2019
Nini mtazamo wa Kanisa juu ya mazingira?
Oktoba 2019


Nini mtazamo wa Kanisa juu ya mazingira?

Neno la msingi katika kuelewa mtazamo wetu juu ya mazingira ni usimamizi. Haimaanishi kwamba watu wanamiliki dunia na wanaweza kuitumia vyovyote wanavyopenda bali tunawajibika kwa jinsi tunavyotumia rasilimali zake (ona Mafundisho na Maagano 104:13–15). Japokuwa “viko vya kutosha na kubaki” (Mafundisho na Maagano 104:17), Mungu anataka tutumie rasilimali za dunia kwa hekima (ona Mafundisho na Maagano 59:20).

Mungu aliumba dunia na kutangaza uumbaji Wake kuwa “mwema sana” (ona Mwanzo 1:1, 31). Dunia hii iliumbwa kuwapa hifadhi watoto wa Mungu kama sehemu ya mpango Wake wa wokovu. Dunia haina budi kusafishwa na kupokea utukufu wa selestia (ona Mafundisho na Maagano 88:18–19).

Mungu aliumba dunia si tu itumike bali pia ya kupendeza. Vitu vya dunia “vimefanywa kwa faida na matumizi ya mwanadamu, kwa kuridhisha jicho na kufurahisha moyo,” vilevile kuchangamsha nafsi” (Mafundisho na Maagano 59:18–19).

Tunapaswa kumheshimu Mungu kwa kutambua uumbaji Wake, kuonyesha shukrani kwa uumbaji huo, na kujitahidi kuufanya kuwa wa kupendeza. Tunapaswa kutunza rasilimali, kulinda asili, na kuepuka uchafuzi na takataka.