2020
Picha Nne kutoka Wiki ya Pasaka
Aprili 2020


Picha Nne kutoka Wiki ya Pasaka

Picha
A crown of thorns.

“Ufalme Wangu sio wa ulimwengu huu” (Yohana 18:36).

Taji ya Miiba

Ona Mathayo 27:29; Marko 15:17; Yohana 19:2.

Wanajeshi Warumi walimvisha Mwokozi taji ya miiba. “Pengine kitendo hiki cha ukatili kilikuwa jaribio la ukaidi la kuiga kumvika heshima mfalme mkuu juu ya kichwa Chake. … Ni uchungu ulioje, ukizingatia kwamba miiba iliashiria kero ya Mungu wakati alipoilaani ardhi kwa ajili ya Adamu kwamba kuanzia wakati huo ingezaa miiba. Lakini kwa kuivaa taji hiyo, Yesu aliibadili miiba kuwa ishara ya utukufu Wake” (Rais James E. Faust, Apr. 1991 mkutano mkuu).

Joho la Rangi ya Zambarau

Ona Mathayo 27:28; Marko 15:17; Yohana 19:2.

Zambarau ilikuwa rangi ya kifalme, na wanajeshi walimvisha Yesu Kristo joho hili kwa dhihaka kwa sababu alikuwa amekiri kuwa mfalme wa Wayahudi. Bila shaka, kwa kweli Yeye ni zaidi ya hilo—Yeye ni “Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana” (1 Timotheo 6:15; Ufunuo 19:16).

Picha
Oil on canvas painting of Christ standing with hands bound in front, and dressed in a purple robe. Pilate is seated and dressed in gold and white. Artist signed and dated painting in lower left hand corner.

“Damu inatiririka kutoka kwenye kila kinyweleo, mateso yake yatakuwa makuu” (Mosia 3:7).

Kisindiko cha Mzeituni

Ona Mathayo 26:36; Marko 14:32; Luka 22:39–40; Yohana 18:1.

“Ni ishara ya kina kwamba ‘damu [ilitiririka] kutoka kila kinyweleo’ [Mosia 3:7] wakati Yesu akiteseka katika Gethsemane, mahali pa kisindiko cha mzeituni. Ili kuzalisha mafuta ya mzeituni nyakati za Mwokozi, mizeituni kwanza ilipondwa kwa kuwekewa jiwe kubwa juu yake. “Rojorojo” iliyofanyika kisha iliwekwa kwenye vikapu laini vya kusukwa vyenye matundu, ambavyo viliwekwa kimoja juu ya kingine. Uzito wa mrundikano huu ulikamua mafuta ya kwanza na safi. Halafu mkamuo ukaongezwa kwa kuwekewa nguzo kubwa au gogo juu ya mrundikano ule wa vikapu, na kutoa mafuta mengi zaidi. Mwishoni kabisa, ili kutoa mafuta ya mwisho, nguzo au gogo liliwekewa mawe juu yake kwenye upande mmoja ili kuleta mkandamizo na kukamua zaidi. Na ndiyo, mafuta ni mekundu kama damu wakati yanatoka” (Mzee D. Todd Christofferson, Okt. 2016 mkutano mkuu).

Picha
A stone olive press

“Hayupo hapa, amefufuka” (Luka 24:6).

Kaburi Wazi.

Ona Mathayo 28:1–8; Yohana 20:1–18.

“Kaburi wazi asubuhi ile ya kwanza ya Pasaka lilikuwa jibu la swali la Ayubu, “Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena?’ [Ayubu 14:14]. Kwa wote wanaoisikia sauti yangu, ninatangaza, Mtu akifa, atakuwa hai tena. Tunajua, kwani tuna nuru ya ukweli uliofunuliwa” (Rais Thomas S. Monson, “Amefufuka!” Apr. 2010 mkutano mkuu).

Picha
Jesus Christ's empty tomb - set at Goshen, Utah

Kielelezo cha taji ya miiba na Dilleen Marsh

Kristo na Pilato, na Marcus Vincent, kwa hisani ya Jumba la Makumbusho ya Historia ya Kanisa

Picha ya kisindiko cha mizeituni kutoka Getty Images