2020
Siku za Baadaye za Kanisa: Kuuandaa Ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi
Aprili 2020


Siku za Baadaye za Kanisa: Kuuandaa Ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho linauandaa ulimwengu kwa ajili ya siku ambayo “dunia itajawa na kumjua Bwana” (Isaya 11:9).

Picha
painting of the Savior’s hand

Within Our Grasp, na Jay Bryant Ward, isinakiliwe

Mimi na wewe tunayo nafasi ya kushiriki katika Urejesho unaoendelea wa injili ya Yesu Kristo. Ni ajabu! Haijatengenezwa na mtu. Inakuja kutoka kwa Bwana, ambaye alisema, “Nitaiharakisha kazi yangu katika wakati wake” (Mafundisho na Maagano 88:73). Kazi hii inahalalishwa na tangazo takatifu lililotolewa miaka 200 iliyopita. Iilikuwa na maneno sita pekee: “Huyu ni Mwanangu Mpendwa. Msikilize Yeye!” (Ona Historia ya—Joseph Smith 1:17).

Iikitamkwa na Mwenyezi Mungu, tangazo hilo lilimleta mvulana Joseph Smith kwa Bwana Yesu Kristo. Hayo maneno sita yalianzisha Urejesho wa injili Yake. Kwa nini? Kwa sababu Mungu wetu aliye hai ni Mungu wa upendo! Anawataka watoto Wake wapate kutokufa na uzima wa milele! Kazi kuu ya siku za mwisho ambayo sisi ni sehemu yake ilianzishwa, kwa wakati, kubariki ulimwengu uliokuwa unasubiri na kulia.

Siwezi kuzungumzia Urejesho kimya kimya. Ukweli huu wa historia hakika ni mzuri mno! Ni wa ajabu! Ni wa kustaajabisha! Ni ajabu gani kwamba malaika kutoka mbinguni walikuja kutoa mamlaka na nguvu kwa ajili ya kazi hii?

Leo, kazi ya Bwana katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho inasonga mbele kwa kasi mno. Kanisa litakuwa na siku za baadaye ambazo hazijashuhudiwa, zisizo za kufanananishwa. “Jicho halikuyaona, wala sikio halikuyasikia, … mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao” (1 Wakorintho 2:9; ona pia Mafundisho na Maagano 76:10).

Kumbuka kwamba utimilifu wa huduma ya Kristo upo katika siku za baadaye. Unabii wa Ujio Wake wa Pili haujatimizwa. Tunajiandaa tu kufikia kilele cha kipindi hiki cha mwisho—wakati Ujio wa Pili wa Mwokozi utakuwa uhalisia.

Kukusanya Israeli kutoka Pande Zote Mbili za Pazia.

Kitendo muhimu cha kutangulia Ujio huo wa Pili ni kukusanywa kwa Israeli kulikosubiriwa kwa muda mrefu (ona 1 Nefi 15:18; ona pia ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni). Mafundisho haya ya ukusanyaji ni mojawapo ya mafunzo muhimu ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Bwana ametangaza: Ninawapatia ishara … kwamba nitawakusanya ndani, baada ya kutawanyika kwa muda mrefu, watu wangu, Ee nyumba ya Israeli, na nitaanzisha tena miongoni mwao Sayuni yangu” (3 Nefi 21:1).

Hatufundishi tu kanuni hii, lakini tunaishiriki pia. Tunafanya hivyo tunaposaidia kuwakusanya wateule wa Bwana kutoka pande zote mbili za pazia. Kama sehemu ya takdiri iliyopangwa kwa ajili ya dunia na wakazi wake, jamaa zetu walioaga dunia wanahitaji kukombolewa (ona Mafundisho na Maagano 128:15). Kwa huruma, mwaliko wa “kuja kwa Kristo” (Yakobo 1:7; Moroni 10:32; Mafundisho na Maagano 20:59) unaweza pia kutolewa kwa wale waliofariki bila ufahamu wa injili (ona Mafundisho na Maagano 137:6–8). Sehemu ya matayarisho yao, hata hivyo, inahitaji juhudi za wengine duniani. Tunakusanya chati za ukoo, tunatengeneza shiti za vikundi vya familia, na kufanya kazi ya hekalu kwa niaba ili kukusanya watu kwa Bwana na katika familia zao (ona 1 Wakorintho 15:29; 1 Petro 4:6).

Picha
painting of Salt Lake Temple

Holiness to The Lord, na Jay Bryant Ward, isinakiliwe

Familia zinahitaji kuunganishwa pamoja milele (ona Mafundisho na Maagano 2:2–3; 49:17; 138:48; Historia ya—Joseph Smith 1:39). Muunganiko wa kuweka pamoja unapaswa kuwekwa baina ya akina baba na watoto. Katika wakati wetu, muungano wote, mkamilifu, na ulio kamili wa vipindi vyote, funguo, na nguvu vinapaswa kuunganishwa pamoja (ona Mafundisho na Maagano 128:18). Kwa ajili ya malengo haya matakatifu, mahekalu matakatifu sasa yanapatikana kote ulimwenguni. Ninasisitiza tena ya kwamba ujenzi wa mahekalu haya huenda usibadilishe maisha yenu, lakini huduma yenu hekaluni hakika itabadilisha.

Wakati unakuja ambapo wale wasiomtii Bwana watatengwa na wale wanaomtii (ona Mafundisho na Maagano 86:1–7). Bima yetu salama kabisa ni kuendelea kuwa wastahiki wa kukubaliwa kuingia katika nyumba Yake takatifu. Zawadi kubwa ambayo unaweza kumpa Mungu ni kujilinda kutokana na mawaa kutoka kwenye ulimwengu, mstahiki kuabudu katika nyumba Yake takatifu. Zawadi Yake kwako itakuwa amani na usalama wa kujua kwamba wewe ni mstahiki wa kukutana Naye, wakati wowote siku hiyo itakapofika.

Kando na kazi ya hekaluni, kuja kwa Kitabu cha Mormoni ni ishara kwa ulimwengu mzima kwamba Bwana ameanza kukusanya Israeli na kutimiza maagano Aliyofanya na Ibrahimu, Isaka, na Yakobo (ona Mwanzo 12:2–3; 3 Nefi 21; 29). Kitabu cha Mormoni kinatangaza mafundisho ya kukusanya (ona, kwa mfano, 1 Nefi 10:14). Kinasababisha watu kujifunza kuhusu Yesu Kristo, kuamini injili Yake, na kujiunga na Kanisa Lake. Kwa kweli, kama kusingekuwa na Kitabu cha Mormoni, mkusanyiko ulioahidiwa wa Israeli haungetokea.

Kazi ya umisionari pia ni muhimu katika kukusanya huko. Watumishi wa Bwana husonga mbele wakihubiri Urejesho. Katika mataifa mengi waumini na wamisionari wetu wamewatafuta wale ambao ni Israeli iliyotawanyika; wamewawinda kutoka kwenye “pango za majabali” (Yeremia 16:16); na wamewavua, kama katika siku za kale.

Kazi ya umisionari inawaaunganisha watu kwenye agano Bwana alilofanya na Ibrahimu zamani:

“Nawe utakuwa baraka kwa uzao wako baada yako, ili katika mikono yao wataichukua huduma hii na Ukuhani kwa mataifa yote;

“Nami nitawabariki wao kupitia jina lako; kwani kadiri wengi watakavyoipokea Injili hii wataitwa kwa jina lako, nao watahesabiwa kuwa uzao wako, na watainuka na kukubariki, kama baba yao” (Ibrahimu 2:9–10).

Kazi ya umisionari ni mwanzo tu wa baraka hiyo. Kutimizwa, kukamilishwa, kwa baraka hizo huja wakati ambapo wale ambao wameingia katika maji ya ubatizo wanakamilisha maisha yao kufikia kiasi cha wao kuingia katika hekalu takatifu. Kupokea endaumenti huko kunawaunganisha waumini wa Kanisa katika agano la Ibrahimu.

Uamuzi wa kuja kwa Kristo si suala la kieneo; ni suala la kujitolea kwa mtu binafsi. Waumini wote wa Kanisa wanaweza kupata mafundisho, ibada, funguo za ukuhani, na baraka za injili, bila kujali eneo lao. Watu wanaweza “kuletwa kwenye ufahamu wa maarifa ya Bwana” (3 Nefi 20:13) bila ya kuondoka kwenye ardhi zao za nyumbani.

Kweli, katika siku za mwanzo za Kanisa, uongofu kawaida ulimaanisha uhamiaji pia. Lakini sasa kukusanyika kunafanyika katika kila taifa. Bwana ametangaza kujengwa kwa Sayuni (ona Mafundisho na Maagano 6:6; 11:6) katika kila ufalme ambapo Amewapa Watakatifu Wake uzao wao na utaifa. “Mahali pa kukusanyika kwa Watakatifu wa Brazili ni Brazili; mahali pa kukusanyika kwa Watakatifu wa Nigeria ni Nigeria; mahali pa kukusanyika kwa Watakatifu wa Korea ni Korea. Sayuni ni “walio safi moyoni” (Mafundisho na Maagano 97:21). Ni popote walipo Watakatifu wenye haki.

Usalama wa kiroho daima utategemea jinsi mtu anavyoishi, si pahali mtu anapoishi. Ninaahidi ya kwamba kama tutafanya kadri ya uwezo wetu kuwa na imani katika Yesu Kristo na kufikia uwezo wa Upatanisho Wake kupitia toba, tutapata uelewa na nguvu za Mungu kutusaidia kupeleka baraka za injili ya urejesho ya Yesu Kristo katika kila taifa, ukoo, ndimi, na watu na kuuandaa ulimwengu kwa Ujio wa Pili wa Bwana.

Ujio wa Pili

Bwana atarudi kwenye ile nchi ambayo Aliifanya kuwa takatifu kupitia misheni Yake huko katika maisha ya kufa. Kwa shangwe, Atarudi tena Yerusalemu. Akiwa amevalia mavazi ya rangi nyekundu ambayo yanaashiria damu yake, ambayo ilivuja kutoka kwenye kila kinyweleo, Atarudi kwenye lile Jiji Takatifu (ona Mafundisho na Maagano 133:46–48). Huko na kwingineko, “utukufu wa Bwana utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja” (Isaya 40:5; ona pia Mafundisho na Maagano 101:23). “Jina lake litaitwa, Ajabu, Mshauri, Mwenyezi Mungu, Baba asiye na mwisho, Mwana Mfalme wa Amani” (Isaya 9:6).

Atatawala kutoka miji miwili mikuu ya dunia: mmoja katika Yerusalemu ya kale (ona Zakaria 14) na mwingine katika Yerusalemu Mpya “iliyojengwa juu ya bara la Amerika” (Makala ya Imani 1:10). Kutoka vituo hivi Ataendesha mambo ya Kanisa na Ufalme Wake. Hekalu lingine kisha litajengwa Yerusalemu. Kutoka katika hekalu hilo Atatawala milele kama Bwana wa Mabwana. Maji yatatoka chini ya hekalu. Maji ya Bahari ya Chumvi yataponywa. (Ona Ezekieli 47:1–8.)

Katika siku hiyo Yeye atamiliki majina mapya na kuzungukwa na Watakatifu maalum. Atajulikana kama “Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao ambao [watakuwa] pamoja naye [watakuwa ni wale] walioitwa, na wateule, na waaminifu” (Ufunuo 17:14) kwa kuamini kwao katika maisha ya sasa. Kisha “atatawala milele na milele” (Ufunuo 11:15).

Dunia itarejeshwa katika hali yake ya kiparadiso na kufanywa kuwa mpya. Kutakuwa na mbingu mpya na nchi mpya (ona Ufunuo 21:1; Etheri 13:9; Mafundisho na Maagano 29:23–24).

Ni jukumu letu—ni heshima yetu—kusaidia kuandaa ulimwengu kwa ajili ya siku hiyo.

Picha
Jesus with little boy

Feed My Sheep, na Jay Bryant Ward, isinakiliwe

Kabiliana na Siku za Baadaye kwa Imani

Kwa sasa, hapa na kwa wakati huu, tunaishi katika muda wa matatizo. Matetemeko ya ardhi na tsunami husababisha maafa, serikali zinavunjika, matatizo ya uchumi ni makali, familia inashambuliwa, na viwango vya talaka vinaongezeka. Tuna sababu kuu za kuwa na wasiwasi. Lakini hatuhitaji kuruhusu hofu yetu ichukue nafasi ya imani yetu. Tunaweza kukabiliana na hofu hizo kwa kuimarisha imani yetu.

Kwa nini tunahitaji imani thabiti kama hiyo? Kwa sababu ya siku ngumu zilizo mbele. Ni nadra katika siku za baadaye kuwa rahisi au ya kupendeza kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho mwaminifu. Kila mmoja wetu atajaribiwa. Mtume Paulo alionya kuwa katika siku za mwisho, wale wanaomfuata Bwana kwa bidii “watapata mateso” (2 Timotheo 3:12). Mateso hayo hayo yanaweza ama kukuvunja hata kwenye udhaifu kimya au kukutia motisha wewe kuwa mfano mwema na kuwa jasiri katika maisha yako ya kila siku.

Jinsi unavyokabiliana na majaribu ya maisha ni sehemu ya ukuaji wa imani yako. Nguvu huja wakati wewe unapokumbuka kwamba wewe una asili takatifu, urithi wa thamani usio na kipimo. Bwana amekukumbusha, watoto wako, na wajukuu wako kwamba nyinyi ni warithi kisheria, kwamba mmehifadhiwa mbinguni kwa muda na wakati wenu maalum wa kuzaliwa, kukua na kuwa wapeperushaji wa bendera Yake na watu Wake wa agano. Unapoingia katika njia ya Bwana ya haki, utabarikiwa kuendelea katika wema Wake na kuwa nuru na mwokozi kwa watu Wake (ona Mafundisho na Maagano 86:8–11).

Fanya kila uwezalo kuimarisha imani yako katika Yesu Kristo kwa kuzidisha uelewa wako wa mafundisho yanayofundishwa katika Kanisa Lake lililorejeshwa na kwa kutafuta ukweli bila kutulia. Ukiweka nanga kwenye mafundisho safi, utaweza kusonga mbele kwa imani na msimamo thabiti na kwa furaha kufanya kadri ya uwezo wako wote kutimiza malengo ya Bwana.

Kutakuwa na siku ambapo utavunjika moyo. Kwa hivyo sali kwa ajili ya ujasiri wa kutokata tamaa! Kwa huzuni, baadhi ya wale uliowadhania kuwa marafiki watakusaliti. Na baadhi ya vitu vitaonekana tu kuwa haviko sawa.

Hata hivyo, ninawaahidi ya kwamba mnapomfuata Yesu Kristo, mtapata amani ya kudumu na furaha ya kweli. Unaposhika maagano yako kwa ongezeko la usahihi, na unapolinda Kanisa na ufalme wa Mungu duniani leo, Bwana atakubariki kwa nguvu na busara ya kutimiza kile ambacho ni waumini tu wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaweza kutimiza.

Tunapaswa kuwa wajenzi wa imani binafsi katika Mungu, imani katika Bwana Yesu Kristo na imani katika Kanisa Lake. Tunapaswa kujenga familia na kuunganishwa katika mahekalu matakatifu. Tunapaswa kujenga Kanisa na ufalme wa Mungu hapa duniani (ona Mathayo 6:33). Tunapaswa kujitayarisha kwa ajili ya takdiri yetu takatifu: utukufu, kutokufa, na uzima wa milele (ona Warumi 2:7; Mafundisho na Maagano 75:5).

Ninashuhudia kwa unyenyekevu kwenu kwamba—kama alivyotangaza Nabii Joseph Smith—injili ya Yesu Kristo iliyorejeshwa “itasonga mbele kwa ujasiri, uadilifu, na kwa uhuru, hadi itakapoingia kila bara, kutembelea kila tabia ya nchi, kufagia kila nchi, na kusikika katika kila sikio, hadi pale malengo la Mungu yatakapokamilika, na Yehova Mkuu atakaposema kazi imekwisha” (Historia ya Kanisa, 4:540).

Tumejiingiza katika kazi ya Mwenyezi Mungu. Ninasali kwamba baraka Zake ziwe pamoja na kila mmoja wenu.