smith. Nilijua kwamba Mungu alijua jina langu na Angenijibu, jinsi vile anavyojua jina lako na atakujibu.

Ushuhuda

Kwa kiasi kikubwa katika miaka 68 ambayo nimeishi duniani, nimeujaribu mtindo wa sala wa Joseph Smith. Kama wafuasi wote wa kweli wa Mwokozi, mimi pia nimepokea majibu kutoka mbinguni. Najua kuwa Yesu ndiye Kristo. Yeye ni Mwana wa Mungu. Alifufuka na yu hai leo. Ana uwezo wa kusamehe dhambi zetu. Kupitia imani, utiifu, na toba yetu, Anaweza kuturejesha salama nyumbani kwetu mbinguni.

Kama Mtume wa Bwana Yesu Kristo na shahidi Wake aliyetawazwa, ninashuhudia kwa uhakika na imani iliyothibitishwa na Roho Mtakatifu kwamba Baba na Mwana walimtokea Joseph katika Msitu Mtakatifu. Ninaomba kwamba mtafuata mtindo wa Joseph wa kusali, mjifunze kweli alizojifunza, na muimarishe imani yenu katika Baba wa Mbinguni na Mwana Wake, Yesu Kristo.

Muhtasari

  1. “Dhamira ya Wasichana,” youngwomen.ChurchofJesusChrist.org.

  2. “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Liahona, Mei 2017, 145.

  3. “Simulizi za Joesph Smith kuhusu Ono la Kwanza,” josephsmithpapers.org.

Kielelezo na David Malan

Kielelezo na Kendall Ray Johnson