2020
Tunaweza Kueneza Nuru ya Injili
Aprili 2020


Vijana Wakubwa

Tunaweza Kueneza Nuru ya Injili

Picha
smiling young adults

Picha na Weston C. Colton

Ujana mkubwa ni wakati wa kukua, fursa nyingi, na nafasi ya kuanza kujenga maisha yako. Na hilo linaweza kuwa la kuchosha mno, kusisimua, na kuogofya yote kwa wakati mmoja (hakika imekuwa hivyo kwetu sisi).

Lakini hata kama hatuna majibu ya maswali yote muhimu ya maisha, kuna kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho—kwamba vijana wakubwa siku zote wamekuwa nguvu muhimu katika Urejesho unaoendelea wa Kanisa la Yesu Kristo.

Katika kupanga sehemu ya mwezi huu, tulizungumza na vijana wengi wakubwa kuhusu kushiriki kwao katika ukusanyaji wa Israeli. Na tumenyenyekezwa sana na upendo wao wa dhati na kujitolea kwao kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo. Bila kujali hali zao, hawa vijana Watakatifu wanaelewa wajibu mkuu walio nao katika kipindi hiki cha mwisho. Katika “Jinsi Vijana Wakubwa Wanavyoleta tofauti katika Urejesho Unaoendelea” katika ukurasa wa 44, unaweza kusoma jinsi vijana wakubwa kutoka India, Hungary, Barbados, Australia, na Marekani wanavyoutayarisha ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi.

Katika makala ya kidijitali pekee, Cesar anatoa umaizi kuhusu jinsi tunavyoweza kupata lengo letu na kuwa viongozi. Lauri anazungumza kuhusu baraka tunazopata kwa kutii ushauri wa nabii. Vijana wengine wakubwa wanashiriki uzoefu wao wa huduma ya hekaluni, kuhudumu, historia ya familia, na kazi ya umisionari. Na tunashiriki mfano kutoka kwa kijana mkubwa kutoka New Caledonia unaoonesha jinsi waumini wa umri mdogo wanavyofanya kazi ya Bwana katika maeneo madogo ya Kanisa.

Popote ulipo na bila kujali hali yako ilivyo, unaweza kuchangia pakubwa katika kukusanya Israeli zaidi ya vile unavyodhania. Kama vijana wakubwa, sisi ni viongozi wa baadaye wa Kanisa hili. Na cheche ya juhudi zetu leo itawaka na kueneza nuru ya injili kote ulimwenguni kesho.

Kwa moyo wa dhati,

Chakell Wardleigh na Mindy Selu

Wahariri wa Magazeti ya Kanisa sehemu ya vijana wakubwa