2019
Ninapataje marafiki ambao wana viwango vizuri?
Oktoba 2019


Maswali & Majibu

“Ninapataje marafiki ambao wana viwango vizuri?”

Ukarimu Ni Muhimu

Waonyeshe upendo na kuwa mkarimu. Onyesha kwamba unawajali na unajali furaha yao. Ikiwa hawaonyeshi kwamba wanakujali na si wakarimu, pengine hutataka kuendelea kutafuta urafiki huo.

Madi B., miaka 15, Arizona, Marekani

Ishi Viwango Vyako

Kuwa mfano wa kuishi viwango vyako. Na ikiwa una marafiki ambao hawana viwango sawa na vyako, waonyeshe kwamba wao ni wa kipekee mbele za Mungu. Yesu alimfundisha kila mmoja na kuwafundisha kufuata njia Zake.

Bernard B., miaka 19, Palawan, Ufilipino

Shiriki injili

Unaweza kupata marafiki wapya wenye viwango vizuri kwa kwenda kufundisha pamoja na wamisionari. Wanawajua vijana kadhaa wanaohitaji rafiki Kanisani.

Mzee Quintanilla, miaka 20, misheni ya Barbados Bridgetown

Omba kwa ajili ya Rafiki Zako

Ninaomba sana ili kuona ikiwa rafiki zangu ni marafiki sahihi ambao wanaweza kunisaidia kuinua viwango vyangu na ushuhuda wangu wa Yesu Kristo.

Imanol M., miaka 18, Chihuahua, Mexico

Mungu Atakusaidia

Nimegundua kwamba ikiwa nitaenda nje ya njia yangu kutafuta watu ambao wanaonesha nuru ya Kristo, hilo limeleta tofauti kubwa. Baba wa Mbinguni anafahamu hamu yako na ikiwa utafanya sehemu yako, ndipo Yeye atajibu maombi hayo.

Olivia T., miaka 18, Utah, Marekani